SGR Mchakato wa Nauli ndiyo huu hapa, mtoto hadi Moro kulipa Tshs 12,400

Sasa Kuna mtu akasema wamepewa wenye njaa kuendesha mashirika makubwa. Ina Mana wenye magari ama mabasi labda Ni wao wenyewe wameshafanya yao kila kitu kinaamuliwa na wao
 
Mtanzania yeye hataki kuwahi (muda sio pesa kwake) yeye anataka kufika tu anapokwenda. Kwa asilimia kubwa ukimuona mtanzania anataka kuwahi mahali ni ama ana dharura au tangu anaianza safari alikuwa ashachelewa.
 
Umasikini ni matokeo ya jamii kuzidiwa na negative energy.
Umasikini ni matokeo ya fikra na sio mazingira.
Mazingira hayamfanyi mtu kuwa masikini bali fikra.
Mkuu kwa kauli hii naomba tubadilishane mawasiliano Mana Naona we vibrate at the same frequency of energy.
Beliefs and thoughts trigger vibration of our body to certain frequency then we manifest what we believe.
To find the secret of Universe think in terms of energy, vibration and frequency
 
Uhalisia hauko hivyo through my experience ya nilivyoona uzunguni.
Mkuu hapa siyo uzunguni? . Tuna namna yetu flan ya kuishi. Hatujafikia level za uzungu kabisa. Wangeangalia watumiaji wengi wapo katika kundi gani na wapange hizo nauli.

Labda kwa vile siyo nauli final , ngoja tusubiri final.
 
Mzungu akisafiri ujue anawahi dill fulani au ni adventure,mswahili anaweza kusafiri kumsalimia shangazi mzaa bibi mzaa binamu ,hapo lazima atafute unafuu wa bei
 
Sasa Kuna mtu akasema wamepewa wenye njaa kuendesha mashirika makubwa. Ina Mana wenye magari ama mabasi labda Ni wao wenyewe wameshafanya yao kila kitu kinaamuliwa na wao
Hapana tusifatute mchawil kwenye hili, wenye ma bus ni watu binafsi wanafanya biashara na hawa SGR ni lazima wafanye kazi kama biashara yaani shirikia liendeshwe kiushindani kwa maana waweke mifumo bora ili umvute mteja awe na sababu ya kuja kwako kwa kusafiri au kusafirisha mizigo, kusiwe na mlolongo wa mambo na pia bei ziwe za kiushindani. Tuache kufanya kazi kimazoea wafanyakazi wote waajiriwe na shirika kwa mikataba huko watu watabanwa na perfomance, sio watu wanaiba mpaka vyuma bado wako wanalipwa mishahara na kodi za watu.
 
Nchi hii imejaza matakataka huko juu! Badala ya train iwe na nauli nafuu ndiyo inakuwa ghari kuliko mabasi? Yaani nilipe nauli kubwa hivyo na kufika nawahiwa na mwenye Bus? Watapanda wachache! Naul ya Morogoro daraja la 3 inatakiwa isizidi elfu 10?
 
Kimsingi huu mradi ulikuwa ni wa magufuli na amefariki hivyo hakuna ambaye ataweza kufanya kama yeye alivyopanga iwe.

Ninachokiona kwasasa ni watu kuhangaika na vitu ambavyo havipo katika uwezo wao kifedha na kiutendaji.

Mara walete engine na mabehewa ya kizamani ambayo hayana vigezo vya kuwekwa kwenye SGR.

Mara washindwe kadiria gharama za uendeshaji wa reli etc.
 
Tazara wana/walikuwa na options za express na ordinary! Wakajifunze huko.
Wewe itakuwa unasoma Tazara Kwa vyombo vya habari tu.

Tazara imeshakufa hamna kitu, kuna treni la Makaburu linapita mule la mizigo wamekodi miundombinu, Tazara treni ya abiria sasa hivi ni kichefuchefu kitupu, ratiba zake hovyo na linaweza kukwama popote na kucancel safari ni Jambo la kawaida.

Kama Una safari yako nakushauri upande bus tu achana na Tazara.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…