TANZIA Sheikh Rashid Njuki afariki dunia. Inadaiwa alisomewa Albadil

TANZIA Sheikh Rashid Njuki afariki dunia. Inadaiwa alisomewa Albadil

Sheikh maarufu Rashid Njuki amefariki dunia usiku wa kuamkia leo baada ya kupata ajali ya gari. Tukio hili limetikisa jamii ya Kiislamu nchini na kuibua maswali mazito baada ya kusambaa kwa sauti na ushuhuda kwamba Sheikh huyo alifanyiwa Albadil (Dua ya mabaya) na baadhi ya wenzake waliokuwa wakipingana naye.

Hapa nitaweka video 👇👇
View attachment 3460715

Katika sauti hiyo, Sheikh Njuki mwenyewe alieleza wazi wazi kuwa alifanyiwa Dua maalum iliyolenga apate ajali ili taasisi yake ya Manasik ife. Na kwenye hiyo video Kuna mmoja alifanikiwa kuingia Dua iliposomwa na akarekodi.

Hali hii imechochea hisia kali mitandaoni na mijadala mikubwa kuhusu nafasi ya maombi ya mabaya ndani ya dini hii, nimewahi kuleta sana masomo na makala kuhusu hii dini inayotumia Majini kuua ,n k

Sheikh Njuki amezikwa leo jioni katika Mkoa wa Manyara mara baada ya Swala ya Magharibi, kwa wingi wa waumini, ndugu na marafiki waliomiminika kumuaga safari yake ya mwisho.

Mazishi yake yameacha simanzi kubwa, huku wengi wakitafakari kauli yake ya mwisho kuhusu Dua aliyosomewa, ambayo leo imetimia kwa njia ile ile aliyotabiriwa ( ajali ya gari.)


TAASISI YA MANASIK

Taasisi ya Manasik, iliyoanzishwa na Sheikh Njuki, ilikuwa na jukumu kubwa la kufundisha Waislamu taratibu za Hija na Umra kwa vitendo.

Ilitoa elimu kwa waumini wanaojiandaa kuelekea Makka, ikiwafundisha namna ya kutekeleza ibada mbalimbali kama tawaf, sa’i, wukufu Arafah na kurusha mawe (jamaraat),

Ilikuwa ikitambuliwa kama kituo maalum cha semina, mihadhara na mafunzo ya Hija kwa njia rahisi na za kisasa.

Kwa muda mfupi tu, taasisi hii ilianza kupata umaarufu mkubwa, ikivutia waumini kutoka maeneo mbalimbali nchini., huyu jamaa akaanza kupata pesa ,kwahiyo chanzo ni CHUKI


KWANINI ILIPIGWA VITA?

1. Wivu na Ushawishi Umaarufu wa Sheikh Njuki na taasisi yake ulionekana tishio kwa madrasa na taasisi nyingine zilizokuwa zikijihusisha na elimu ya Hija na Umra.,(kumbuka hijja na Umra ni biashara za watu ,nishaeleza sana Kuna Uzi nilileta Mods wakauondoa ,nilionesha jinsi watu wanavyopiga pesa kwa hii biashara ,jinsi Waarabu wanavyoingiza mabilion na mabilion kupitia mfuko wa PIF)


2. Tofauti za Kiiitikadi – Wapo masheikh na walimu waliokuwa na mitazamo tofauti ya kifiqhi. Tofauti hizo zilipelekea kumtazama kama mpinzani na sio mshirika.,


3. Hofu ya Kupoteza Wafuasi – Kadri waumini walivyoelekea kwenye Manasik, baadhi ya viongozi wengine waliamini kuwa ushawishi wao na nafasi zao kijamii vitadhoofika.,Kumbuka hii ni biashara kama biashara nyingine ,hivo wanaibiana wateja(maamuma)


4. Fitna na Mashindano – Badala ya mshikamano, chuki binafsi na mashindano ya kijamii yakawa chanzo cha maombi ya mabaya. Hatimaye Sheikh Njuki akajikuta akifanyiwa Albadil Dua ya kumuombea apate ajali ili kuua taasisi yake.


Pumzika kwa Amani Sheikh Njuki
Siyo mbaya kama kitabu wanachosoma na kukiamini kinaruhusu kurogana basi amekufa shahidi.
 
Kuna Shehe alikuja saiti tunafanya kazi ya kumwaga zege akasema kama mngekuwa waislam na mna Imani na Allah, manaswali swala 5 basi hii zege yote hapa mngeweza kumuomba Mwenyezi Mungu awape malaika waibebe hii zege ndani ya dakika chache 🤣🤣
Nilibaki nacheka tu moyoni nasema yaani wewe ungejua
Imani ni kazi kubwa sana, na aina hii ya imani utaisikia afrika tu
 
Hilo neno Yehova ni lugha yavkiebrania kwa masna ya Mungu,tumis akili.Waebrania wanamuita Mungu Yehova,hiuo Ye kwa masharika ya kati,ni sawa na kusema the kwa English,waarabu wao wanatumia Ya,
Mkuu, ukisoma Kutoka 6:2 mbona inajieleza vyema.
 
Binafsi nafahamu Nguvu ya Albadiri, nimekulia Uswahili, Kuna miaka ya Nyuma sehemu nilipokulia kulikua na Tajiri mmoja alikua akimiriki Canter kadhaa za Mchanga, miongoni wa Madereva wa Gari yake mmoja kulikua na Mzee mmoja akitoka mtaani kwangu kabisa.

Yule Mzee alikua akipaki gari maeneo Fulani ya mtaani, ghafla siku Moja akakuta Ile Canter ipo juu ya Matofari, na hakuna Matairi, yote 6 yameibiwa.

Baada ya muda yule Mzee alichapisha Matangazo akaweka Kila sehemu, akitoa siku 7 mtu aliyeiba arudishe, pia alipita yeye mwenye Vijiweni akitoa taarifa Kwa mdomo, Binafsi nilikua Bado Kijana Mdogo, so niliona harakati zake Kwa macho, nikisoma Matangazo yake mtaani.... Mwishoni mwa Tangazo lake akasema ikipita siku 7 kitachotokea tusilaumiane.ita

Mtaani kukawa na fununu kwamba Kijana wa Mzee mmojawapo wa Mtaani Kwa kushirikiana na wenzake ndiyo waliiba Yale Matairi, na sote tunamjua huyo Kijana na baadhi ya Marafiki zake wakiwa ni Wakubwa mbali kwangu Enzi hizo.

Baada ya siku 7 kupita hajui ni wapi yule Mzee alienda ila aliporudi mtaani kukaanza kutokea Misiba ya Vijana, mmoja mpaka mwingine, na Mtu wa mwisho ambaye alikua ndo in charge wa Wizi huo ambao Watu wote tunamfahamu, akawa Mwendawazimu mpaka muda huu, na Bado yupo mtaani, na ratiba ya mizunguko yake mpaka Sasa ni Barabarani, barabara kubwa ya mtaani.

Swali Kwa Masheikh, Mimi nilikua najua Albadir huwapata ama kumpata Mtu aliyefanya Ubaya ni kama njia ya kulipa kisasi... Je! Albadir inaweza kumpata hata mtu ambaye hajafanya Ubaya kwa Mtu ila imesomwa tu Kwa Chuki...?

hayo ni mambo ya kichawi sio katika Dini Hakuna pahala katika uislam panaelekeza kusoma dua za namna hiyo Hakuna ni ushirikina na wanaviumbe wao ambao wanawategemea kufanya izo ibada zao ni washirikina na end of the day adhabu yao ni chungu mno😭
 
Eti kuna mtu alikuwa anauliza juzi kuwa NOVENA ni kama albadil nikamjibu hapa BIG NO sisi hatuna maombi ya kuombea mabaya bali NOVENA ni maombi kwa Mungu pale akili yetu ya kibinadamu inapokuwa imefika mwisho huoni pa kutokea ndio unaomba NOVENA kuomba Mungu akusaidie

Na mara zote tinayaqcha MAPENZI YA MUNGU yatimie

Sasa hizi habari za kuombeana mabaya na kutumiana majini🤣🤣🤣🤣hii dini sijawahi kuielewa
 
Alisema mwenyewe na aliipost video akiombewa ALBADIL afe kwa ajali
Mkuu mbona nimekukubalia kama unavotaka kafa kwa ALBADIL.
Au unataka unithibitishie kisayansi na kiroho namna ALBADIL inavoua?
Haya nifafanulie namna ALBADIL ilivochomoa tairi la gari na kusababisha ajali maana unataka nikuelewa zaidi.
 
MAJINI ni waislamu Mzee,

Sura Al-Jinn 72:1-2
“Majini waliosikia Qur’an wakasema, ‘Tumesikia Qur’an ya ajabu; inatuongoza kwenye haki. Kwa kweli tumeamini; basi hatutamsaidia yeyote isipokuwa Allah.’”

Hii inathibitisha majini walisilimu na kukubali Qur’an.
Yesu alitaka kuwangiza majini kwrnye ukristo mzee wakasema afadhali waimgie kwa ngyruwe,kuliko.kuwa wakristo,wakaimgia kwa nguruwe.Kasome Biblia uone
 
Eti kuna mtu alikuwa anauliza juzi kuwa NOVENA ni kama albadil nikamjibu hapa BIG NO sisi hatuna maombi ya kuombea mabaya bali NOVENA ni maombi kwa Mungu pale akili yetu ya kibinadamu inapokuwa imefika mwisho huoni pa kutokea ndio unaomba NOVENA kuomba Mungu akusaidie

Na mara zote tinayaqcha MAPENZI YA MUNGU yatimie

Sasa hizi habari za kuombeana mabaya na kutumiana majini🤣🤣🤣🤣hii dini sijawahi kuielewa
Hiyo neno Novena kwa kiebrania maana yake uchawi wa majini
 
Kilicho niumiza sana ni kitendo cha huyo Shehe mlozi kuwashirikisha watoto wadogo kati mambo ya urozi:
Hao watoto watakuwa na maadili gani ?
Alishundwaje kusoma hiyo Albadiri peke yake au na warazi wenzake ?
Hii imenima sana
 
Eti kuna mtu alikuwa anauliza juzi kuwa NOVENA ni kama albadil nikamjibu hapa BIG NO sisi hatuna maombi ya kuombea mabaya bali NOVENA ni maombi kwa Mungu pale akili yetu ya kibinadamu inapokuwa imefika mwisho huoni pa kutokea ndio unaomba NOVENA kuomba Mungu akusaidie

Na mara zote tinayaqcha MAPENZI YA MUNGU yatimie

Sasa hizi habari za kuombeana mabaya na kutumiana majini🤣🤣🤣🤣hii dini sijawahi kuielewa
Kwa muktadha wa uchaguzi ndugu watanzania labda tuanze vurugu mtindo mmoja , kuiyos ccm kws maombi ni kazi ngumu wakuu
 
Mkuu mbona nimekukubalia kama unavotaka kafa kwa ALBADIL.
Au unataka unithibitishie kisayansi na kiroho namna ALBADIL inavoua?
Haya nifafanulie namna ALBADIL ilivochomoa tairi la gari na kusababisha ajali maana unataka nikuelewa zaidi.
Hapo atakukimbia tu
 
Sheikh maarufu Rashid Njuki amefariki dunia usiku wa kuamkia leo baada ya kupata ajali ya gari. Tukio hili limetikisa jamii ya Kiislamu nchini na kuibua maswali mazito baada ya kusambaa kwa sauti na ushuhuda kwamba Sheikh huyo alifanyiwa Albadil (Dua ya mabaya) na baadhi ya wenzake waliokuwa wakipingana naye.

Hapa nitaweka video 👇👇
View attachment 3460715

Katika sauti hiyo, Sheikh Njuki mwenyewe alieleza wazi wazi kuwa alifanyiwa Dua maalum iliyolenga apate ajali ili taasisi yake ya Manasik ife. Na kwenye hiyo video Kuna mmoja alifanikiwa kuingia Dua iliposomwa na akarekodi.

Hali hii imechochea hisia kali mitandaoni na mijadala mikubwa kuhusu nafasi ya maombi ya mabaya ndani ya dini hii, nimewahi kuleta sana masomo na makala kuhusu hii dini inayotumia Majini kuua ,n k

Sheikh Njuki amezikwa leo jioni katika Mkoa wa Manyara mara baada ya Swala ya Magharibi, kwa wingi wa waumini, ndugu na marafiki waliomiminika kumuaga safari yake ya mwisho.

Mazishi yake yameacha simanzi kubwa, huku wengi wakitafakari kauli yake ya mwisho kuhusu Dua aliyosomewa, ambayo leo imetimia kwa njia ile ile aliyotabiriwa ( ajali ya gari.)


TAASISI YA MANASIK

Taasisi ya Manasik, iliyoanzishwa na Sheikh Njuki, ilikuwa na jukumu kubwa la kufundisha Waislamu taratibu za Hija na Umra kwa vitendo.

Ilitoa elimu kwa waumini wanaojiandaa kuelekea Makka, ikiwafundisha namna ya kutekeleza ibada mbalimbali kama tawaf, sa’i, wukufu Arafah na kurusha mawe (jamaraat),

Ilikuwa ikitambuliwa kama kituo maalum cha semina, mihadhara na mafunzo ya Hija kwa njia rahisi na za kisasa.

Kwa muda mfupi tu, taasisi hii ilianza kupata umaarufu mkubwa, ikivutia waumini kutoka maeneo mbalimbali nchini., huyu jamaa akaanza kupata pesa ,kwahiyo chanzo ni CHUKI


KWANINI ILIPIGWA VITA?

1. Wivu na Ushawishi Umaarufu wa Sheikh Njuki na taasisi yake ulionekana tishio kwa madrasa na taasisi nyingine zilizokuwa zikijihusisha na elimu ya Hija na Umra.,(kumbuka hijja na Umra ni biashara za watu ,nishaeleza sana Kuna Uzi nilileta Mods wakauondoa ,nilionesha jinsi watu wanavyopiga pesa kwa hii biashara ,jinsi Waarabu wanavyoingiza mabilion na mabilion kupitia mfuko wa PIF)


2. Tofauti za Kiiitikadi – Wapo masheikh na walimu waliokuwa na mitazamo tofauti ya kifiqhi. Tofauti hizo zilipelekea kumtazama kama mpinzani na sio mshirika.,


3. Hofu ya Kupoteza Wafuasi – Kadri waumini walivyoelekea kwenye Manasik, baadhi ya viongozi wengine waliamini kuwa ushawishi wao na nafasi zao kijamii vitadhoofika.,Kumbuka hii ni biashara kama biashara nyingine ,hivo wanaibiana wateja(maamuma)


4. Fitna na Mashindano – Badala ya mshikamano, chuki binafsi na mashindano ya kijamii yakawa chanzo cha maombi ya mabaya. Hatimaye Sheikh Njuki akajikuta akifanyiwa Albadil Dua ya kumuombea apate ajali ili kuua taasisi yake.


Pumzika kwa Amani Sheikh Njuki
Fitna na Mashindano – Badala ya mshikamano, chuki binafsi na mashindano ya kijamii yakawa chanzo cha maombi ya mabaya. Hatimaye Sheikh Njuki akajikuta akifanyiwa Albadil Dua ya kumuombea apate ajali ili kuua taasisi yake.🥺🥺🥺🥺
 
Sio vema Mashehe kuwashirikisha watoto katika mambo ya chuki, visasi na kuumizana:
 
Isaya 53
5 Bali alijeruhiwa kwa makosa yetu, Alichubuliwa kwa maovu yetu; Adhabu ya amani yetu ilikuwa juu yake, Na kwa kupigwa kwake sisi tumepona.

6 Sisi sote kama kondoo tumepotea; Kila mmoja wetu amegeukia njia yake mwenyewe; Na Bwana ameweka juu yake Maovu yetu sisi sote.


Kifupi cha Maelezo ya Fasihi kuhusu Isaya 53:


Wakristo hudai kuwa Isaya 53 ilitabiri kifo na kufufuka kwa Yesu, lakini historia ya kifungu hicho inaonyesha kuwa "mtumishi" anayetajwa ni taifa la Israeli, si mtu binafsi. Manabii kama Yeremia, Ezekieli, Hosea na Nahumu wanaelezea mateso ya Israeli kama taifa lililonyanyaswa, kupelekwa utumwani Babeli, kisha kurejeshwa na Mungu kwa heshima na ukombozi.


Katika Isaya 53, mataifa ya watu wa nje (Wapagani) ndio wanaozungumza, wakistaajabu kwa yale waliyoona yakimtokea “mtumishi wa Bwana.” Maelezo hayo yanafanana na mateso ya Israeli: kudharauliwa, kuumizwa, na kuonekana kana kwamba wamelaaniwa. Biblia yenyewe mara kadhaa inamwita Israeli “mtumishi,” “kondoo wa kuchinjwa,” na “chipukizi la shina kavu.”


Isaya 53 haimhusu Yesu kwa sababu:


  • Yesu hakusifiwa wala kupokelewa na watu wake.
  • Hakuwa na kizazi (hana "zera" – uzao wa damu).
  • Hakuishi muda mrefu ("hakuongeza siku zake").
  • Alizungumza alipokuwa akiteswa, kinyume na unyenyekevu wa “mtumishi” wa Isaya 53.
  • Biblia inakataza sadaka ya dhambi ya mwanadamu kwa ajili ya mwingine (Ezekieli 18:20).
  • Tafsiri za Kikristo zimegeuza maana ya maandiko ya Kiebrania kuthibitisha mafundisho ya kafara.

Badala ya Yesu, "mtumishi" anayeteseka ni Israeli, aliyepitia udhalilishaji, uhamisho, na kuahidiwa ukombozi wa Mungu. Kifungu hiki kinahusu mateso ya kihistoria ya taifa, si mtu mmoja aliyejitoa kuwa sadaka.




Hitimisho la Kifasihi:


Isaya 53 ni simulizi ya maumivu na tumaini la Israeli, si unabii wa Yesu. Ukristo umechukua kifungu hicho nje ya muktadha wake halisi. Uislamu nao unasisitiza kuwa Yesu hakusulubiwa, bali alinyakuliwa na Allah.

Hivyo, madai ya kafara yanatenguka kisayansi, kihistoria na kimaandiko.
 
Back
Top Bottom