Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
8:mwenye matege au anaetumia mguu wa kushoto huaminika anajua mpira kuliko wengine7. Mwenye mpira ndio anaanza kuchagua wachezaji wazuri wachezee upande wake
HahahahaAnayeruhusiwa kupiga shuti kali ni mwenye mpira tuu
6.Giza likianza kuingia faulo zinaruhusiwa4. Kama timu yetu hatuna viatu, na ninyi vueni viatu
5. Hakuna refa, uamuzi wa mchezo mf. faulo au kona ni makubaliano
Wa kwanza kufungwa ndo wanavua mashatikama hamna jezi timu moja wanavua mashati au t shirt.
Sijui watoto wetu wamepumbazwa na ma-TV? Yaani wanacheza kwa kusuasua sana, wakati enzi zile tulikuwa tunatoka mtaa kwenda kushindana na mtaa mwingine au kijiji kimoja na kingine! Mkitoka suluhu zinapigwa ngumi angalau timu moja ionekane bingwa!!Kuna moja ya Kipa na Ndani,haaahaaaa raha sana.Siku hizi watoto hawachezi kabisa
Kwa hiyo mlikuwa na jeuri ya kunyima namba wenye Tv kwao?SHERIA 15 ZA MPIRA ZA KIPINDI CHA UTOTONI
1. Mkubwa Hachezi Na Akicheza Mnaingia Wawili.
2.Mwenye Mpira Hatolewi Hata Akicheza Vibaya.
3.Inaruhusiwa Kubadili Kipa Kama Penati Imetokea Na Baada Ya Penati Anaruhusiwa Kurudi Wa Mwanzo.
4.Yule Mtaalam Wa Soka Hakosi Namba Hata Siku Moja.
5. Dogo Mnene Lazima Awe Golikipa.
6.Mwenye Mpira Ataamua Nani Asicheze.
7.Penati Itatokea Tu Pale Mchezaji Akiumia Sana Na Kutoka Damu.
8.Mechi Itaisha Kama Kila Mchezaji Atakuwa Amechoka.
9. Hakuna Free Kick,refa Wala Offside.
10. Ukichaguliwa Mwishoni Ujue Uwezo Wako Mdogo Kuliko Wote Uwanjani.
11.Mtaalam Wa Timu Akipewa Kazi Na Wazazi Wake Lazima Mumsaidie Ndo Mwende Kucheza.
12.Ukiumia Kidonda Kinawekwa Mchanga.
13.Kipa Anaruhusiwa Kudaka Popote.
14. Wale Ambao Wamekosa Namba Kazi Yao Ni Kufata Mipira Ikitoka.
15. Mwenye Mpira Akikasirika Mechi Ndo Inakuwa Imeisha
Sio tv, sema KIDEOKwa hiyo mlikuwa na jeuri ya kunyima namba wenye Tv kwao?