NAMBA MOJA AJAYE NCHINI
JF-Expert Member
- Oct 29, 2019
- 9,863
- 20,806
Lengo kuu no lugha za kichina,kiarabu,kifaransa n.k!Serikali kupitia TAMISEMI imetoa fursa kwa Wahitimu wa kidato cha nne mwaka 2023 kuongeza au kufanya marekebisho ya machaguo mapya ya tahasusi (combination) baada ya kuongezwa kwa tahasusi mpya 49 kutoka 16 zilizokuwepo awali na kufanya tahasusi za kidato cha tano kufikia 65.
Akiongea leo Jijini Dar es salaam, Waziri wa TAMISEMI, Mohamed Mchengerwa amesema Serikali kupitia TAMISEMI imekamilisha zoezi la awali la kuingiza kwenye kanzidata taarifa zilizo kwenye fomu za uchaguzi za Wanafunzi kama zilivyojazwa na Wanafunzi wakiwa Shuleni.
“Napenda mtambue kuwa Mabadiliko ya Sera ya Elimu na Mafunzo ya Mwaka 2014 Toleo la Mwaka 2023 na Mitaala ya Elimu kwa Kidato cha Tano yameanza kutekelezwa, ambapo utekelezaji huo umehusisha uanzishaji wa tahasusi mpya 49, kutoka 16 zilizokuwepo awali hadi kufikia tahasusi 65”
“TAMISEMI inatoa fursa kwa Wahitimu kubadili machaguo ili kutoa nafasi kwa Wanafunzi kusoma combination itakayomuandaa kuwa na utaalamu stahiki katika maisha yake ya baadaye hii ni kwakuwa wakati wa ujazaji fomu za machaguo ya awali tahasusi mpya 49 hazikuwepo kwenye orodha na matokeo ya kidato hayakuwa yametoka”
View attachment 2940275View attachment 2940276View attachment 2940277View attachment 2940278
Pia soma: Mtaala wa Elimu 2023 (Kidato V na VI): Tahasusi zafutwa, nyingine kama HGFa, KArCh, KTeFi zaongezwa
Kuwapa vijana exposure ya kuajiriwa kimataifa na kitaifa!!
Lakini Hilo sio swala la msingi kutangazwa na waziri husika!!ungetoka waraka tu was maana!!
Wangetangaza mambo ya maana yanayohusu maslahi kwenye elim!!!