goli linaweza kuwa ni mawe au ndala/kandambili. Kama tumeshinda au tupo droo na tunaelekea fungwa ilikuwa ni lazima kulitibua goli, kama ni ndala au viatu utapiga teke moja tu, mfungaji atakosa pa kufungia, kama ni jiwe litarushwa mbali na mechi itakuwa imeisha.
Mpira unaoingia golini hautakiwi vuka juu ya magoti, na ukivuka hapo tu basi hakuna goli, itahesabika umepaisha.
Shule Timu yangu tuliiita new balance sababu wengi tulivaa viatu vya mtumba vilivyoandika new balance.
Kwa home mechi iliisha punde tu sauti ya land rover 109 iliposikika, maana ilikuwa inasikika kona 3 kabla ya kufika home, ushahidi wa magoli ulitibuliwa, kama ni ndala kila mtu alivaa zake, kama ni mawe basi tulitupa mbali, watoto wa majilani walikimbilia kwao, huku tukiomngoja baba kwa nje.