JF itaanza kusakamwa sana ili iwe offline, wakishindwa kabisa kabisa, wanaweza kuleta figisufigisu ipumzike kwa muda.
Yote kwa yote, nchi haiko salama hata kidogo.
Walikua wanasingizia uhaini na uhalifu, sasa nauona kabisa mambo yatakavyobadilika na kwenda tofauti na mipango.
Balozi mkuu ana watu, ndani na nje ya mfumo.
Jeshi napo sio wote wanaokubaliana na yanayoendelea.
Bado kuna kundi halikufurahishwa na kifo cha balozi mdogo.
Haya yote ni kama bomu linalosubiri kulipuka muda wowote.
Mtawala ni kama amemeza ndoana, haimezeki wala kutemeka.