Dream Queen
JF-Expert Member
- Nov 4, 2015
- 8,263
- 18,201
Nilikuwa Mtaalamu sana wa kufuma mipira ya Makaratasi hata uwe na kucha ndefu za Miguu au kupiga 'dochi' huwezi kuufumua. 1965-1975 Mission Quatre Kariakoo mkimaliza mpira mnafata Bagia Mnazi mmona
Hakuna tena wababe sasaTatizo yale maeneo yote ya wazi wameyafisadi na barabarani hawawezi kucheza magari yamekuwa mengi, enzi zile iliogopwa baiskeli. Ila wababe wa mtaa siku hizi siwasikii kabisa.
Wish wangeyaonja yale maisha yetu ya utotoni.Watoto wetu,kutwa wapo kwa Play stations,ndio viwanja vyao Eti!
Ha ha hasisi kwetu tulikua na deki ya mikanda mikubwa VHS afu mwenye mpira kwao hamna na hua anakuja kumcheki vandame aisee kila jion nkitoka tuition nikifika nkikuta mechi ipo kati inaendelea akiniona tu lazma mmoja atoke niingie
Hebu tukumbushe na wadada mlikuwa mnacheza nini, vipi kitu rede (sic)?Naona wababa,mnakumbushia enzi zenu.Teh
Baada ya mpira kuishi,kasheshe ipo home
Mnanawa miguu badala ya kuoga.LOL
Magwambara au magaga sio mchezo ni bora ukutane na msasa wa chuma kuliko hiyo miguu kuna jamaa alikuwa nayo unaweza kuweka sent ishirini ikazama bila wasiwasi.Wachezaji wenye machacha ni ngumu kupata Namba kwa hofu ya kupasua mpira ama kuharibu mpira!
Balaa balaa kakaMagwambara au magaga sio mchezo ni bora ukutane na msasa wa chuma kuliko hiyo miguu kuna jamaa alikuwa nayo unaweza kuweka sent ishirini ikazama bila wasiwasi.
Haaaahaaaa mlitsha sana aisee kama mtaani kwetu yaan,goli linaweza kuwa ni mawe au ndala/kandambili. Kama tumeshinda au tupo droo na tunaelekea fungwa ilikuwa ni lazima kulitibua goli, kama ni ndala au viatu utapiga teke moja tu, mfungaji atakosa pa kufungia, kama ni jiwe litarushwa mbali na mechi itakuwa imeisha.
Mpira unaoingia golini hautakiwi vuka juu ya magoti, na ukivuka hapo tu basi hakuna goli, itahesabika umepaisha.
Shule Timu yangu tuliiita new balance sababu wengi tulivaa viatu vya mtumba vilivyoandika new balance.
Kwa home mechi iliisha punde tu sauti ya land rover 109 iliposikika, maana ilikuwa inasikika kona 3 kabla ya kufika home, ushahidi wa magoli ulitibuliwa, kama ni ndala kila mtu alivaa zake, kama ni mawe basi tulitupa mbali, watoto wa majilani walikimbilia kwao, huku tukiomngoja baba kwa nje.
Haaaahaaa umenikumbusha mbali sana na hawa watu waliokuwa wanaitwa nyama kiukweli walikuaga wanapata shida sana uwanjani,hahahahahaha.,.nimekumbuka mambo kibao,kupunguza goli kama mashambuliz yamezidi,ukitukana tu inapgwa faulo,kama kuna refa ukila red unakaa nje dakika 5 na kuingia,filimbi ni mluzi tu.
kuna jamaa alikataa kutoka,tukamtangazia nyama,alipogusa mpira tu,mpinzan alikuja mbio akaingia na miguu minne,jamaa mguu ukateguka na mpira ukaishia hapo,ilikuwa maeneo ya yombo kilakala kwa mzee chakala.kitambo sana.
duh hii kali sana4. Kama timu yetu hatuna viatu, na ninyi vueni viatu
5. Hakuna refa, uamuzi wa mchezo mf. faulo au kona ni makubaliano