bongo dili
JF-Expert Member
- Feb 13, 2015
- 12,350
- 25,180
Ndo kusema huku napo muarabu alipataka
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Hayo madudu si mnajiandikia wenyewe tu na yanawasuta wenyewe Unamaanishana bunge liko makini au siyo?
Tulia kishasema, mjadala kuhusu IGA yaliyopitishwa bungeni kwa sasa hakuna , kawakumbusha wabunge wote, sasa tungoje kuja kusimamia uendeshaji.
Umeelewa kijana?
Hayo madudu si mnajiandikia wenyewe tu na yanawasuta wenyewe Unamaanishana bunge liko makini au siyo?
Tulia kishasema, mjadala kuhusu IGA yaliyopitishwa bungeni kwa sasa hakuna , kawakumbusha wabunge wote, sasa tungoje kuja kusimamia uendeshaji.
Umeelewa kijana?
Bunge la Mazuzu lililojifanya nunda? Huyu Spika mbovu ndo aliyeiambia serikali ilete sheria haraka wao watapitisha!! Leo anajifanya Bunge limekataa mapendekezo ya serikali?? Bunge lipi? Hili kusanyiko la Wahuni????Pale hakuna Bunge bila wananchi shupavu mithili ya Mwambukusi na wengineo wengi wangepitisha kama kawaida yao.
Waraka wa mtume Paulo kwa wagaratia imeandikwa kila goti litapigwa mpaka muikiri kweliSerikali imeyaondoa mapendekezo yaliyopelekwa Bungeni ya kufanya marekebisho ya sheria ya Sheria ya Mamlaka ya Nchi Kuhusiana na Umiliki wa Maliasili ya mwaka 2017 na Sheria ya Mapitio na Majadiliano Kuhusu Masharti Hasi Katika Maliasili ya nchi ya mwaka 2017 kuwa zisitumike katika miradi ya bandari.
Sheria hizo zilikuwa ni miongoni mwa sheria zilizojumuishwa katika Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria Mbalimbali Na. 2 wa Mwaka 2023, uliokusudia kurekebisha, pamoja na sheria nyingine, sheria hizo mbili ili zisitumike katika uendeshaji wa miradi ya uendeshaji, uendelezaji na bandari.
Taarifa ya kuondolewa kwa marekebisho hayo ilitolewa leo Jumanne, Agosti 29, 2023, na Spika wa Bunge Tulia Ackson.
“Sehemu ya nne inafutwa ambayo inahusu mabadiliko kwenye sheria yetu ile ya marekebisho ya Sheria ya Mamlaka ya Nchi Kuhusiana na Umiliki wa Maliasili ya mwaka 2017, mapendekezo yaliyokuwa yameletwa yanafutwa yote,” alitamka Dk Ackson.
“Sehemu ya tano inahusu marekebisho ya Sheria ya Mapitio na Majadiliano Kuhusu Masharti Hasi Katika Maliasili ya nchi ya mwaka 2017 nayo inafutwa kwa maana ya kwamba Bunge halijaafiki,” aliongeza kiongozi huyo.
Hatua hii ya Bunge inakuja siku tano tangu The Chanzo iongee na Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Katiba na Masuala ya Kisheria, Joseph Mhagama, ambaye alieleza kuwa Kamati yake ilisitisha kupokea maoni juu ya mabadiliko haya yaliyopendekezwa na Serikali kwa sababu ilihitaji maelezo zaidi juu ya maudhui ya mapendekezo hayo.
Marehemu ambaye alipambana sana kuhakikisha maliasili za nchi yetu haziibiwi,na akatunga sheria ambazo leo zimetuokoa.Tena lililoratibiwa na marehemu mmoja alipambana sana kutuletea wajinga bungeni
Mazee ya kugonga meza na kusema ndioooo...Bunge la Mazuzu lililojifanya nunda? Huyu Spika mbovu ndo aliyeiambia serikali ilete sheria haraka wao watapitisha!! Leo anajifanya Bunge limekataa mapendekezo ya serikali?? Bunge lipi? Hili kusanyiko la Wahuni????
Unasikiliza redio gani?Si kweli fuatilia tena
Nunua redio angalau ya shs. 5,000/= uwe unapata habari!Hizi ni habari za Bunge lipi ?
Nop! She can't be trusted!Is she worth trusting ? Or they are re-naming and bring back kivingine ?
Rushwa iliwaziba midomo! Sasa mpaka wazitalike!Bunge linawapoza machungu wananchi kujifanya wanaweza kuigomea Serikali Mbona haikuugomea Mkataba wa DP WORLD wenye Utata mwingi
Hizo ndo siasa za sisiem na wanajua kwa ujinga wetu waTZ hakuna kitu tutawafanya.Unatengeneza tatizo.. Unasikilizia .. Kelele zikizidi unalitatua kisha unasifiwa na kupongezwa..[emoji23] [emoji1544][emoji1550]
...Tulia, Suluhu itapatikana.Nimeabudu mzimu gani?
Kwa hiyo nakukera eeh?😅
Endelea kusubiri nazi chini ya mwarobaini...Tulia, Suluhu itapatikana.
Dawa inachemka.
Anaongelea sheria kuhusu raslimali.Mtoa post unapotosha sheria zote pendekezwa zimepita kama kawaida tena kwa kishindo
Mkuu usiwe unapoteza muda na wapumbavu kama hao ….amekariri mito na bahahri na madini anafikiri kila neno lina maana hiyo hiyo kila sehemu…..hao wapuuze wanapoteza muda wala hajui kinacho endeleaBasView attachment 2732628
Basi ukichopambania ulikuwa hukijui
Punguza kuwaza ushoga.Tech ni group of gays
Mbona wanahangaika?. Ukiona mtu anahangaika mara apitie mlango wa nyuma ujue Hana Nia nzuri.Mazuzu nyie,kila kitu kitaenda vilevile tu
Hili ni Changa la macho tu. Kitu wanachakifanya ni kufanya marekebisho kwenye sheria zingine mbalimbali na kupachika hayo waliyoyataka kuyaweka au kuyaondoa humo kwenye sheria ya Maliasili na kuyaweka huko kwingine....mfanoSerikali imeyaondoa mapendekezo yaliyopelekwa Bungeni ya kufanya marekebisho ya sheria ya Sheria ya Mamlaka ya Nchi Kuhusiana na Umiliki wa Maliasili ya mwaka 2017 na Sheria ya Mapitio na Majadiliano Kuhusu Masharti Hasi Katika Maliasili ya nchi ya mwaka 2017 kuwa zisitumike katika miradi ya bandari.