Shambulizi la Lissu: Wanaomdhania dereva anahusika sio wajinga, Wana hoja za msingi. Je, anahusika?

Shambulizi la Lissu: Wanaomdhania dereva anahusika sio wajinga, Wana hoja za msingi. Je, anahusika?

Pascal Mayalla umelishemsha dude mchana wa leo na hii single ya singeli yako mpya, yaani hapa umeongea point tu na it's true kwa uyasemayo ila nasikitika tu kwa baadhi ya wabongo kuyapinga kwa kuwa walishajiaminisha ujinga bila kufikiri nje ya box. Yes, unaweza kuwa umetoka mbali na mtu ila katika hela Usishangae ukaja salitiwa kwani hata Yesu ilimtokea sembuse Lissu, who is he? Watanzania wengi (binadamu) si wa kuwaamini 100%, you'll be a fool to do so. Well said Pascal. Wewe ni kichwa. Subiri kuitwa tena Dodoma kwenye kamati ya ulinzi ukaulizwe ulifikiriaje. Keep it up.
 
Mm nakubali kuwa Dereva wa Lisu alihusika lakini swali langu ni kwa nini CCTV camera zote za Nyumba xajirani pale zilizimwa je zilizimwa na nani nakwa nini
Kama zilikua oni kwa nini police wasichukue mkanda wa video yake kutumia kama ushahidi
Jiulize hapo walio mtuma Dereva ni waupande gani
 
Dereva hakuumia kwanini walimkimbiza Nairobi, Serekali haiendi nchi nyingine kiholela, Dreva kapelkwa Ubelgiji , yote hiyo mko sawa tuu? Mtasema anamsaidia lissu, hiyo ni kazi ya Hospitali, Nairobi Hospital is one of the best in EAst Africa, ninaojua vizuri sana, kuna wagonjwa kweye coma NA wanahudumiwa NA Nurses .

Wana Chadema hampendi kuulizwa maswali , mnapenda watu wale YES man kwenu ama kwa jambo lenu lolote.

Pascal ameuliza very valid questions NA yanahitaji majibu yeye busara, NA LISSU AKISHINDWA KUYAJIBU HAYA VIZURI NA BILA JAZBA ZAKE, BASI ATAKUWA GUILTYBIN CONSIPARANCY NA WALE WALIOMTEDEA MABAYA, kwani anazui ukweli usitoke NA kuitumia hali yake kisiasa.

Which is very cheap and crocked politics
Huna hoja ya msingi hoja zako mfu kabisa!!! Hivi kama dereva kahusika ilikuaje msaidie baada tu ya wasiojulikana kuondoka? Kama kahusika si angemmalizia tu pale pale??
Je zile CCTV camera kwann kalemani aling'oa??
 
Hili ni bandiko la maswali kwa Tundu Lissu na dereva wake, kufuatia shambulio la Lissu,
Shambulizi la Lissu, Wanaomdhania Dereva Anahusika, Sio Wajinga!, Wana Hoja za Msingi!. Jee Anahusika?.
Maswali haya ni kufuatia hoja za Lissu kwenye bandiko hili.
Mhe. Tundu Lissu,
Kwanza pole sana kwa yaliyokusibu.
Umezungumza mengi kuhusu kilichotokea mwaka mmoja uliopita, ila watu wanaohoji kuhusu dereva wako, nakuomba sana usiwaite wajinga, au wametumwa, kwa sababu mashaka yao ni very valid.

Kwa vile mashuhuda ni nyinyi wawili tuu, wewe na dereva wako, then kuna mambo tungependa kujua kutoka kwa Lissu mwemyewe na dereva wake.

Hoja kuwa tumetoka naye mbali hivyo tunaaminiana, hazina mashiko mbele ya watu na kazi zao. Lissu alipotoka na dereva wake, anaweza kujilinganisha Dr. Slaa na mlinzi wake Kagenzi walipotoka, halafu what happened?!.
Baadhi ya maswali ni haya...
  1. Baada kuona kuna gari linawafuatilia, mlichukua hatua gani?.
  2. The common sense ya kufuatiliwa inaelekeza, uki note you're followed, hatua ya kwanza ni kumpote anaye kufollow kwa makusudi, ili kwanza kujiridhisha kuwa anakufollow.
  3. Ukiisha jiridhisha you are followed, una change direction kumpoteza maboya.
  4. Ukimuona bado yupo, then kama uko fit, unamlengesha mahali kwenye kona ambapo hawezi kuchomoka, mnamalizana!.
  5. Kama hauko fit, unamlengesha kwenye safe area ,usually sehemu open kwenye makundi ya watu na kumripoti kunakohusika.
  6. Baada ya kuona mnafuatwa, kwa nini mliendelea kuelekea nyumbani?.
  7. Mlipofika mkasimama, mkawaona watu wawili wanashuka na AK 47, kitendo tuu cha kujua tuu bunduki zile ni AK 47, hii maana yake ni close proximity, kwenye shooting that close!, risasi 38!, dereva huyu amesalimikaje asipitiwe hata na moja?.
  8. Ametokaje kwenye gari na kujificha chini ya gari ya jirani bila kugundulika?!.
  9. Anafichwa nini kuhojiwa?, kuna nini kinafichwa?.
  10. Maswali yataendelea
Hitimisho.
The only defence ya Dereva wa Lissu has nothing to do na hiyo shooting, ni uzito tuu wa serikali kugoma kuita wachunguzi wa nje. Ingekuwa ni inside job ya Chadema, tungeshuhudia serikali fasta ingechunguza!.

Lakini kwa vile wasiojulikana ni hawa

Tusitegemee lolote jipya hapa.
Tundu Lissu, just get well soon, na sasa inakubidi uchangue kati ya uanaharakati na kuishi.

Pole.

P.

Au mimi ndiyo sijui kusoma? mbona jamaa kalenga hapo kwenye red na maswali hayo ni kile wazungu wanasema pomposity a.k.a mbwembwe. Mimi naona message iko clear sana kwenye hiyo red au mnataka wenzenu waandike tu mnadhani hivi vita ni vya kiroho? oooh wakuu hivi vita ni vya mwili na damu na watu wana watoto
 
Paskali Pascal Mayalla,
Ninavyofahamu vyombo vya usalama na intelejensia vya Belgium vilivyo makini wangeweza kumpa viza dereva kuingia Belgium na kumruhusu kukaa na Tundu Lissu nchini Ubelgiji? Bado sijagusia vyombo vya usalama Kenya nao vikose umakini kumruhusu dereva kuwa pamoja na Tundu Lissu!
Hoja zingine ni nyepesi sana tumsikilize Mh. Tundu Lissu akielezea serikali kushindwa kufanya uchunguzi makini ktk video clip hii kuanzia dakika ya 2 . Tundu Lissu yupo name dereva wake kuanzia Dodoma akawa naye Nairobi wakati wa matibabu na sasa dereva huyo yupo na Mh. Tundu Lissu nchini Ubelgiji.

Hivi kweli Paskali unaweza 'kumtuhumu' huyu dereva Kwa hoja nyepesi hivyo!

Source: BBC swahili


There is fire behind the smoke, kama wanemuani NA hahusiki kwanini wanamkimbiza hivyo, mara Nairobi NA leo Belgium. Hivi wewe huoni hapo pana kitu kinafichwa.
 
Enyi kizazi kisichoelewa? tutakaa nanyi mpaka lini? je... ni kufungwa au kurogwa kwa akili zenu? ikiwa Pascal Mayalla amelieleza hili kwa lugha nyepesi na hamkuweza kulielewa.je si vyema aliyosema nabii wetu kuwa yeye ni kichaa na anateua watu vichaa? je sisi tutakuwa salama katika hili? ni vyema alivyotabiri nabii .......akisema "watu hawa hu graduate kwa vyeti ila akili zao zipo mbali na elimu, nao hupoteza muda bure kujifunza elimu iliyo utashi wa mwanadamu"

pascal ni kazi sana kuwwandikia watanzania wakaelewa. uelewa wao ni mdogo sana. na huo mdogo umekuwa clouded na mahaba. they dont think wanaendeshwa na mahaba.
Huenda hata wew uelewa wako mdogo zaid ndomana unafikiri kila MTU yupo km wew
 
Paskali Pascal Mayalla,
Ninavyofahamu vyombo vya usalama na intelejensia vya Belgium vilivyo makini wangeweza kweli kabisa kumpa viza dereva 'mtuhumiwa' kuingia Belgium na kumruhusu kukaa na Tundu Lissu nchini Ubelgiji? Bado sijagusia vyombo vya usalama Kenya nao vikose umakini kumruhusu dereva kuwa pamoja na Tundu Lissu!

Hoja zingine ni nyepesi sana tumsikilize Mh. Tundu Lissu akielezea serikali kushindwa kufanya uchunguzi makini ktk video clip hii kuanzia dakika ya 2 .

Tundu Lissu yupo na dereva wake kuanzia Dodoma akawa naye Nairobi wakati wa matibabu na sasa dereva huyo huyo yupo na Mh. Tundu Lissu nchini Ubelgiji. Hii maana yake ni kuwa vyombo vya usalama na intelejensia nchini Kenya na Ubelgiji baada ya kupitia, kuchambua, kuhoji mazingira ya shambulizi, wamejiridhisha dereva siyo mtuhumiwa.

Hivi kweli Paskali unaweza 'kumtuhumu' huyu dereva Kwa hoja nyepesi hivyo!

Source: BBC swahili
c.c. Pascal Mayalla
 
Ndugu Pascal, nakupongeza kwa ujasiri wako, umeuliza maswali stahiki sana, na yanahitaji majibu na sio kejeli au matusi.

Wasio kuwa NA akili ama wale BLIND SUPPOTERS , hawana uwezo wa kuukubali ukweli wala kujibu hoja kwa hoja.

Utatukanwa sana kwa hili bandiko, lakini kaa ukijua umemuuliza Lissu maswali yanayo stahili majibu ya ukweli. Nami namshauri asitumie tukio lililompata kuendelezea umaarufu wake wa kisiasa, bali ajitahidi kuitumia kupata haki zake, NA mojawapo ni utata wa Dereva wa gari lake?
Huko Lumumba wanawatia sumu mbaya sana kiasi kwamba uwezo wenu wakufikiri unakuwa zero kabisaaa!!!! Dereva km kahusika je alishindwa kipi kummalizia tu pale pale? Hujui nini unaongea na huyo pasko!!!
 
Mayala bhana., watu wakivaa tshet zenye picha ya lisu wanakamatwa... Hebu habar ya risas tuiache jaman, . Watu tushachoka na stor tunataka maendeleo
 
Angekuwa hausiki angekwenda kuhojiwa, madawa aliyopewa Lissu kusinzia ili afanyiwe hayo, risasi zinapiga kushoto anaumia kulia, kiti cha lissu kinalazwa alale dereva hapati hata jeraha,

Camera zinatolewa kwa uchunguzi watu wanadhani ni serikali imezitoa kuficha ukweli,

Suala la Lissu Mbowe anahusika sana sema hamuelewi n.a. Lissu ni mjanja mno anawasiliana na Magufuli ili akipona ndo amwage cheche, mpaka sasa Mbowe hajatulia anatapa tapa kupoteza ushahid wote , lakin Sami ya Mtu ni nzito sana haimwagiki tu,

Leo hii waliopaswa kulipwa ujira wa kazi hiyo wananyongwa tu kupoteza ushahidi, kuna mengi watu wanajua ila wanaogopaga tu kutoa ushahidi,

Britannica
Aisee jamii forum imeanza kuumwa ugonjwa wa magufuli na mpina.
 
Mayalla usianzie kwenye kufatwa na gari .. hata unaposema walipoona AK47 na jinsi gani walijinasua na dereva kupona hupaswi kuhoji haya wkt mlengwa alichapwa risasi 16 kati ya 38.
... UNAPASWA kuhoji "kwanini wauaji wakafanye tukio baya kama lile ndani ya majengo ya serikali na kuna ulinzi mkali na CCTV zipo.
Walinzi walikuwa wapi km wanalinda 24 hours?

Hapa mbona ni akili ndogo tu itahoji hv.. Sio wewe unaesema dereva angepeleka gari sijui eneo gani, sjui kwenye kona gani?..
Hv mayalla uko unaposema palikuwa salama kuzidi alikoshambuliwa?.. Mbona Aquilina alichapwa mbele ya umati unashuhudia , Je nani kashikwa, je kuna kesi ya muuaji au season tu.
Ukiwa mwandishi kama wewe na ukabanwa na serikali usiseme ukweli, basi achana naya siasa andika ya MAPENZI au SPORT bado utabaki kuwa mwandishi.
Kuliko kuficha akili kwenye soksi kiasi hiki kaka.
Mkuu hao wanatumiwa vibaya!! Huyo pasko toka aitwe bungeni akakutana na timu Fulani ikiongozwa na mkuchika na hayo ndo matokeo yake
 
Kabla ya kutoa hio dhana yako ningekuomba ujibu Masuala 3 tu:-
1. Kwa nini siku ya tukio hapakua na Mlinzi Bungeni
2. Jee kwanini Picha za Camera ulinzi hazijuilikani zilipo?
3. Kwa nini Serikali ikatae uchunguzi huru ukishirikisha vyombo vya Kimataifa?
Hata haya uliyouliza yapate majibu vipi lkn bado maswali ya Pascal ni valid.Inawezekana vipi bunduki ya kivita imuache salama dereva huku ikimjeruhi lisu tena risasi 38?
 
Back
Top Bottom