Katibu wa Halmashauri kuu ya Taifa, Itikadi na Uenezi Ndugu. SHAKA HAMDU SHAKA leo Oktoba 31 atazungumza na waandishi wa vyombo vya Habari kuanzia saa 6 mchana ofisi Ndogo za CCM - LUMUMBA Dar es salaam.
=====
CCM yapiga ‘stop’ agizo la kuzuia bodaboda, bajaji kuingia mjini
CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) kimeagiza marufuku ya waendesha bodaboda na bajaji kutofika au kufanya shughuli zao katikati jiji la Dar isitishwe mara moja kwa kuwa si muafaka lakini pia imetolewa kwa kukurupuka.
Kauli hiyo ya CCM imekuja siku moja baada ya Kamishana Msaidizi wa Polisi, Mkuu wa Usalama Barabarani Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Abdi Issango kunukuliwa akipiga marufuku bodaboda na bajaji wote kuingia mjini na wale walioko mjini watoke isipokuwa bajaji za walemavu. Marufuku hiyo ilikuwa ianze kutekelezwa rasmi tarehe 1 Novemba mwaka huu.
Aidha, akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo tarehe 31 Oktoba, 2021, Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM, Itikadi na Uenezi, Shaka Hamdu Shaka amesema marufuku hiyo ilitolewa bila kuzingatia taratibu za msingi zinazopaswa kufanya uamuzi unaogusa masilahi ya wananchi.
Amesema jambo hilo limeleta taharuki na CCM imepokea kwa mshangao mkubwa kwani ni jambo ambalo halikuwa na matayarisho mithili ya watu kukurupuka katika kutoa maamuzi hayo.
“CCM kimepokea na kufuatilia malalamiko ya wananchi mbalimbali ikiwamo, machinga, waendesha bodaboda, sanjari na malalamiko hayo, CCM kinaungana na Rais Samia katika dhamira yake ya kuona nchi yetu inapangwa vizuri na kuwa kivutio kwa kuwapanga vema machinga na wafanyabiashara wengine.
“Tuliona sasa Rais amewajali na kuwathamini kwa kutoa maelekezo kwamba watoa huduma hizo wapangwe katika maeneo rafiki,” amesema.
Amesema Chama kimeagiza Mamlaka za kiserikali mkoa wa Dar es Salaam zinazohusisha viongozi na watendaji, vyombo vya dola na mamlaka zingine zenye majukumu ya kusimamia usafiri na usafirishaji maeneo mbalimbali ya jiji la Dar es Salaam chini ya mkuu wa mkoa kwa kushirikiana na wadau wengine katika sekta hiyo, zikutane kwa haraka iwezekanavyo.
“Lengo ni kuangalia iwapo kuna changamoto zozote zilizojitokeza ili zijadiliwe na kupata ufumbuzi wa muda mfupi, wa kati na mrefu ama ufumbuzi wa kudumu ili kutoathiri na kubughudhi ustawi wa shughuli za makundi ya watu wanaohusika.
“Chama kinasisitiza kwa kuzingatia umuhimu wa suala hili, kitafuatilia na kuhakikisha
utekelezaji huu unafanyika kwa mafanikio makubwa,” amesema.
Karibu kiongozi tukusikilize...naomba upangue pumba za wale mashabiki wa chadema...wanaotoa judgement kabla ya mahakama yenyewe wakati ushahidi wa bwana yule upo wazi kabisa...ni aibu jamuhuri kushindwa kesi ambayo ipo wazi namna hii.
Katibu wa Halmashauri kuu ya Taifa, Itikadi na Uenezi Ndugu. SHAKA HAMDU SHAKA leo Oktoba 31 atazungumza na waandishi wa vyombo vya Habari kuanzia saa 6 mchana ofisi Ndogo za CCM - LUMUMBA Dar es salaam.View attachment 1993070View attachment 1993073
Hivi ile "royal tour documentary" ya Rais wetu wa JMT iliishia wapi!? Pengine Shaka angezungumzia pia suala hili muhimu la kitaifa kwa upande wa chama tawala.
Hivi ile "royal tour documentary" ya Rais wetu wa JMT iliishia wapi!? Pengine Shaka angezungumzia pia suala hili muhimu la kitaifa kwa upande wa chama tawala.
Hivi ile "royal tour documentary" ya Rais wetu wa JMT iliishia wapi!? Pengine Shaka angezungumzia pia suala hili muhimu la kitaifa kwa upande wa chama tawala.
Mkuu hivi umeelewa msingi wa swali langu? Hiyo lugha uliyoitumia mtu ya kwenda chooni na kurudi kwenye "laptop" sikutegemea kabisa kutoka kwa mtu kama wewe. Lakini sishangazwi sana katika kipindi kama hiki kwa watu kujitoa ufahamu na kujipendekeza ili tu wapate teuzi.
Serikali ya kiki na matamko. Hakuna organisation, hakuna plan, hakuna mawasiliano, bali kila mtu anajaribu kufanya anachoota usiku. Hawa ndiyo wanasema tuwaache wanajenga uchumi kwanza.