SI KWELI Shemasi ‘George Rugambwa’ awauliza maswali sita Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC)

SI KWELI Shemasi ‘George Rugambwa’ awauliza maswali sita Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC)

Baada ya kuitathmini taarifa hii, tumebaini kuwa si ya kweli.
Kuna ujumbe unasambazwa WhatsApp, una kichwa kinachosema Maswali Sita kwa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC) je, ni wa kweli?

1692377824932.jpeg
 
Tunachokijua
Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (kwa Kiingereza Tanzania Episcopal Conference, TEC) ni muundo wa Kanisa Katoliki unaokutanisha maaskofu wake wote wa nchi ya Tanzania, wakiwa wanaongoza jimbo, au ni waandamizi, wasaidizi au wamestaafu.

Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC) limetoa tamko tarehe 18, 08, 2023 juu ya mkataba (makubaliano) wa bandari ya Tanzania ambao wameweka msimamo wao wa kutouunga mkono mkataba huo.
F30BJgDWgAACEjR

Mara baada ya kutolewa kwa tamko hilo, umeonekana ujumbe ambao unasambaa kupitia mtandao wa WhatsApp, ukidaiwa kuandikwa na Shemasi George Rugambwa wa Seminari ya Ntungamo, Bukoba, Ujumbe huo una kichwa cha habari, Maswali Sita kwa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC)

1692369684035-png.2720856

Ni upi ukweli kuhusu ujumbe huu?

JamiiForums
ilifanya mawasiliano na Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC) ili kupata kujua ukweli wa ujumbe huo, ambao wamekanusha kuwepo kwa Shemasi mwenye jina la George Rugambwa katika hiyo Seminari wala kuwepo kwa Shemasi yoyote Seminari ya Ntungamo.

"Hakuna Shemasi katika hiyo Seminari anayejulikana kwa jina hilo na wala hakuna Shemasi kabisa katika hiyo seminari" Walisema TEC

Kufuatia TEC kukanusha kuwepo kwa Shemasi yeyote katika Seminari ya Ntungamo, JamiiForums Imejiridhisha kuwa ujumbe wenye kichwa Maswali Sita kwa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC) unaodaiwa kuandikwa na Shemasi George Rugambwa wa Seminari ya Ntungamo kuwa ni wa kuzushwa na hauna ukweli wowote.
Dubai sio nchi mkataba ni batili Dubai haina bendera un sawa sawa na zanzibar therefore contract us null and void
 
Back
Top Bottom