Sheria 13 za mpira wakati tukiwa watoto

Sheria 13 za mpira wakati tukiwa watoto

mpira ukipita katikati ya miguu ya golikipa na kuingia golini, yanahesabiwa magoli mawili.
 
mi nakumbuka zile dakika za lala salama,ilikuwa ukisikia zilinde basi ujue muda wa viatu umefika.
 
Hapo ana maana kua mpira unaweza kua umetengenezwa na mtu mmoja au mara nyingine hutokea watu wengi wanashiriki kutengeneza mpira
 
mwenye mpira akikasirika anachukua mpira anaweka kwapani anaondoka
alaf ilikua mtu aliyezidi umri sana haruhusiw kucheza
 
dah, nimekumbuka mbali sana, uwanja wa mbuzi vibandani morogoro, baada ya mechi ni ngumi na watoto wa vibandani
 
kasheshe ni tunapocheza na watoto wa Manzese morogoro balaa, wanacheza na viwembe mfukoni, mkiwafunga tu kimenuka
 
kuna siku tulienda kucheza tabata walitusakizia mbwa baada ya kuwafunga 13-6

ha ha ha 13 kwa sita... kuna siku nilimuuliza mtoto wa sista leo mmtoka ngapi ngapi akaniambia tumewafunga 32 kwa 20
duh nilikumbuka mbali sana... enzi hizo timu inaweza shinda kwa goli 98..
 
Kona
Si lazima Kutumia mguu unapopiga kona, Ukiona mazingira hayakuruhusu, rusha kwa mikono (unaweza kutumia Mkono mmoja kama mpira ni mdogo)

2.Mwenye Mpira
Mwenye mpira ndiye ana maamuzi ya nani acheze na
nani asicheze, ni marufuku kumtoa Mwenye mpira hata akicheza vibaya. Anaruhusiwa kukutoa endapo hutampa pasi (hatakama ulifunga)

3.Upangaji wa Kikosi
Mwenye mwili mkubwa huyo ni beki mnene lazima awe golikipa,Ila mwenye mpira anaruhusiwa kupanga upya, na yeye lazima awe mshambuliaji

4.Penati

Itatokea tu pale mchezaji akiumia sana, akalia na kutoka damu. (mara nyingi hatoendelea na mpira)
5.Kuotea (offside)
Hakuna Kuotea, Free kick itapigwa pale tu mtu akishika mpira.
6. Refa
Ni Yule mchezaji mbabe, au mwenye mpira, ila mchezaji anaweza kuzunguka
na mpira hata nyuma ya goli.

Kubadili Mchezaji
7. Inaruhusiwa kubadili Mchezaji endapo ataitwa kwao na akirudi, ataendelea na nafasi yake. Pia ni ruksa kubadili golikipa kamapenati ikitokea na baada ya penati golikipa anaweza kuendelea yule wa mwanzo.

8.Wachezaji wa akiba
Wale ambao wamekosa namba kazi yao ni kufata mpira ukitoka, au kutungua mpura endapo utanasa kwenye mti huku wakisubiria mchezaji aitwe kwao na wao wapate nafasi.


9.Jezi
Upande wa mwenye mpira watavaa mashati na wengine watavua. Suala la viatu, Mwenye Mpira anaamua Wote Mcheze peku au na viatu, akikasirika, mechi ndo itakua imefika mwisho

10.Mpira Kumalizika
Mechi itaisha pale tu Mwenye mpira ataitwa nyumbani,atakapochoka, au kama kila mchezaji atakua amechoka, au giza kuingia.
 
haahaha hizi sheria zimenikumbusha mbali.nilikua mwenye mpira siku zote lazima wakupape
 
Nimecheka vibaya sanaaa yaaani unanikumbusha mbali kinomi.Yaani mwenye mpira alikuwa kama Mungu halafu sasa mchezaji anayejua jua kucheza kila mtu anamtaka awe upande wake
 
nimecheka sana, mapumziko(halftime) hutokea muda wowote mzee "mnoko" akitokea au mwenye nyumba ambapo uwanja upo(ambaye mara nyingi hukataza watoto wasicheze mpira uwanjani kwakwe".
Kabisa mkuu yaan ilikuwaga noma sana,
 
Back
Top Bottom