Serikali yafuta mapendekezo ya kuzifanyia Marekebisho ya Sheria zinazohusu Umiliki wa Maliasili

Serikali yafuta mapendekezo ya kuzifanyia Marekebisho ya Sheria zinazohusu Umiliki wa Maliasili

Mu mpe hongera na Mwabukusi, jamaa kapambana kabla ata ya TEC, ila watu wamempuuzia, mi binafsi nampongeza sana
Hakuna aliyempuuza Mwambukusi kaamusha wengi wakiwemo TEC, kama ni mnara basi ujengwe wa Mwambukusi.
 
Nchi imejaa wajinga kila kona. Bandari huwezi kuiweka kwenye kundi la maliasili, yale maji ndio yanaingia kwenye kundi hilo.

Meli ya mzigo inayoleta magari kutoka Japan utaiweka vipi kwenye kundi la rasilimali za Taifa?.

Meli ya mzigo inayoleta mafriji na vifaa vya majumbani utaiweka vipi katika kundi la raslimali za Taifa?.

Zile mashine za kushusha na kupakia makontena utaziweka vipi kwenye kundi la rasilimali?. Zote hizi ni juhudi za wanaharakati kutaka kusema kuwa bandari yetu ni sehemu ya rasilimali, hizi ni akili za kipuuzi kabisa.
Tofautisha mali asili na rasilimali
 
Muone mjinga huyu.

TEC wanahusikaje hapo? Hata mimi niliwasilisha maoni yangu bungeni kuwa hakuna haja ya kufanya haya mabadiliko kwa kuwa masuala ya uwekezaji kwenye Bandari hayahusiani na Sheria hizi.
Wewe ni Nani hadi wakusikilize chawa mmoja wewe. Hapo ni TEC, Viongozi wako wakubwa na watu nyeti serikalini tangu Uhuru wamekuwa wakilelewa na kuchukuliwa kutoka katika kanisa katoliki
 
Bandali ni Nini Kama sio raslimali ya Taifa.

Mlima Kilimanjaro ni rasilimali ya Taifa, Mikumi, Serengeti, Tarangire hizo zote ndio rasilimali za Taifa. Twiga, Tembo, Simba hao wanyama ndio rasilimali za Taifa.

Meli ya MSC inayokuja na makontena elfu mbili na kuyashusha pale bandarini huwezi kuiita rasilimali.

Mashine za kushusha na kupakia makontena melini huwezi kuziita rasilimali. Pia kumbuka bandarini inaweza kubomolewa pale TPA ikaenda kujengwa nyingine Kilwa au Mafia.

Bandari ni miundo mbinu ya kibiashara, chanzo cha mapato cha Taifa sawa sawa na viwanja vya ndege.
 
Mnashindwa kuwachukulia hatua mafisadi mnawakumbatia halafu mnakuja kupiga kelele kinafiki.
Ndio wanapunguzwa kwa kuanzia na hao wa bandarini, ni mwendo wa kisayansi zaidi. Si unazisikia kelele za Tibaijuka?, zinawakilisha kilio cha wapigaji wengi nchini wakiwemo baadhi ya maaskofu wa TEC.
 
Sasa hayo maji ndo yanasababisha hyo bandari iwepo hapo
Bado sio kigezo cha kuipa bandari sifa ya kuitwa maliasili. Tunapiga siasa zetu za kijamaa wakati Kule DRC na Rwanda mwekezaji keshamalizana na serikali.

Ninaielewa sana awamu ya sita kuamua kuendelea na huu uwekezaji, kwani ni kwa lengo la kuinua uchumi mzima wa Tanzania, ni kwa lengo la kuwatendea haki wafanya biashara wakubwa wanaokwazwa na huu ujuaji wetu pamoja na mijadala mingi isiyokwisha.
 
Bado sio kigezo cha kuipa bandari sifa ya kuitwa maliasili. Tunapiga siasa zetu za kijamaa wakati Kule DRC na Rwanda mwekezaji keshamalizana na serikali.

Ninaielewa sana awamu ya sita kuamua kuendelea na huu uwekezaji, kwani ni kwa lengo la kuinua uchumi mzima wa Tanzania, ni kwa lengo la kuwatendea haki wafanya biashara wakubwa wanakwazwa na huu ujuaji wetu pamoja na mijadala mingi isiyokwisha.
Ni miongoni mwa rasilimali za taifa...inachangia pato kwny taifa....unavyofanya kuwekeza kwa mikataba ya muda mrefu si afya kwa uchumi wa taifa husika
 
Bado sio kigezo cha kuipa bandari sifa ya kuitwa maliasili. Tunapiga siasa zetu za kijamaa wakati Kule DRC na Rwanda mwekezaji keshamalizana na serikali.

Ninaielewa sana awamu ya sita kuamua kuendelea na huu uwekezaji, kwani ni kwa lengo la kuinua uchumi mzima wa Tanzania, ni kwa lengo la kuwatendea haki wafanya biashara wakubwa wanaokwazwa na huu ujuaji wetu pamoja na mijadala mingi isiyokwisha.
mkataba Yao kidogo imekaa kwa mfumo wa kuzisaidia Nchi husika....hapa kwetu Hawa wanasheria uchwara wamesaini tu hata yasiyohitajika
 
Ni miongoni mwa rasilimali za taifa...inachangia pato kwny taifa....unavyofanya kuwekeza kwa mikataba ya muda mrefu si afya kwa uchumi wa taifa husika
TICTS alikuwa pale kwa miaka 22 hatujui DP World atakuwa pale kwa muda gani, pia ukumbuke kuna mwekezaji mwingine atapewa magati namba tisa mpaka kumi na mbili na mwingine atapewa bandari nzima ya Bagamoyo.

Wataalam wa uchumi wamemshauri Rais baada ya kufanya utafiti wa kina sio kwamba ni maamuzi ya kukurupuka.

Lazima vichwani mwetu tuondokane na zile maana za bandari za kizamani, maana mpya ya bandari ni kutoka mzigo unapopakiwa mpaka unapomfikia mteja, wanaita end to end logistic. DPW anao uzoefu mkubwa sana kwenye hizi biashara za bandari kisasa.

Huwezi kuiweka bandari kwenye kundi la rasilimali za Taifa, kama unaongelea bandari kwa maana za kisasa, huu sio ulimwengu wa kijamaa kama ule wa enzi za awamu ya kwanza ya Mwalimu Nyerere.
 
Naona wame amka. Sio kila kitu ndiyoooo. Hata la bandari tuna taka lifutwe. Hatuwezi kuuza kila kitu kwa wageni ati kisa walioko bandarini ni wezi!!! Hivi hatuna soni?? Nani kaweka wezi bandarini kama sio Ccm na serikali yake??
Mara mufumo haisomani
 
Unatengeneza tatizo.. Unasikilizia .. Kelele zikizidi unalitatua kisha unasifiwa na kupongezwa..[emoji23] [emoji1544][emoji1550]
Acha tu mkuu. Yaani hawa jamaa wanatuona mabwege, mandorobo, mazombi, bendera fuata upepo nk nk
Ila NAHISI WADANGANYIKA KIDOGO KIDOGO WANAJITAMBUWA...
 
Hii ni Baada ya wachumia Tumbo kupigwa kikumbo na TEC yanii hamna namnaa
 
Hili ni Changa la macho tu. Kitu wanachakifanya ni kufanya marekebisho kwenye sheria zingine mbalimbali na kupachika hayo waliyoyataka kuyaweka au kuyaondoa humo kwenye sheria ya Maliasili na kuyaweka huko kwingine....mfano

Someni hiyo ya PPP ndio yenye maudhui mazuri.

Hatahivyo, kwa kusononeka kabisa, nasema, kuyaondoa mapendekezo hayo, hakuondoi uvunjwaji wa sheria au utumiaji wa Nguvu na mabavu kuhakikisha Waarabu wanakuja kututawala.

Pingeni Dhulumat hii
Nakazia.
Changa la macho walilopigwa Watanzania kuhusu kusitishwa na zoezi la kufanyia marekebisho ya sheria kwenye sheria ya maliasili ni hatari kuliko Mkataba baina ya Serikali na DPW wenyewe. Uwii.

Eh Lengai, sadia Baba. Sadia Tanzania.
 
Mindyou tupo pamoja. Nimekusoma kwenye ule uzi wako na sasa natafuta majibu kwenye marekebisho ya sheria mbalimbali zinazohusiana na Foreign Trade Policies. Nina wasiwasi humo ndimo kuna upenyo(cracks) zinazofanya yanayotokea, yatokee. Uwe na amani tu. Tanzania ni yetu sote.

Mkuu umeibua mjadala unaohitaji utulivu wa mukichwa, facts [evidence].

Wewe umetoa zako, zitetee na usitetereke.

Wacha ni peruzi.
 
Back
Top Bottom