Serikali yaunda timu ya wataalamu kupitia upya sakata la Tozo. Yasema zitarekebishwa ila hazitaondoka

Mwigulu Nchemba hadhi yake alipaswa awe mchunga Ng'ombe na sio uwaziri
 
Kuna kanuni nyepesi za uchumi ambazo wizara ya fedha ingepaswa izifahamu kama ina wachumi angalau wenye digrii moja, hizo ni pamoja;
Kujiepusha na double taxation, huwezi kutoza tozo mshahara wa mtu alioamua kuuhifadhi benki kwa sababu tayari unakuwa umelipiwa kodi.
Kodi/tozo zinapaswa kutozwa kutoka kwenye kipato kilichotoka katika biashara au ajira, huo ndio msingi wa kodi/tozo. Huwezi kuwatoza watu kwa sababu tu wamechagua benki kama njia yao ya kuhifadhi pesa zao.
Hahiitaji kamati kuelewa haya.
Unataka waamuaje?
 
Tatizo walitumia muda mwingi sana kushambulia Kaburi badala ya kujipanga….
 
Anzisha tatizo halafu litatue usifiwe
 
Nahisi suala la Vodacom kutangaza kupata hasara kubwa ndilo limewaamsha na sio huruma kwa wananchi
Kwakweli ni mwezi wa tatu sijatumia MPesa na sio kawaida yangu, halafu nimeacha na ule ujinga wakutuma ela kwa Sim Banking naenda kwenye ATM popote ilipo ntafika tu 🤣🤣🤣
 
Si ilisemwa wananchi ndiyo walishauri uwepo wa tozo! Mbano hawarudi kwa wananchi. Au hiyo timu ndiyoinwakilisha wananchi?
 
Mna uhakika huyu jamaa ni waziri kweli au?
 
Wakati mnapeleka muswada bungeni kwani mliunda kamati ya kufanya upembuzi yakinifu kuhusu tozo? Sasa mnaunda kamati ya kazi gani wakati tayari mnazo evidence za kutosha kabisa kwamba wananchi hawataki tozo maana ni mzigo kwao!

Kuna evidence gani zaidi ya hii?👇


Mategemeo yalikuwa kupata trilioni 1.25 lakini iliyopatikana ni bilioni 360 tuu. Hakuna evidence nzuri kama hii, hiyo kamati italeta majibu ya kisiasa tuu kama yale ya Twaweza..

HATUTAKI TOZO.
 
Kwenye Wodi ya Vichaa,, tahira alipewa ukiranja,,,Mwendawazimu aliporudi akakuta mwezi mchanga amesha danja...

Mazuzu hawana la kufanya wamebaki wanamshangaa tu Chizi aliyewaambia wahame nyumbani eti kisa redio inazingua...

Blame Society.
 
Ajabu sana watu wanajadili jambo ambalo limekataliwa tayari.
 
Si wameshaona mitanzania Ni midebweda ya kuchezea. Twist them the way you want
 
Tusitegemee lolote jipya toka kwa Too Madelu, yeye kila siku analia jinsi utoto wake kijijini ulivyokuwa wa shida akisahau anavyo ogelea kwenye utajiri siku hizi
 
posho ya lamati nayo inatoka kwenye tozo!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…