Serikali ya CCM mmeamua kutusaliti wananchi, Tunaenda kukumbwa na njaa kubwa hali ni mbaya

Mfuko wa mbolea umepanda hadi 130,000+, ni wapi serikali imesaidia kwenye hilo? Huyu mleta uzi ni wapi amewanunulia mbolea wakulima ili waogope kuuza nje kwa faida?
Sasa tuizungumzie serikali ndiyo yenye lawama. Sera mbovu kabisa.
 

Kama wakulima wanauza kwa bei isiyo na faida huo ni ujinga wao, ila wakulima wajue kwa sasa chakula kinauzwa bei nzuri. Ni juu yao kuuza bei juu ili waondokane na umasikini, au waendelee kuwa wajinga wakati wenzao wanafaidika.
 
Huko tuendako kutakuwa hakuna chakula kabisa.

Serikali inatuangusha.
 
Sasa tuizungumzie serikali ndiyo yenye lawama. Sera mbovu kabisa.

Hapo sawa, mambo ya kusema chakula kinaenda nje huku serikali haimsaidii mkulima kwenye pembejeo sio sahihi. Serekali inatakiwa inunue hicho chakula, na sio kuzuia kwenda nje wakati hawajamsaidia yoyote kulima.
 
Mfuko wa mbolea wa kilo 50 unauzwa 125,000 tsh kutoka kuuzwa tsh 60,000 msimu wa 2020/2021

Bei za kulima mashamba zimepanda sababu ya mafuta kupanda

Bei za kusafirisha mazao toka shamba zimepanda mara dufu

Bati,Cement,nondo zimepanda bei

Unataka vyakula viuzwe bei ya chini ili mkulima ashindwe hata kununua baiskeli ya kumsaidia kwenda shamba..?

Kama vyakula vinaenda nje ya nchi maana yake vipo vya kutosha ila wewe ndo unaona Kuna njaa sababu huna pesa ya kununulia
 
Kilimo ni biashara kama biashara nyingine na mazao ni bidhaa kama nyingine ,acheni ujinga wa kupangia watu nini cha kufanya kwenye biashara zao
 
Kumbuka kwamba kama wewe unavyofanya biasha upate faida, kilimo nacho ni biashara. Elewa kwamba sasa ni fursa ya mkulima kupata faida. Zingatia mkulima siyo punda wa taifa. Kama unaona vipi acha kupiga soga hapo mjini nenda kajilimie chakula chako.
Kunywa soda baridiiii
 
Kilimo ni biashara kama biashara nyingine na mazao ni bidhaa kama nyingine ,acheni ujinga wa kupangia watu nini cha kufanya kwenye biashara zao
Kama mimi ni "mjinga" kama unavyosema hapo juu, wewe ni mbombavu kabisa asieweza hata kujua kwamba hakuna biashara yoyote inayofanyika kiholela tu!

Mi nadhani hata kwenye upumbavu hustahili, labda ni kilaza kabisa!
 
Tunalamba asali na tunaupiga mwingi wewe utakuwa sukumagang una chuki na mama yetu.
Nchi inafunguka, royo tua inafanya kazi wacha rule raha
 
Mnawasemea Wakulima kama watu ambao hawajui kitu. Mimi nafanya biashara ya kununua mahindi direct kwa wakulima kwa matumizi ya ndani. na tunapambana na Wakenya. Bei gunia sh 85,0000 hadi 95,000 analipwa mkulima bila Dalali. Miaka ya nyuma angekuwa analamba 40,000. Acha wapone majeraha ya huko nyuma. Labda ninacho weza kuishauri serikali ni kwanza kuwahamasisha Wakulima waweke akiba ya chakula. Pili serikali inununue mahindi haraka kwa bei ya soko kwa wakulima na kuhifadhi kwenye reserve yake. Tuachane na habari ya kufunga mipaka karne hii ya kilimo biashara. Mahindi bado yapo ukipambana na bei ya soko ila kufikia September kazi ipo.
 
Nani asiekujua chawa?

Hapo unajita awamu ya 6 utafikiri wewe ni miongoni mwao!

Muuonee huruma mamako kule kijijini kwa maisha anayoishi
Sisi ni Kazi tuu nyie endeleeni na uzushi 👇
 

Attachments

  • Screenshot_20220717-155926.png
    86.8 KB · Views: 7
  • Screenshot_20220717-160208.png
    66.9 KB · Views: 6
  • Screenshot_20220717-155114.png
    173.5 KB · Views: 6
  • Screenshot_20220717-083520.png
    176.9 KB · Views: 5
  • Screenshot_20220715-205205.png
    134.1 KB · Views: 5
Wacheni mama aupige mwingi, chuki zenu mkazikwe nazo Chato kwani mama Nyuki ndie kasababisha Vita ya yukreini na Hali ya hewa mbaya?
Mna chuki Sana nyie sukumagang hamjui biashara huria na mama ameifungua nchi wakulima waliteseka Sana miaka sita Sasa wauze watajirike wasizuiwe...
Hatuna njaa nchi hii tuna akiba ya mazao miaka yote mama Nyuki atakayokaa madarakani
 
Kumbuka kwamba kama wewe unavyofanya biasha upate faida, kilimo nacho ni biashara. Elewa kwamba sasa ni fursa ya mkulima kupata faida. Zingatia mkulima siyo punda wa taifa. Kama unaona vipi acha kupiga soga hapo mjini nenda kajilimie chakula chako.
Umejibu kilamba asali Sana, hebu shushia na maji ya Nazi hapo Mkunazini maana baa la njaa litawatesa wasukumagang peke Yao kwakuwa hawajui mkulima ndio muda wake wa kulamba asali huu
 
Waachwe wauze Mali yao wanavyopenda hata wakigawa bure hiyo ni Mali yao !! Msitupangie hamtusaidii mbolea wala pembejeo !! Kila MTU ayasikie maumivu ya vita vya Ukraine !!
 
Acha chuki na wivu kwa mama yetu anatulambisha asali
Lambeni tu mkuu maana kuna jitu linalaza mimacho utafikri limewekewamo! Ji zamu yenu hii. Nasikia kuna trillion 1.2 mmelamba tena!
 

Uko sahihi, hiki usemacho ndio msimamo wangu kuhusu wakulima, kwani hata mimi ni mkulima. Anayeona chakula kunapungua na yeye akalime ili kisipungue.
 
Unafahamu Hali ya uzalishaji hizo nyakati unazotaja?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…