Serikali yafuta mapendekezo ya kuzifanyia Marekebisho ya Sheria zinazohusu Umiliki wa Maliasili

Serikali yafuta mapendekezo ya kuzifanyia Marekebisho ya Sheria zinazohusu Umiliki wa Maliasili

Tulichoandika wenyewe nn?
Hayo madudu si mnajiandikia wenyewe tu na yanawasuta wenyewe Unamaanishana bunge liko makini au siyo?

Tulia kishasema, mjadala kuhusu IGA yaliyopitishwa bungeni kwa sasa hakuna , kawakumbusha wabunge wote, sasa tungoje kuja kusimamia uendeshaji.

Umeelewa kijana?
 
20230829_205208.jpg
 
Pale hakuna Bunge bila wananchi shupavu mithili ya Mwambukusi na wengineo wengi wangepitisha kama kawaida yao.
Bunge la Mazuzu lililojifanya nunda? Huyu Spika mbovu ndo aliyeiambia serikali ilete sheria haraka wao watapitisha!! Leo anajifanya Bunge limekataa mapendekezo ya serikali?? Bunge lipi? Hili kusanyiko la Wahuni????
 
Serikali imeyaondoa mapendekezo yaliyopelekwa Bungeni ya kufanya marekebisho ya sheria ya Sheria ya Mamlaka ya Nchi Kuhusiana na Umiliki wa Maliasili ya mwaka 2017 na Sheria ya Mapitio na Majadiliano Kuhusu Masharti Hasi Katika Maliasili ya nchi ya mwaka 2017 kuwa zisitumike katika miradi ya bandari.

Sheria hizo zilikuwa ni miongoni mwa sheria zilizojumuishwa katika Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria Mbalimbali Na. 2 wa Mwaka 2023, uliokusudia kurekebisha, pamoja na sheria nyingine, sheria hizo mbili ili zisitumike katika uendeshaji wa miradi ya uendeshaji, uendelezaji na bandari.

Taarifa ya kuondolewa kwa marekebisho hayo ilitolewa leo Jumanne, Agosti 29, 2023, na Spika wa Bunge Tulia Ackson.

“Sehemu ya nne inafutwa ambayo inahusu mabadiliko kwenye sheria yetu ile ya marekebisho ya Sheria ya Mamlaka ya Nchi Kuhusiana na Umiliki wa Maliasili ya mwaka 2017, mapendekezo yaliyokuwa yameletwa yanafutwa yote,” alitamka Dk Ackson.

“Sehemu ya tano inahusu marekebisho ya Sheria ya Mapitio na Majadiliano Kuhusu Masharti Hasi Katika Maliasili ya nchi ya mwaka 2017 nayo inafutwa kwa maana ya kwamba Bunge halijaafiki,” aliongeza kiongozi huyo.

Hatua hii ya Bunge inakuja siku tano tangu The Chanzo iongee na Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Katiba na Masuala ya Kisheria, Joseph Mhagama, ambaye alieleza kuwa Kamati yake ilisitisha kupokea maoni juu ya mabadiliko haya yaliyopendekezwa na Serikali kwa sababu ilihitaji maelezo zaidi juu ya maudhui ya mapendekezo hayo.
Waraka wa mtume Paulo kwa wagaratia imeandikwa kila goti litapigwa mpaka muikiri kweli
 
Bunge la Mazuzu lililojifanya nunda? Huyu Spika mbovu ndo aliyeiambia serikali ilete sheria haraka wao watapitisha!! Leo anajifanya Bunge limekataa mapendekezo ya serikali?? Bunge lipi? Hili kusanyiko la Wahuni????
Mazee ya kugonga meza na kusema ndioooo...
Hayana akili ni kugonga meza na kula posho na kuondoka, waalchache ndio wanaelewa nini kimewapeleka pale ndani.
Tulia huyu nae ni bure kabisa halafu nashangaa siku moja anasema mkataba wa dpw uko sawa na kama una mapungufu atawajibika nikaona huyu ni mpuuzi kabisa, uwajibike wakati utakuwa tayari umetuweka hasara......!
 
Tatizo la Tanzania ni Elimu bora na Umasikini
 
Unatengeneza tatizo.. Unasikilizia .. Kelele zikizidi unalitatua kisha unasifiwa na kupongezwa..[emoji23] [emoji1544][emoji1550]
Hizo ndo siasa za sisiem na wanajua kwa ujinga wetu waTZ hakuna kitu tutawafanya.
 
Serikali imeyaondoa mapendekezo yaliyopelekwa Bungeni ya kufanya marekebisho ya sheria ya Sheria ya Mamlaka ya Nchi Kuhusiana na Umiliki wa Maliasili ya mwaka 2017 na Sheria ya Mapitio na Majadiliano Kuhusu Masharti Hasi Katika Maliasili ya nchi ya mwaka 2017 kuwa zisitumike katika miradi ya bandari.
Hili ni Changa la macho tu. Kitu wanachakifanya ni kufanya marekebisho kwenye sheria zingine mbalimbali na kupachika hayo waliyoyataka kuyaweka au kuyaondoa humo kwenye sheria ya Maliasili na kuyaweka huko kwingine....mfano

Someni hiyo ya PPP ndio yenye maudhui mazuri.

Hatahivyo, kwa kusononeka kabisa, nasema, kuyaondoa mapendekezo hayo, hakuondoi uvunjwaji wa sheria au utumiaji wa Nguvu na mabavu kuhakikisha Waarabu wanakuja kututawala.

Pingeni Dhulumat hii
 
Back
Top Bottom