Sheria 13 za mpira wakati tukiwa watoto

Sheria 13 za mpira wakati tukiwa watoto

Kama kwenu kuna Tv hukosi namba na hata kama ulichelewa ukifika uwanjani lazima atafutwe mnyonge atoke.
 
Nilikuwa Mtaalamu sana wa kufuma mipira ya Makaratasi hata uwe na kucha ndefu za Miguu au kupiga 'dochi' huwezi kuufumua. 1965-1975 Mission Quatre Kariakoo mkimaliza mpira mnafata Bagia Mnazi mmona
 
Nimecheka vibaya sanaaa yaaani unanikumbusha mbali kinomi.Yaani mwenye mpira alikuwa kama Mungu halafu sasa mchezaji anayejua jua kucheza kila mtu anamtaka awe upande wake
Kama kawaida hvyo ndo ilikuwa aisee wenye mipira walkuwaga nuksi sana,
 
Nilikuwa Mtaalamu sana wa kufuma mipira ya Makaratasi hata uwe na kucha ndefu za Miguu au kupiga 'dochi' huwezi kuufumua. 1965-1975 Mission Quatre Kariakoo mkimaliza mpira mnafata Bagia Mnazi mmona
Mlitisha sana aiseee,
 
Nawakumbuka Lanziko,Remsi Mkung'a,Kasim na Hemedi Mangula,Idika Mihale,Boi,Adume,Abel,dah nimekumbuka mbali sana.Nilikuwa golkipa maarufu kama nyani.
 
Duh mzee umenikumbusha mbali. Pia mwenye mpira akiona amechoka na hataki kutoka anakwenda kumtoa golikipa akacheze ndani afu yeye akae golini kudaka ndo kupumzika kwake huko. Akiona kapumzika vya kutosha basi anamrudisha jamaa kwenye nafasi yake ya ukipa halafu yeye anarudi ndani.
 
Aiseee mi nilikuwa pande za Lugalo jeshini 1992-1995 yaani mechi ikienda pigwa area E au D lazima tukawaombee ruhusa wale wachezaji ambao wadingi zao ni wanoko si mnajua tena wajeda wanatupa muda wa watoto wao kurudi home yaani ikifika sa 12 jioni wawe ndani
 
Wachezaji wenye machacha ni ngumu kupata Namba kwa hofu ya kupasua mpira ama kuharibu mpira!
 
Back
Top Bottom