Jabali la Siasa
JF-Expert Member
- Jul 10, 2020
- 2,823
- 2,466
CCM ndio yenye mkataba na wananchi, Serikali haiwajibiki popote,Hakika imani inarudi kwa chama
Machinga tembeeni kifua mbele mnacho chama makini cha CCM,
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
CCM ndio yenye mkataba na wananchi, Serikali haiwajibiki popote,Hakika imani inarudi kwa chama
Rais hajasema watu wanyaing'nywe bidhaa zao,Huu ni ule ule upumbavu wa kusema rais anapotoshwa na washauri wake utadhani rais ni zuzu asiye na akili. Rais ndiye anajichonganisha mwenyewe. Nchi yetu system ya uongozi imepitwa na wakati. Haiwezekani rais ndiye awe think tank wa kila kinachotokea kwenye nchi. Akiambiwa inahitajika system overhaul anajitoa akili na kusema eti apewe muda aujenge uchumi wakati kujenga uchumi bila kwanza kuweka misingi mizuri ya uongozi ni kitu kisichowezekana.
Africa ni Bara Masikini,Mtoto wa maskini?!
Huyo wa mtoto wa maskini ni yupi... mmiliki wa ajaji/bbodaboda, dereva au anayepanda bajaji/bbodaboda?
Kama anayepanda... HAPANA!
Labda kama ule uchumi wa kati waliotuambia The World Bank, ndo upo hapo Daslam!!
CCM HAWATEGEMEI SANDUKU LA KURA, TISS NA POLISI WAPO.[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
Lazima ajue 2025 tunauchaguzi,
Hahahahah......Upumbavu mwingine Wa baadhi ya wanaJF bana! Utadhani kabla Shaka hajaja na press yake hakukaa na uongozi wa mkoa wa DSM kuteta haya mambo na kupata cha kuongea leo mbele ya waandishi wa habari. Alichokiongea Shaka leo Makala anataarifa nacho na SSH anataarifa nacho. It's a collective decision.CCM imepata viongozi imara sana,
Leo nimeona nguvu ya chama dhidi ya dola,
Hongera sana Shaka, endelea kutupigania ndg zako,
Unajua hata kinachojadiliwa hapa? Nani kasema rais au chama kimesema?Rais hajasema watu wanyaing'nywe bidhaa zao,
Hajasema wapelekwe Porini,
Hajasema wanyanyaswe ,
Hivyo Chama kiko sahihi,
Naunga mkono hoja
P
CCM CHAMA,Katibu wa Halmashauri kuu ya Taifa, Itikadi na Uenezi Ndugu. SHAKA HAMDU SHAKA leo Oktoba 31 atazungumza na waandishi wa vyombo vya Habari kuanzia saa 6 mchana ofisi Ndogo za CCM - LUMUMBA Dar es salaam.
=====
CCM yapiga ‘stop’ agizo la kuzuia bodaboda, bajaji kuingia mjini
CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) kimeagiza marufuku ya waendesha bodaboda na bajaji kutofika au kufanya shughuli zao katikati jiji la Dar isitishwe mara moja kwa kuwa si muafaka lakini pia imetolewa kwa kukurupuka.
Kauli hiyo ya CCM imekuja siku moja baada ya Kamishana Msaidizi wa Polisi, Mkuu wa Usalama Barabarani Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Abdi Issango kunukuliwa akipiga marufuku bodaboda na bajaji wote kuingia mjini na wale walioko mjini watoke isipokuwa bajaji za walemavu. Marufuku hiyo ilikuwa ianze kutekelezwa rasmi tarehe 1 Novemba mwaka huu.
Aidha, akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo tarehe 31 Oktoba, 2021, Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM, Itikadi na Uenezi, Shaka Hamdu Shaka amesema marufuku hiyo ilitolewa bila kuzingatia taratibu za msingi zinazopaswa kufanya uamuzi unaogusa masilahi ya wananchi.
Amesema jambo hilo limeleta taharuki na CCM imepokea kwa mshangao mkubwa kwani ni jambo ambalo halikuwa na matayarisho mithili ya watu kukurupuka katika kutoa maamuzi hayo.
“CCM kimepokea na kufuatilia malalamiko ya wananchi mbalimbali ikiwamo, machinga, waendesha bodaboda, sanjari na malalamiko hayo, CCM kinaungana na Rais Samia katika dhamira yake ya kuona nchi yetu inapangwa vizuri na kuwa kivutio kwa kuwapanga vema machinga na wafanyabiashara wengine.
“Tuliona sasa Rais amewajali na kuwathamini kwa kutoa maelekezo kwamba watoa huduma hizo wapangwe katika maeneo rafiki,” amesema.
Amesema Chama kimeagiza Mamlaka za kiserikali mkoa wa Dar es Salaam zinazohusisha viongozi na watendaji, vyombo vya dola na mamlaka zingine zenye majukumu ya kusimamia usafiri na usafirishaji maeneo mbalimbali ya jiji la Dar es Salaam chini ya mkuu wa mkoa kwa kushirikiana na wadau wengine katika sekta hiyo, zikutane kwa haraka iwezekanavyo.
“Lengo ni kuangalia iwapo kuna changamoto zozote zilizojitokeza ili zijadiliwe na kupata ufumbuzi wa muda mfupi, wa kati na mrefu ama ufumbuzi wa kudumu ili kutoathiri na kubughudhi ustawi wa shughuli za makundi ya watu wanaohusika.
“Chama kinasisitiza kwa kuzingatia umuhimu wa suala hili, kitafuatilia na kuhakikisha
utekelezaji huu unafanyika kwa mafanikio makubwa,” amesema.
Pia soma:
Thread 'Kuanzia Novemba Mosi Bajaji na Bodaboda marufuku kuingia Mjini' Kuanzia Novemba Mosi Bajaji na Bodaboda marufuku kuingia Mjini
Ccm inahujumiwaKatibu wa Halmashauri kuu ya Taifa, Itikadi na Uenezi Ndugu. SHAKA HAMDU SHAKA leo Oktoba 31 atazungumza na waandishi wa vyombo vya Habari kuanzia saa 6 mchana ofisi Ndogo za CCM - LUMUMBA Dar es salaam.

Pole kaka nimeiudhi nafsi yako.Wewe ni mtu mpumbavu sana. Ungemjibu vizuri ungekufa?