Sasa tuizungumzie serikali ndiyo yenye lawama. Sera mbovu kabisa.Mfuko wa mbolea umepanda hadi 130,000+, ni wapi serikali imesaidia kwenye hilo? Huyu mleta uzi ni wapi amewanunulia mbolea wakulima ili waogope kuuza nje kwa faida?
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Sasa tuizungumzie serikali ndiyo yenye lawama. Sera mbovu kabisa.Mfuko wa mbolea umepanda hadi 130,000+, ni wapi serikali imesaidia kwenye hilo? Huyu mleta uzi ni wapi amewanunulia mbolea wakulima ili waogope kuuza nje kwa faida?
Pale iringa yale mavihenge mawili yamechukuliwa na mkenya amejaza mahindi mle na anakobokoa kisha anapaki unga kwenda kuuza kwao!
Wanaofikri mkulima ndio anafaidika hawana akili! Mkulima hakuna chochote anachofaidika. Wanaofaidika ni walanguzi wanaoenda kulangua mahindi kwa wakulima kisha wao huuza kwa profit kubwa kubwa!
Hata mahindi yakiuzwa debe kwa laki 1 hakuna chochote mkulima wa jembe la mkono hapa tz atafaidi!
Njaa ikianza wakwanza kulalamika watakuwa ni hao wakulima.
Sasa tuizungumzie serikali ndiyo yenye lawama. Sera mbovu kabisa.
Kilimo ni biashara kama biashara nyingine na mazao ni bidhaa kama nyingine ,acheni ujinga wa kupangia watu nini cha kufanya kwenye biashara zaoHapana, si hivyo.
Nadhani hukuelewa alichomaanisha yeye. Hajakataa wakulima kuuza kwa faida kwa yeyote yule iwe ndani au nje ya nchi. Lakini hili halifanyiki holela tu. Hakuna serikali popote duniani inayoruhusu namna hiyo ya ufanya biashara.
Kama wakulima wenyewe wanaouza mazao yote, hata akiba ya chakula chao, njaa ikiingia nchini, hilo siyo janga?
Kunywa soda baridiiiiKumbuka kwamba kama wewe unavyofanya biasha upate faida, kilimo nacho ni biashara. Elewa kwamba sasa ni fursa ya mkulima kupata faida. Zingatia mkulima siyo punda wa taifa. Kama unaona vipi acha kupiga soga hapo mjini nenda kajilimie chakula chako.
Kama mimi ni "mjinga" kama unavyosema hapo juu, wewe ni mbombavu kabisa asieweza hata kujua kwamba hakuna biashara yoyote inayofanyika kiholela tu!Kilimo ni biashara kama biashara nyingine na mazao ni bidhaa kama nyingine ,acheni ujinga wa kupangia watu nini cha kufanya kwenye biashara zao
Tunalamba asali na tunaupiga mwingi wewe utakuwa sukumagang una chuki na mama yetu.Serikali ya CCM chini ya Rais Samia Imeamua kwa makusudi kutuacha watanzania na kuangali maslai yao
Hali ni mbaya sana mtaani vyakula bei hazishikiki
Vyakula vinavushwa mipakani na kwenda nje ya nchi sisi hatupati
imefika hatua sasaivi mabwenyenye wananunua mzigo bado upo shambani wanavuna na kupeleka nje ya nchi, Kilimanjaro kuna njaa lakini mahindi yanapitia hapohapo kwenda kenya
Sasaivi unga wa sembe kilo moja 2000 hii haijawai kutokea kabisa
mchele 2400 kilo
Serikali ipo kimya tu wao wanahela za kula
CCM imeamua kutusaliti, sasaivi sokoni hatuoni mahindi yanatoka kwenye stock yanawekwa kwenye maroli yanavuka boda
tukisema hivi wanaona kama tunatania maana wao hali ya mtaani hawaijui
Sawa bwana
Mnawasemea Wakulima kama watu ambao hawajui kitu. Mimi nafanya biashara ya kununua mahindi direct kwa wakulima kwa matumizi ya ndani. na tunapambana na Wakenya. Bei gunia sh 85,0000 hadi 95,000 analipwa mkulima bila Dalali. Miaka ya nyuma angekuwa analamba 40,000. Acha wapone majeraha ya huko nyuma. Labda ninacho weza kuishauri serikali ni kwanza kuwahamasisha Wakulima waweke akiba ya chakula. Pili serikali inununue mahindi haraka kwa bei ya soko kwa wakulima na kuhifadhi kwenye reserve yake. Tuachane na habari ya kufunga mipaka karne hii ya kilimo biashara. Mahindi bado yapo ukipambana na bei ya soko ila kufikia September kazi ipo.
Sisi ni Kazi tuu nyie endeleeni na uzushi 👇Nani asiekujua chawa?
Hapo unajita awamu ya 6 utafikiri wewe ni miongoni mwao!
Muuonee huruma mamako kule kijijini kwa maisha anayoishi
Wacheni mama aupige mwingi, chuki zenu mkazikwe nazo Chato kwani mama Nyuki ndie kasababisha Vita ya yukreini na Hali ya hewa mbaya?Tulishauri mwaka huu mavuno ni kidogo wafunge mipaka kwani hata soko la ndani tu linatosha wakashupaza vichwa vyao, mavuno yakiwa mengi watu wauze nje ni sawa lakini mwaka wenye mavuno kidogo nao wauze nje kipindi chote hapana, Burundi kuuza mahindi, maharage, mtama na muhogo ni uhujumu uchumi kwa sasa, uganda kazuia hakuna kuuza chochote nje isipokua ni ruhusa kununua, na kuingiza ndani, Rwanda kazuia kabisa hakuna kutoa hata kiazi, wizara ya kilimo ipo ipo tu imekalia siasa, hakuna usalama kama nchi haina chakula cha kutosha na mkumbuke dunia nzima mavuno kwa mwaka ulioisha yalikua hafifu sana, viongozi hawachukui maamuzi simply sababu wao na familia zao njaa haitowakumba.
Acha chuki na wivu kwa mama yetu anatulambisha asaliNaomba niseme tu hili mama hakuna kitu kabisa! Linaburuzwa na wanaume! Ngoja wakulima wauze kila kitu nchi iingie kwenye baa la njaa labda akili italikaa sawia!
Kwa watoto wa marehemu kutoka Chato pekee ndio wanatesekaKupanda kwa maisha na mfumko wa bei kwa bidhaa mbalimbali, inawahusu na Mataga au ni kwa wanachadema tu?
Umejibu kilamba asali Sana, hebu shushia na maji ya Nazi hapo Mkunazini maana baa la njaa litawatesa wasukumagang peke Yao kwakuwa hawajui mkulima ndio muda wake wa kulamba asali huuKumbuka kwamba kama wewe unavyofanya biasha upate faida, kilimo nacho ni biashara. Elewa kwamba sasa ni fursa ya mkulima kupata faida. Zingatia mkulima siyo punda wa taifa. Kama unaona vipi acha kupiga soga hapo mjini nenda kajilimie chakula chako.
We jamaaMay 2020 unga wa mahindi kilo moja ilikuwa 2500. Unasemaje haijawahi kutokea?
Waachwe wauze Mali yao wanavyopenda hata wakigawa bure hiyo ni Mali yao !! Msitupangie hamtusaidii mbolea wala pembejeo !! Kila MTU ayasikie maumivu ya vita vya Ukraine !!Nani kakwambia mkulima ndiye anayenufaika na biashara hii ya chakula kupelekwa nnje ya nchi?!??
Njoo huku Kusini (Mtwara na Lindi) uone jinsi tunavyonunua ufuta kilo moja tsh 1100 - 2000 kutoka kwa mkulima na sisi tunauza tsh 3190 kwa kilo.
Mkulima ananufaikaje na bei hiyo ya 3190 kwa kilo!!??
Mnapenda kuongea vitu ambavyo hamvifahamu.
Wakulima wanaonufaika na bei kubwa ya mazao ni wakulima wakubwa tuu.
Wanufaika wakubwa wa kupanda kwa bei ya mazao ni watu wa kati (madalali) ma wafanyabiashara wa mazao.
Nikupe mfano mmoja,kuna kijiji ambacho wakazi wake walilima ufuta na kupata mavuno mazuri lakini changamoto yao ni kuwa umbali wa kutoka hapo kijijini mpaka kwenye mnada wa ufuta ni km 29.
Hakuna usafiri wa mabasi.
Mimi nimeenda huko nikawaambia nanunua ufuta kwa tsh 1200 kwa kilo,wamekubali kuliko kusubiri kwenda mnada ambao watauza kwa utaratibu wa stakabadhi ghalani itakayowachukua wiki kupata fedha yao.
Umeona mkulima anavyoteseka hapo sasa!!???
Lambeni tu mkuu maana kuna jitu linalaza mimacho utafikri limewekewamo! Ji zamu yenu hii. Nasikia kuna trillion 1.2 mmelamba tena!Acha chuki na wivu kwa mama yetu anatulambisha asali
Mnawasemea Wakulima kama watu ambao hawajui kitu. Mimi nafanya biashara ya kununua mahindi direct kwa wakulima kwa matumizi ya ndani. na tunapambana na Wakenya. Bei gunia sh 85,0000 hadi 95,000 analipwa mkulima bila Dalali. Miaka ya nyuma angekuwa analamba 40,000. Acha wapone majeraha ya huko nyuma. Labda ninacho weza kuishauri serikali ni kwanza kuwahamasisha Wakulima waweke akiba ya chakula. Pili serikali inununue mahindi haraka kwa bei ya soko kwa wakulima na kuhifadhi kwenye reserve yake. Tuachane na habari ya kufunga mipka karne hii ya kilimo biashara. Mahindi bado yapo ukipambana na bei ya soko ila kufikia September kazi ipo.
Unafahamu Hali ya uzalishaji hizo nyakati unazotaja?Wakati awamu ya nne, mkulima alipewa uhuru wa kuuza anapotaka. Ukawa mwanzo wa mkulima kupata faida. Kila mkulima akavutika kuongeza uzalishaji kwa kuongeza eka anazolima na kuongeza ubora kv mbolea, mbegu bora, kupanda kwa vipimo nk.
Faida katika kilimo ikawavutia waajiriwa kuingia ktk kilimo na baadaye wafanyabiara wakaingia. Hapo kilimo kikawa cha biashara na uzalishaji ukaongezeka maradufu.
Awamu ya tano ikaingia na mwelekeo kama wa mleta mada. Bei ya mazao ya chakula ikaporomoka. Wafanya biashara na waajiriwa wakajichomoa katika kilimo. Wakulima original wakapunguza eka na ubora wa kilimo mwaka hadi mwaka. Uzalishaji wa mazao ya chakula ukaporomoka sana.
Kwa mtu mwenye vision lazima atapenda model ya wamu ya nne. Mimi naipenda na mama anaipenda pia. Sababu inapaisha uzalishaji, mauzo nje ya nchi, mkulima na nchi inafaudika kwa uendelevu.
Kwa ambaye hana vision ataona karibu tu kama mtoa mada. Hilo lilitokea ktk awamu ya tano na kilimo cha mazao ya chakula kikakosa maana. Uzalishaji ukaporomoka vibaya. Mwendelezo huo ungetufikisha mahali nchi isijitosheleze kwa chakula na kuanza kuagiza toka nje.
Sera ya mama ya kilimo cha chakula ni BORA ashikilie hapohapo.