Shambulizi la Lissu: Wanaomdhania dereva anahusika sio wajinga, Wana hoja za msingi. Je, anahusika?

Shambulizi la Lissu: Wanaomdhania dereva anahusika sio wajinga, Wana hoja za msingi. Je, anahusika?

Hili ni bandiko la maswali kwa Tundu Lissu na dereva wake, kufuatia shambulio la Lissu,
Shambulizi la Lissu, Wanaomdhania Dereva Anahusika, Sio Wajinga!, Wana Hoja za Msingi!. Jee Anahusika?.
Maswali haya ni kufuatia hoja za Lissu kwenye bandiko hili.
Mhe. Tundu Lissu,
Kwanza pole sana kwa yaliyokusibu.
Umezungumza mengi kuhusu kilichotokea mwaka mmoja uliopita, ila watu wanaohoji kuhusu dereva wako, nakuomba sana usiwaite wajinga, au wametumwa, kwa sababu mashaka yao ni very valid.

Kwa vile mashuhuda ni nyinyi wawili tuu, wewe na dereva wako, then kuna mambo tungependa kujua kutoka kwa Lissu mwemyewe na dereva wake.

Hoja kuwa tumetoka naye mbali hivyo tunaaminiana, hazina mashiko mbele ya watu na kazi zao. Lissu alipotoka na dereva wake, anaweza kujilinganisha Dr. Slaa na mlinzi wake Kagenzi walipotoka, halafu what happened?!.
Baadhi ya maswali ni haya...
  1. Baada kuona kuna gari linawafuatilia, mlichukua hatua gani?.
  2. The common sense ya kufuatiliwa inaelekeza, uki note you're followed, hatua ya kwanza ni kumpote anaye kufollow kwa makusudi, ili kwanza kujiridhisha kuwa anakufollow.
  3. Ukiisha jiridhisha you are followed, una change direction kumpoteza maboya.
  4. Ukimuona bado yupo, then kama uko fit, unamlengesha mahali kwenye kona ambapo hawezi kuchomoka, mnamalizana!.
  5. Kama hauko fit, unamlengesha kwenye safe area ,usually sehemu open kwenye makundi ya watu na kumripoti kunakohusika.
  6. Baada ya kuona mnafuatwa, kwa nini mliendelea kuelekea nyumbani?.
  7. Mlipofika mkasimama, mkawaona watu wawili wanashuka na AK 47, kitendo tuu cha kujua tuu bunduki zile ni AK 47, hii maana yake ni close proximity, kwenye shooting that close!, risasi 38!, dereva huyu amesalimikaje asipitiwe hata na moja?.
  8. Ametokaje kwenye gari na kujificha chini ya gari ya jirani bila kugundulika?!.
  9. Anafichwa nini kuhojiwa?, kuna nini kinafichwa?.
  10. Maswali yataendelea
Hitimisho.
The only defence ya Dereva wa Lissu has nothing to do na hiyo shooting, ni uzito tuu wa serikali kugoma kuita wachunguzi wa nje. Ingekuwa ni inside job ya Chadema, tungeshuhudia serikali fasta ingechunguza!.

Lakini kwa vile wasiojulikana ni hawa

Tusitegemee lolote jipya hapa.
Tundu Lissu, just get well soon, na sasa inakubidi uchangue kati ya uanaharakati na kuishi.

Pole.
P.
Mkuu sikujua kama unaupumbavu kiasi hiki shame on you
Vyeo visikufanye ukapoteza cv yako uliojijengea hope utaona wangapi wanaokusapoti kwa huu upuuzi uliaondika hapo
 
Hoja ya serekali kumtaka dereva ni ya kujihami kwa ajilli ya kupotosha ukweli waonekane kuwa hawahusiki na tukio.
 
bavicha wajinga sana nyie, kwahiyo mnampangia MTU cha kuandika? nyie hamtakagi kusemwa madudu Na madhaifu yenu Ila serikali kuu ndio ipondwe. MTU akiiponda serikali ndio mbamuona ana akili.
poleni sana Sahauini kushika dola kwenye taifa hilii
Duuh sitaki kuamini MTU kama wewe unaongea haya daah kweli kwa hayo mkuu unayosema unamuenzi lucky dube?
Nimepitia Uzi wako juu ya lucky dube ukajinasibu kuwa ni mfuasi wake kindakindaki sasa iweje Leo ufarahie ubaya wa ccm kwa wananchi na wapinzani???
 
Hata Mungu alijua kuwa Yesu atasulubiwa ili aliacha yatimie ili sisi tukombolewa.

Kupitia shambulio la Lissu,hata sisi tutakombolewa(sometimes Mungu huruhusu mambo fulani yatokee kwa malengo maaalumu).

Kumbuka wangekuwa na nia wasingeshindwa kwenda kuwahoji hospitalI ya Nairobi.

Jiulize tu angekuwa ni kigogo wa serikali alieshambuliwa kama huyo dereva wasingemfuata kumuhoji hata kama angekuwa ni Ulaya.
Mission ilifeli serikali ikaumbuka na itaendelea kuumbuka. Aibu tupu.
 
With all my respect kwako Mr.Mayala huu ni uzi ambao labda ninafikiria umeandikiwa au umeuandika bila ya to apply your mind,mie ni neutral kwa siasa zinazofanyika hapa nyumbani Tanzania,na maelezo yako yote hapo juu ni matokeo ya kuishi ndani ya nchi ya kusadikika soma na elewa yafuatayo:the golden rule unapoona unafuatiliwa na gari nyuma ni kuendesha gari lako uelekeo wa kituo cha polisi(hii italeta woga kwa wanaokufuatilia)sio takataka za maelezo yako hapo juu,pili ile ilikuwa ni security complex yenye walinzi getini na cctv(ni wajibu wa walinzi kuandika kwenye logo book yao magari yote yanayotoka na kuingia) hii inathibiti kuingia na kutoka kwa vyombo vya moto na wenzetu sasa wanakifaa kama meter ya kusomea maji ambacho wanakitumia to clic driving licence na disc ya gari kwa hiyo taarifa za dereva na owner wa gari zinatunzwa ndani ya mashine hii,;uzembe wa jeshi letu la polisi inapelekea kesi hii kuwa the cold one kwa sababu walishindwa hata ku secure the crime scene,hakuna wataalamu wa foresic waliokwenda eneo la tukio;hii ni siasa na upepo wa kisiasa utakapokuja kubadilika nchini ukweli utajulikana.
 
Enyi kizazi kisichoelewa? tutakaa nanyi mpaka lini? je... ni kufungwa au kurogwa kwa akili zenu? ikiwa Pascal Mayalla amelieleza hili kwa lugha nyepesi na hamkuweza kulielewa.je si vyema aliyosema nabii wetu kuwa yeye ni kichaa na anateua watu vichaa? je sisi tutakuwa salama katika hili? ni vyema alivyotabiri nabii .......akisema "watu hawa hu graduate kwa vyeti ila akili zao zipo mbali na elimu, nao hupoteza muda bure kujifunza elimu iliyo utashi wa mwanadamu"

pascal ni kazi sana kuwwandikia watanzania wakaelewa. uelewa wao ni mdogo sana. na huo mdogo umekuwa clouded na mahaba. they dont think wanaendeshwa na mahaba.
 
Paskali Pascal Mayalla,
Ninavyofahamu vyombo vya usalama na intelejensia vya Belgium vilivyo makini wangeweza kweli kumpa viza dereva kuingia Belgium na kumruhusu kukaa na Tundu Lissu nchini Ubelgiji? Bado sijagusia vyombo vya usalama Kenya nao vikose umakini kumruhusu dereva kuwa pamoja na Tundu Lissu!

Hoja zingine ni nyepesi sana tumsikilize Mh. Tundu Lissu akielezea serikali kushindwa kufanya uchunguzi makini ktk video clip hii kuanzia dakika ya 2 .

Tundu Lissu yupo na dereva wake kuanzia Dodoma akawa naye Nairobi wakati wa matibabu, pia sasa dereva huyo huyo yupo na Mh. Tundu Lissu nchini Ubelgiji. Hii ina maana vyombo vya usalama na intelejensia Kenya na Ubelgiji baada ya kupitia, kuchambua, kuhoji mazingira ya tukio la shambulizi, wamejiridhisha dereva siyo mtuhumiwa.

Hivi kweli Paskali unaweza 'kumtuhumu' huyu dereva Kwa hoja nyepesi hivyo!

Source: BBC swahili
c.c. Pascal Mayalla
 
Ndugu Pascal, nakupongeza kwa ujasiri wako, umeuliza maswali stahiki sana, na yanahitaji majibu na sio kejeli au matusi.

Wasio kuwa NA akili ama wale BLIND SUPPOTERS , hawana uwezo wa kuukubali ukweli wala kujibu hoja kwa hoja.

Utatukanwa sana kwa hili bandiko, lakini kaa ukijua umemuuliza Lissu maswali yanayo stahili majibu ya ukweli. Nami namshauri asitumie tukio lililompata kuendelezea umaarufu wake wa kisiasa, bali ajitahidi kuitumia kupata haki zake, NA mojawapo ni utata wa Dereva wa gari lake?
 
UFIPA kama wamepoteana kwenye hii thread..

Freedom of Speech inaendana sambamba na demokrasia,

Pascall katumia demokrasia kutoa maoni yake kama mtanzania..
 
Mayalla usianzie kwenye kufatwa na gari .. hata unaposema walipoona AK47 na jinsi gani walijinasua na dereva kupona hupaswi kuhoji haya wkt mlengwa alichapwa risasi 16 kati ya 38.
... UNAPASWA kuhoji "kwanini wauaji wakafanye tukio baya kama lile ndani ya majengo ya serikali na kuna ulinzi mkali na CCTV zipo.
Walinzi walikuwa wapi km wanalinda 24 hours?

Hapa mbona ni akili ndogo tu itahoji hv.. Sio wewe unaesema dereva angepeleka gari sijui eneo gani, sjui kwenye kona gani?..
Hv mayalla uko unaposema palikuwa salama kuzidi alikoshambuliwa?.. Mbona Aquilina alichapwa mbele ya umati unashuhudia , Je nani kashikwa, je kuna kesi ya muuaji au season tu.
Ukiwa mwandishi kama wewe na ukabanwa na serikali usiseme ukweli, basi achana naya siasa andika ya MAPENZI au SPORT bado utabaki kuwa mwandishi.
Kuliko kuficha akili kwenye soksi kiasi hiki kaka.
 
Pascal Mayalla hapa huwezi jibiwa swali hata moja kati ya ulilouliza, nilichokiona hapa hawa wafuasi wa hicho chama wanapingana na wanachokipigania. Sasa tuwaelewe vipi?

Si wanataka uhuru wa kujieleza na kuhoji mambo, sasa mbona wao hawatoi huo uhuru wa kuhojiwa na wao. Wakiulizwa swali defense yao ni kushutumu mtu mara kachukue buku saba Lumumba, utasikia pia unataka uupate uteuzi.
MTU ANASHINDWA KUKIFANYA HICHO ANACHOKIPIGANIA ILI AWE MFANO BORA.... SI UNAFIKI HUU.

Hayo maswali uliyouliza, wengi wamehoji yanayofanana ila wanaambulia kashfa tu.
 
Angekuwa hausiki angekwenda kuhojiwa, madawa aliyopewa Lissu kusinzia ili afanyiwe hayo, risasi zinapiga kushoto anaumia kulia, kiti cha lissu kinalazwa alale dereva hapati hata jeraha,

Camera zinatolewa kwa uchunguzi watu wanadhani ni serikali imezitoa kuficha ukweli,

Suala la Lissu Mbowe anahusika sana sema hamuelewi n.a. Lissu ni mjanja mno anawasiliana na Magufuli ili akipona ndo amwage cheche, mpaka sasa Mbowe hajatulia anatapa tapa kupoteza ushahid wote , lakin Sami ya Mtu ni nzito sana haimwagiki tu,

Leo hii waliopaswa kulipwa ujira wa kazi hiyo wananyongwa tu kupoteza ushahidi, kuna mengi watu wanajua ila wanaogopaga tu kutoa ushahidi,

Britannica
Tumbo niache nimuachie Manenge.
Inahitajika mtu awe zaidi ya Zezeta ndo anaweza kulielewa bandiko lako mkuu.

Naona jua limeshaanza kuwa kali.
 
Namba Tisa imefanya nikudharau,
Labda umepoteza umakini sababu umeandika meeeengi,nadhani ukirudia utagundua kitu,
Lkn una hakika hawakuyafanya unayosema?,
Kuhusu dereva km unadhani anahusika alishindwaje kummalizia lisu baada ya kuona hajafa na badala yake akawa wa kwanza kutoa taarifa kwa MBOWE,siyo polic
Mkuu hoja hizo ngumu sana kujibika kwa hawa ccm na ukatili wao
 
Hili ni bandiko la maswali kwa Tundu Lissu na dereva wake, kufuatia shambulio la Lissu,
Shambulizi la Lissu, Wanaomdhania Dereva Anahusika, Sio Wajinga!, Wana Hoja za Msingi!. Jee Anahusika?.
Maswali haya ni kufuatia hoja za Lissu kwenye bandiko hili.
Mhe. Tundu Lissu,
Kwanza pole sana kwa yaliyokusibu.
Umezungumza mengi kuhusu kilichotokea mwaka mmoja uliopita, ila watu wanaohoji kuhusu dereva wako, nakuomba sana usiwaite wajinga, au wametumwa, kwa sababu mashaka yao ni very valid.

Kwa vile mashuhuda ni nyinyi wawili tuu, wewe na dereva wako, then kuna mambo tungependa kujua kutoka kwa Lissu mwemyewe na dereva wake.

Hoja kuwa tumetoka naye mbali hivyo tunaaminiana, hazina mashiko mbele ya watu na kazi zao. Lissu alipotoka na dereva wake, anaweza kujilinganisha Dr. Slaa na mlinzi wake Kagenzi walipotoka, halafu what happened?!.
Baadhi ya maswali ni haya...
  1. Baada kuona kuna gari linawafuatilia, mlichukua hatua gani?.
  2. The common sense ya kufuatiliwa inaelekeza, uki note you're followed, hatua ya kwanza ni kumpote anaye kufollow kwa makusudi, ili kwanza kujiridhisha kuwa anakufollow.
  3. Ukiisha jiridhisha you are followed, una change direction kumpoteza maboya.
  4. Ukimuona bado yupo, then kama uko fit, unamlengesha mahali kwenye kona ambapo hawezi kuchomoka, mnamalizana!.
  5. Kama hauko fit, unamlengesha kwenye safe area ,usually sehemu open kwenye makundi ya watu na kumripoti kunakohusika.
  6. Baada ya kuona mnafuatwa, kwa nini mliendelea kuelekea nyumbani?.
  7. Mlipofika mkasimama, mkawaona watu wawili wanashuka na AK 47, kitendo tuu cha kujua tuu bunduki zile ni AK 47, hii maana yake ni close proximity, kwenye shooting that close!, risasi 38!, dereva huyu amesalimikaje asipitiwe hata na moja?.
  8. Ametokaje kwenye gari na kujificha chini ya gari ya jirani bila kugundulika?!.
  9. Anafichwa nini kuhojiwa?, kuna nini kinafichwa?.
  10. Maswali yataendelea
Hitimisho.
The only defence ya Dereva wa Lissu has nothing to do na hiyo shooting, ni uzito tuu wa serikali kugoma kuita wachunguzi wa nje. Ingekuwa ni inside job ya Chadema, tungeshuhudia serikali fasta ingechunguza!.

Lakini kwa vile wasiojulikana ni hawa

Tusitegemee lolote jipya hapa.
Tundu Lissu, just get well soon, na sasa inakubidi uchangue kati ya uanaharakati na kuishi.

Pole.
P.
Mbona jiwe linafuhia tukio hilo?
 
Back
Top Bottom