Shaka apiga ‘stop’ agizo la kuzuia bodaboda, bajaji kuingia katikati ya Mji wa Dar
IMG_1900.jpg
 
NUKUU: KATIBU WA NEC ITIKADI NA UENEZI CCM TAIFA SHAKA HAMDU SHAKA AKIZUNGUMZA NA WAANDISHI WA HABARI LEO TAREHE 31/10/2021

"Chama Cha Mapinduzi ndicho kimepewa dhamana ya kuongoza Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, hivyo ndicho chenye mkataba na wananchi nini kifanyike
Eneo kubwa na la msingi tulioahidi watanzania ni namna ya kusimamia haki na usawa na fursa za maendeleo zinatolewa wakati wote na kuhakikisha upatikanaji wa Ajira kwa Vijana"

Rais Samia alitoa malekezo kwa viongozi kuwapanga upya wamachinga,Rais Samia alisisitiza upangaji huo uambatane na wafanyabishara hao kupewa maeneo rafiki ya kufanyia biahara hizo"

"Chama Cha Mapinduzi tunawapongeza wafanyabiashara wadogo almaarufu machinga kwa mapokeo yao mazuri ya maelekezo ya kuhamia kwenye maeneo rasmi waliyotengewa kufanyia kazi"

Chama cha mapinduzi inatoa kauli ifuatayo 1 marufuku ya waendesha bodaboda au bajaji sio muafaka bali ingetumia taratibu shirikishi kwa wananchi na viongozi wao hivyo CCM inasitisha mara moja jambo hilo"

"Chama Cha Mapinduzu kinaonya kuhusu utaratibu ulioanza kuibuka kwa mtu au mamlaka kuanza kutoa kauli au maagizo yasiyokihaki hali ambayo inaibua sintofahamu kwa wananchi wetu"

"Mhe Rais Samia Suluhu Hassan alitoa malekezo kwa viongozi kuwapanga upya wamachinga,Rais Samia alisistiza upangaji huo uambatane na wafanyabishara hao kupewa maeneo rafiki yakufanyia biahara zao"

"Kitendo cha kuwahamisha wafanyabiashara wadogo bila kuwawekea mazingira rafiki na mazuri. watakaofanyia biashara zao ni marufuku na haikubaliki
Chama Cha mapinduzi tunazielekeza kamati za siasa za Mikoa na Wilaya kuhakikisha kuwa maelekezo ya Mhe. Rais kwenye mikoa yao yanatekelezwa kwa malengo tarajiwa ikitokea haziendi vema kweye jambo hili na hazioneshi mafanikio kama ilivyo malengo ya Mhe.Rais Samia basi zitawajibika"

#KaziInaendele

IMG_20211031_133954_756.jpg
 
Wamachinga wanalipia dhambi yao ya usaliti,walinunuliwa na jiwe kwa vitambulisho vya 20k
 
Siku si nyingi wamachinga watarudi kwenye maeneo yao na kuendelea na biashara kama kawaida
 
Ila huyu jamaa Shaka namkubali, japo fisiemu siwaelewi lakini ana siasa isiyo ya kinafiki, tunahitaji wengine wengi kama huyu...

Safi sana
 
Comment za mwanzo kabla hii yangu mbona sizielewi..isije ikawa mmeshapangwa siku ile na shaka alivyokutana na nyie MATAGA wa mtandaoni kwamba kuna mtu ataanzisha uzi kuhusu mimi then mkasapoti kwa nguvu nimewaza tu..haiwezekani tatizo lianzishwe na haohao ccm then mnakuja kujifaragua hapa eti hongera CCM,viva mama kenge nyie
 
Ndo hii mwanaharakati mmoja amesema vyama vya wafanyakazi vimekosa sauti ya wafanyakazi mishahara na mafao yanachezewa lakini makundi ya machinga na bodaboda ndo yanaumiza vichwa vya wanasiasa.

Jeshi la polisi lenye dhamana ya kulinda raia na Mali zao wanaona hatari ya bodaboda kiusalama, mwanasiasa anapigia chepuo kura.

Jana mkuu wa mkoa kasema Kuna maongezi, huyu naye kwa nini afanye ni ajenda yake? Mnatoa picha gani kwa wananchi?
 
Naipenda CCM na Serikali lakini wakati mwengine tukubali kuna watu hawakustahili kuwepo hapo walipo!!..Hivi Mwenezi wa chama ana wezaje kutoa Kauli ya kukemea utendaji wa mkuu wa Mkoa!!..Huyu ana jua kashkash za Hawa Boda Boda hapo ferry?!...Au kule kariakoo!!..
 
Naipenda CCM na Serikali lakini wakati mwengine tukubali kuna watu hawakustahili kuwepo hapo walipo!!..Hivi Mwenezi wa chama ana wezaje kutoa Kauli ya kukemea utendaji wa mkuu wa Mkoa!!..Huyu ana jua kashkash za Hawa Boda Boda hapo ferry?!...Au kule kariakoo!!..
Kccm ccm ,mwenezi ana pawa kuliko mkuu wa mkoa.
 
Back
Top Bottom