Hili ni bandiko la maswali kwa Tundu Lissu na dereva wake, kufuatia shambulio la Lissu,
Shambulizi la Lissu, Wanaomdhania Dereva Anahusika, Sio Wajinga!, Wana Hoja za Msingi!. Jee Anahusika?.
Maswali haya ni kufuatia hoja za Lissu kwenye bandiko hili.
Mhe. Tundu Lissu,
Kwanza pole sana kwa yaliyokusibu.
Umezungumza mengi kuhusu kilichotokea mwaka mmoja uliopita, ila watu wanaohoji kuhusu dereva wako, nakuomba sana usiwaite wajinga, au wametumwa, kwa sababu mashaka yao ni very valid.
Kwa vile mashuhuda ni nyinyi wawili tuu, wewe na dereva wako, then kuna mambo tungependa kujua kutoka kwa Lissu mwemyewe na dereva wake.
Hoja kuwa tumetoka naye mbali hivyo tunaaminiana, hazina mashiko mbele ya watu na kazi zao. Lissu alipotoka na dereva wake, anaweza kujilinganisha Dr. Slaa na mlinzi wake Kagenzi walipotoka, halafu what happened?!.
Baadhi ya maswali ni haya...
- Baada kuona kuna gari linawafuatilia, mlichukua hatua gani?.
- The common sense ya kufuatiliwa inaelekeza, uki note you're followed, hatua ya kwanza ni kumpote anaye kufollow kwa makusudi, ili kwanza kujiridhisha kuwa anakufollow.
- Ukiisha jiridhisha you are followed, una change direction kumpoteza maboya.
- Ukimuona bado yupo, then kama uko fit, unamlengesha mahali kwenye kona ambapo hawezi kuchomoka, mnamalizana!.
- Kama hauko fit, unamlengesha kwenye safe area ,usually sehemu open kwenye makundi ya watu na kumripoti kunakohusika.
- Baada ya kuona mnafuatwa, kwa nini mliendelea kuelekea nyumbani?.
- Mlipofika mkasimama, mkawaona watu wawili wanashuka na AK 47, kitendo tuu cha kujua tuu bunduki zile ni AK 47, hii maana yake ni close proximity, kwenye shooting that close!, risasi 38!, dereva huyu amesalimikaje asipitiwe hata na moja?.
- Ametokaje kwenye gari na kujificha chini ya gari ya jirani bila kugundulika?!.
- Anafichwa nini kuhojiwa?, kuna nini kinafichwa?.
- Maswali yataendelea
Hitimisho.
The only defence ya Dereva wa Lissu has nothing to do na hiyo shooting, ni uzito tuu wa serikali kugoma kuita wachunguzi wa nje. Ingekuwa ni inside job ya Chadema, tungeshuhudia serikali fasta ingechunguza!.
Lakini kwa vile wasiojulikana ni hawa
Tusitegemee lolote jipya hapa.
Tundu Lissu, just get well soon, na sasa inakubidi uchangue kati ya uanaharakati na kuishi.
Pole.
.