Serikali yafuta mapendekezo ya kuzifanyia Marekebisho ya Sheria zinazohusu Umiliki wa Maliasili

Serikali yafuta mapendekezo ya kuzifanyia Marekebisho ya Sheria zinazohusu Umiliki wa Maliasili

Serikali imeyaondoa mapendekezo yaliyopelekwa Bungeni ya kufanya marekebisho ya sheria ya Sheria ya Mamlaka ya Nchi Kuhusiana na Umiliki wa Maliasili ya mwaka 2017 na Sheria ya Mapitio na Majadiliano Kuhusu Masharti Hasi Katika Maliasili ya nchi ya mwaka 2017 kuwa zisitumike katika miradi ya bandari.

Sheria hizo zilikuwa ni miongoni mwa sheria zilizojumuishwa katika Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria Mbalimbali Na. 2 wa Mwaka 2023, uliokusudia kurekebisha, pamoja na sheria nyingine, sheria hizo mbili ili zisitumike katika uendeshaji wa miradi ya uendeshaji, uendelezaji na bandari.

Taarifa ya kuondolewa kwa marekebisho hayo ilitolewa leo Jumanne, Agosti 29, 2023, na Spika wa Bunge Tulia Ackson.

“Sehemu ya nne inafutwa ambayo inahusu mabadiliko kwenye sheria yetu ile ya marekebisho ya Sheria ya Mamlaka ya Nchi Kuhusiana na Umiliki wa Maliasili ya mwaka 2017, mapendekezo yaliyokuwa yameletwa yanafutwa yote,” alitamka Dk Ackson.

“Sehemu ya tano inahusu marekebisho ya Sheria ya Mapitio na Majadiliano Kuhusu Masharti Hasi Katika Maliasili ya nchi ya mwaka 2017 nayo inafutwa kwa maana ya kwamba Bunge halijaafiki,” aliongeza kiongozi huyo.

Hatua hii ya Bunge inakuja siku tano tangu The Chanzo iongee na Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Katiba na Masuala ya Kisheria, Joseph Mhagama, ambaye alieleza kuwa Kamati yake ilisitisha kupokea maoni juu ya mabadiliko haya yaliyopendekezwa na Serikali kwa sababu ilihitaji maelezo zaidi juu ya maudhui ya mapendekezo hayo.
Nanyama kimia kwa hili ,naamua kunyamaza , maana katika serikali hii kila jambo huwa hipo na plan A,B,C,D , E, F G
 
Toka maktaba :

Tulisema majaji wamewatupia kitu kizito Bunge, ona sasa kelele zote zile wamegwaya bungeni

TUNAKWENDA MAHAKAMA YA RUFAA

Judgement: Soma kurasa zote 91 ya kesi hii ya kikatiba .....

In the upshot of all this we find this, petition barren of fruits.
Accordingly, the same is hereby dismissed. Since this is a public interest matter, we do not find any justification for granting of costs. We, therefore, make no order as to costs.

Order accordingly.

DATED at MBEYA this 10th August, 2023.

DUNSTAN B. NDUNGURU
JUDGE
10/08/2023

MUSTAFA K. ISMAIL
JUDGE
10/08/2023

ABDI S. KAGOMBA
JUDGE
10/08/2023
Page 91

Endelea kusoma kurasa zone 91 za judgement hii : source :

N.B
Wachambuzi wameona kuwa

Maoni : MTEGO KWA KIKAO CHA BUNGE AGOSTI 2023

Kufuatia maamuzi yaliomo ndani ya hukumu ya Mahakama Kuu kuhusu kesi ya kikatiba iliyofunguliwa mjini Mbeya, Tanzania

Sasa mpira umerudishwa bungeni kuona kama vifungu vilivyokiukwa vya sovereignty ya Tanzania zitatetewa visibadilishwe au vitabadilishwa ili uwekezaji wa Dubai kupitia DP World ufanikiwe.

Bunge la Marekani walipinga uwekezaji wa DP World nchini Marekani mbali ya kutetewa sana na viongozi wa utawala waliokuwa White House wakati huo.

Tukumbuke bunge la Muungano wa Tanzania kizalendo lilijadili muswada wa sheria mpya 30 Juni, 2017

30 Juni 2017​

Bunge laongeza Siku ili kuchambua Miswada mitatu ya Sheria za Ulinzi wa Rasilimali za Taifa​

Bunge limeongeza siku za Mkutano wa Saba hadi tarehe 05 Julai 2017, ili kupitia Miswada mitatu ya sheria inayohusu marekebisho ya Sheria za Madini na ulinzi wa rasilimali za Taifa.

Akitoa maelezo Bungeni, Spika wa Bunge Mhe Job Ndugai alisema kuwa Kamati ya Uongozi ilikutana tarehe 28 Juni, 2017 Jioni, ili kufanya marekebisho ya Ratiba ya Mkutano wa saba Bunge ambao ulitarajiwa kuisha tarehe 30 Juni, 2017 na kukubaliana kuongeza siku tatu za kazi hadi tarehe 5 Julai, 2017 ili kuliwezesha Bunge kupitia Miswada hiyo.

Kufuatia uamuzi huo Mhe Spika alilieleza Bunge kuwa ameunda Kamati ya pamoja itakayopitia Miswada miwili ambayo tayari imeshasomwa kwa mara ya kwanza Bungeni.

Miswada hiyo ni; Muswada wa Sheria ya Mapitio na Majadiliano kuhusu Masharti Hasi katika Mikataba ya Maliasili za Nchi wa Mwaka 2017 [The Natural Wealth and Resources Contracts (Review and Re-Negotiation of Unconscionable Terms)] Bill, 2017];(iii)Muswada wa Sheria ya Mamlaka ya Nchi kuhusiana na Umiliki wa Maliasili wa Mwaka 2017 [The Natural Wealth and Resources (Permmanent Sovereignty)] Bill, 2017].

Mhe Spika alisema kuwa Kamati hiyo ya pamoja itakayo chambua miswada hiyo itaongozwa na Mwenyekiti wa Kamati ya Nishati na Madini Mhe Dotto Biteko na itajumuisha Wajumbe wa Kamati nne za Bunge ambazo ni Kamati ya Nishati na Madini, Kamati ya Ardhi, Maliasili na Utalii, Kamati ya Katiba na Sheria na Kamati ya Sheria Ndogo.

Aidha kwa upande mwingine Mhe Spika alilieleza Bunge kuwa Kamati ya Katiba na Sheria chini ya Uenyekiti wa Mhe Mohamed Omary Mchengerwa itauchambua Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria Mbalimbali wa Mwaka 2017 [The Written Laws (Miscellaneous Amendments) Bill, 2017]

Na sasa miaka mitano baadaye yaani 2023 bunge hili linaona sheria hiyo ya mwaka 2017 inahitaji mabadiliko hivyo kualika wadau wakitazamia mwezi Agosti 2023 wataifanyia mabadiliko ili kuwezesha uwekezaji.
 
Sio kila kitu ndiyoooo. Hata la bandari tuna taka lifutwe
29 Agosti 2023
Dodoma, Tanzania

View: https://m.youtube.com/watch?v=qsZ440OLWKU
Uamuzi wa leo tarehe 29 Agosti 2023 wa Bunge kutotaka kurekebisha sheria ya ulinzi wa maliasilia za nchi ya 2017 inamaana kuwa kuna fundamental breach / obstacle na hivyo kuwepo ugumu mkubwa mkataba wa DP World kutekelezeka na inaweza kuwa mwisho wa ndoto ya Dubai na madalali wa bandari kuchukua bandari zote za Tanganyika milele ikiwemo bandari kuu ya Dar es Salaam.
 
Ni hatua Nzuri sana, sheria itabaki kulinda rasilimali za taifa Kama ilivyokusudiwa.

Wasiwasi wetu isijepitishwa mlango wa jikoni kwa jina jingine.

Lakini……..Je, hii sio kamali inachezwa na mtego kwa watanzania?

Huku Serikali (Rais) imetangaza nia yake ya kuendelea na mchakato wa uwekezaji wa DP World katika Bandari za TZ bila kuweka bayana majibu ya vifungu vinavyolalamikiwa na wadau mbali mbali,, huku bunge linapiga chini ombi la Serikali (Rais?!) La kubadiri Sheria ili kuwezesha wawekezaji ?

Wakati huo huo Usalama kuna mabadiriko makubwa?!

Feels like a movie on HBO.
 
Muone mjinga huyu.

TEC wanahusikaje hapo? Hata mimi niliwasilisha maoni yangu bungeni kuwa hakuna haja ya kufanya haya mabadiliko kwa kuwa masuala ya uwekezaji kwenye Bandari hayahusiani na Sheria hizi.
Sawa, basi na wewe Hongera
 
Naona wame amka. Sio kila kitu ndiyoooo. Hata la bandari tuna taka lifutwe. Hatuwezi kuuza kila kitu kwa wageni ati kisa walioko bandarini ni wezi!!! Hivi hatuna soni?? Nani kaweka wezi bandarini kama sio Ccm na serikali yake??
Mpaka leo wale wa ufafanuzi hawajarudi kujibu hili
 
Serikali imeyaondoa mapendekezo yaliyopelekwa Bungeni ya kufanya marekebisho ya sheria ya Sheria ya Mamlaka ya Nchi Kuhusiana na Umiliki wa Maliasili ya mwaka 2017 na Sheria ya Mapitio na Majadiliano Kuhusu Masharti Hasi Katika Maliasili ya nchi ya mwaka 2017 kuwa zisitumike katika miradi ya bandari.

Sheria hizo zilikuwa ni miongoni mwa sheria zilizojumuishwa katika Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria Mbalimbali Na. 2 wa Mwaka 2023, uliokusudia kurekebisha, pamoja na sheria nyingine, sheria hizo mbili ili zisitumike katika uendeshaji wa miradi ya uendeshaji, uendelezaji na bandari.

Taarifa ya kuondolewa kwa marekebisho hayo ilitolewa leo Jumanne, Agosti 29, 2023, na Spika wa Bunge Tulia Ackson.

“Sehemu ya nne inafutwa ambayo inahusu mabadiliko kwenye sheria yetu ile ya marekebisho ya Sheria ya Mamlaka ya Nchi Kuhusiana na Umiliki wa Maliasili ya mwaka 2017, mapendekezo yaliyokuwa yameletwa yanafutwa yote,” alitamka Dk Ackson.

“Sehemu ya tano inahusu marekebisho ya Sheria ya Mapitio na Majadiliano Kuhusu Masharti Hasi Katika Maliasili ya nchi ya mwaka 2017 nayo inafutwa kwa maana ya kwamba Bunge halijaafiki,” aliongeza kiongozi huyo.

Hatua hii ya Bunge inakuja siku tano tangu The Chanzo iongee na Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Katiba na Masuala ya Kisheria, Joseph Mhagama, ambaye alieleza kuwa Kamati yake ilisitisha kupokea maoni juu ya mabadiliko haya yaliyopendekezwa na Serikali kwa sababu ilihitaji maelezo zaidi juu ya maudhui ya mapendekezo hayo.
Pascal Mayalla ona faida za waraka, zinaanza kuonekana
 
Naona wame amka. Sio kila kitu ndiyoooo. Hata la bandari tuna taka lifutwe. Hatuwezi kuuza kila kitu kwa wageni ati kisa walioko bandarini ni wezi!!! Hivi hatuna soni?? Nani kaweka wezi bandarini kama sio Ccm na serikali yake??
Tangu lini uwekezaji ukawa uuzwaji?

Wapi na lini Bandari imeuzwa? Tupe uthibitisho
 
Nchi imejaa wajinga kila kona. Bandari huwezi kuiweka kwenye kundi la maliasili, yale maji ndio yanaingia kwenye kundi hilo.

Meli ya mzigo inayoleta magari kutoka Japan utaiweka vipi kwenye kundi la rasilimali za Taifa?.

Meli ya mzigo inayoleta mafriji na vifaa vya majumbani utaiweka vipi katika kundi la raslimali za Taifa?.

Zile mashine za kushusha na kupakia makontena utaziweka vipi kwenye kundi la rasilimali?. Zote hizi ni juhudi za wanaharakati kutaka kusema kuwa bandari yetu ni sehemu ya rasilimali, hizi ni akili za kipuuzi kabisa.
Yaani bandari inajengwa wapi!?
 
Ndo kusema walitaka kumaliza kabisa raslimali zetu bila tatizo na kuzisafirisha kupitia bandari yetu.
 
Sasa itskuwaje DI PII kile kipengele Cha katatulia migogoro Aflika ya kuthini kw Shelia za uingeleza? Maana hizi sheria zinabana kuwa migogoro kama hiyo itatuliwe Papaapa mu TANZANIA through Shelia za TANZANIA?
 
Hongera TEC
Je waliotaka kufanya upuuzi huu bado wanasubiri nini ndani ya ofisi za umma?
Hongera TEC? Siyo hongera Bunge? Kama ni hivyo basi ni hongera kada Kitima hongera CHADEMA
 
Serikali imeyaondoa mapendekezo yaliyopelekwa Bungeni ya kufanya marekebisho ya sheria ya Sheria ya Mamlaka ya Nchi Kuhusiana na Umiliki wa Maliasili ya mwaka 2017 na Sheria ya Mapitio na Majadiliano Kuhusu Masharti Hasi Katika Maliasili ya nchi ya mwaka 2017 kuwa zisitumike katika miradi ya bandari.

Sheria hizo zilikuwa ni miongoni mwa sheria zilizojumuishwa katika Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria Mbalimbali Na. 2 wa Mwaka 2023, uliokusudia kurekebisha, pamoja na sheria nyingine, sheria hizo mbili ili zisitumike katika uendeshaji wa miradi ya uendeshaji, uendelezaji na bandari.

Taarifa ya kuondolewa kwa marekebisho hayo ilitolewa leo Jumanne, Agosti 29, 2023, na Spika wa Bunge Tulia Ackson.

“Sehemu ya nne inafutwa ambayo inahusu mabadiliko kwenye sheria yetu ile ya marekebisho ya Sheria ya Mamlaka ya Nchi Kuhusiana na Umiliki wa Maliasili ya mwaka 2017, mapendekezo yaliyokuwa yameletwa yanafutwa yote,” alitamka Dk Ackson.

“Sehemu ya tano inahusu marekebisho ya Sheria ya Mapitio na Majadiliano Kuhusu Masharti Hasi Katika Maliasili ya nchi ya mwaka 2017 nayo inafutwa kwa maana ya kwamba Bunge halijaafiki,” aliongeza kiongozi huyo.

Hatua hii ya Bunge inakuja siku tano tangu The Chanzo iongee na Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Katiba na Masuala ya Kisheria, Joseph Mhagama, ambaye alieleza kuwa Kamati yake ilisitisha kupokea maoni juu ya mabadiliko haya yaliyopendekezwa na Serikali kwa sababu ilihitaji maelezo zaidi juu ya maudhui ya mapendekezo hayo.
🤣🤣🤣🤣🤣👆👆👆 Hii Nchi hii!!
 
Mama samia msikivu, mpole, muungwana, mwadilifu, mkweli, mnyenyekevu na zaidi ya yote mpambanaji,
Hongera sana mama
Mungu akupe nguvu utuvushe hapa penye chuki fitina za kutoka hukoooo mbali na hata karibu yetu kwa majirani
Ameeeen
 
Back
Top Bottom