Sheria 13 za mpira wakati tukiwa watoto

Sheria 13 za mpira wakati tukiwa watoto

Dah! umenikumbusha zamani pale tx kino ndani ya uwanja wa kanisa la RC na mpira wetu unaitwa nyuzi mbanano bei yake ulikuwa 500. Rafik yangu ndie alikua straiker yeye ndie aliekuwa anaweza kubetua mpira kwa nyuma na kuuleta kwa mbele.
 
Watoto wa siku hizi hawaenjoy maisha kabisa, sana wanawahi kufanya ngono mapema kitu ambacho enzi zetu hakuna!.
Tatizo yale maeneo yote ya wazi wameyafisadi na barabarani hawawezi kucheza magari yamekuwa mengi, enzi zile iliogopwa baiskeli. Ila wababe wa mtaa siku hizi siwasikii kabisa.
 
mwenye mpira alitukuzwa sana.yeye ndo hupanga nani awe ndani na nan out.mtoto wa kishua alikuwa hakosi namba hata kama hana kiwango.
 
Naona wababa,mnakumbushia enzi zenu.Teh

Baada ya mpira kuishi,kasheshe ipo home

Mnanawa miguu badala ya kuoga.LOL
 
Dah! umenikumbusha zamani pale tx kino ndani ya uwanja wa kanisa la RC na mpira wetu unaitwa nyuzi mbanano bei yake ulikuwa 500. Rafik yangu ndie alikua straiker yeye ndie aliekuwa anaweza kubetua mpira kwa nyuma na kuuleta kwa mbele.
Basi mkawa mnamwaminia sana uongo?
 
Naona wababa,mnakumbushia enzi zenu.Teh

Baada ya mpira kuishi,kasheshe ipo home

Mnanawa miguu badala ya kuoga.LOL
Passpot zilihusika sana hasa kipindi cha baridi haogi mtu labda kama hom kuna ubwabwa siku hiyo,
 
mh hapo kinyengwa au kinyengo kinahusika sana
 
Nimeshatoa kucha sana aisee. Kesho naweka plasta naendelea kusakata gozi kama kawaida.

Hizi sheria umenifanya nicheke sana[emoji2] [emoji2] [emoji12]
 
Ishu ilikuwa ni kuufuta mpira kama ukitoka njee ya uwanja then uwanja uwe upo juu ya mlima milimani au uwe pembeni ya mto... Mtapumzika mno..

Ukiwa unatumia mguu wa kushoto hutokosa namba tena 11. Au 6
 
Viwanja havina alama ikitokea penalt hapo hapo inaanza kuhesabiwa miguu 12....yule anaepiga hatua kubwa kubwa wenye penalt wanapinga, anaingia wenye penalt kuhesab hatua akipiga ndogo ndogo wenye adhabu wanapinga kwamba anataka kumumiza kipa wao....yan ni full ubishi na hapo kuwa makini ngumi zinabipiwa hapo
 
Nilikua golikipa mzuri sana na kila nikidaka ilikua napiga sarakasi na mpira, ilimradi kuwe na mbwembwe tu hasa kukiwa na mechi kubwa kubwa! Siku moja tulikua na mechi na mahasimu zetu wakubwa, kama kawaida nikadaka kwa manjonjo weee zile dakika za mwisho mwisho ikapigwa penati, nikaidaka vizuri sana kisha nikaurusha juu mpira nikauzungusha nyuma dahhhh ukateleza mikononi ukaingia golini. Aiseee nilichezea kipondo balaaa hahahaahahaaaaa sio Mimi nilisimuliwa na Babu
 
Kama kwenu kuna Tv hukosi namba na hata kama ulichelewa ukifika uwanjani lazima atafutwe mnyonge atoke.

sisi kwetu tulikua na deki ya mikanda mikubwa VHS afu mwenye mpira kwao hamna na hua anakuja kumcheki vandame aisee kila jion nkitoka tuition nikifika nkikuta mechi ipo kati inaendelea akiniona tu lazma mmoja atoke niingie
 
Back
Top Bottom