Sheria ya Jeshi kuhusu mavazi ni ya kishamba na kizamani sana

Only in Africa wapi sio kila kinachofanyika nje kinatufaa na sisi mbona Kuna mambo tunasema sio sawa yanaenda kinyume na sheria na tamaduni zetu.It is all about law.Fanya mchakato wa kubadili sheria ili tuanzie hapo mkuu.Sheria inakataza mavazi yanayofanana na majeshi for a reason.Hata katika biashara ndio maana tunasajili nembo/Alama,majina ya biashara ili kujitodautisha na ukiiga linakuwa kosa
 
Hivi imagine Kila kitu kinafanana kasoro nembo huoni Kwa tz inaweza kutumika kutapeli au kuonea watu...huko vijijini raia wanajua kweli mambo ya nembo?
Kama jeshi lisingekuwa na sifa ya kuonea watu basi nadhani kusingekuwa na sababu ya kuhofia kwamba raia akivaa nguo yenye kufanana na jeshi ataonea watu.
 
JF bhana.
Kila siku mada za kijinga jinga kuhusu majeshi
Uhuru umewazidi uwezo wenu wa kawaida
Acha kuwa na mawazo ya kidikteta. Anasemwa Mungu litakuwa Jeshi hili la Nguo ??
 
Kwetu watu walionekana kutumia sare za jeshi kutapel
Wakati watu wanafanya huo utapeli jeshi lilikuwa limelewa pombe gani? Kazi ya jeshi ni kuzuia uhalifu siyo kugombea nguo
 
Kwani hao wezi kwenye ripoti ya CAG wanavaa sare za jeshi? Mnaacha uhalifu wa maana, mnahangaika na mambo madogo madogo ya mavazi
Acha kunililia. Mimi sio CDF. Kama vipi Vaa hizo sare zao kisha pita pale Lugalo
Wala sitamani kuvaa hizo nguo zenye kushabihiana na jeshi, maana nina nguo za kutosha. Ninachosema hilo jeshi lijihusishe na mambo ya maana, hizo nguo kuvaliwa na raia linaweza kushughulikiwa na polisi.
 
Nakubaliana yaani Kila mtu katimba mabaka mabaka eti kisa marekani wanavaa! Mbona tunapinga ushoga na marekani wanaukubali?
Kwani ushoga tunaupinga kwa sababu ya Marekani au kwa sababu ya ubaya wa ushoga wenyewe? Tunaweza kuelezea athari za huo ushoga na tukaziona hizo athari hata huko Marekani kwenyewe, sasa huku kukatazana kuvaa nguo zenye kufanana na jeshi athari zake ni kwa Tz tu?
 
Yanini kulazimisha kuvaa nguo za watu waliojitoa maisha yao hadi kufa ili kukulinda wewe. Kwanini hukwenda Jeshini kama unapenda kuvaa mavazi yao? Hujawahi kulipa gharama za kuwa Mwanajeshi unataka kuonekana kama wao. Kuna watu wanakufa mazoezini au kuwa vilema ili siku moja avae vazi ambalo wewe unatamani uvae bure bure tu. APIGWE TU ATAKAYE KAIDI AGIZO
 
Sisi bado tunahitaji maji safi na salama pia tunahitaji umeme wa uhakika na mengineyo kibao !
Hatuhitaji sare za majeshi yetu tuvae kisha wengine wakafanyie utapeli !!
Sio kila kinachofanywa na wale wehu wa huko majuu na sisi tuige ! Big NO !!!
Safi sana Taifa linahitaji Nguvu kazi kama hii...Sio mtu kung'angania kufanyia Unyangema Nguo za Jeshinkwa kigezo cha Majuu wanavaa
 
Ukiwa na vijana (boys) vema kuwazoesha kuvaa mavazi ya kijeshi ili wakue wakiipenda, na hatimaye waje kujiunga na kutumikia jeshini. Vema kueleza kiagaubaga hizo rangi kisayansi, kikemekali, kidesign, texture, density, reflection, strength zikoje. Huko mahakamani ya haki itakuwaje?
 
Anaongea bila kufikiri huyo ,anaweza akavaa tu mtu t-shirt kama y bakabaka yuko kweny Gari akasimamishwa n traffic asisimame, hapa mtakuja kusema mjeda kakataa kusimama.
Nadhani jeshi ndio linatakiwa kubadilika kisha ndio lianze kutumia nguvu kuzuia hizo nguo zenye kufanana na sare zao.
 
Siku hizi Jeshi limeacha show zake za kuvunja tofali kwa kichwa sasa hivi linakomalia nguo?. Very petty issue.

Mimi ninavyojua ni kuwa sheria imekataza kuvaa sare ya majeshi yetu lakini siyo nguo ya mabakabaka ambayo siyo sare ya jeshi lolote duniani.
 
Nyie wote mnaokomalia kuvaa nguo za wajeda, naona mnajikuta much know sana kama kitu kimekatazwa msifosi. Nguo za kuvaa zipo nyingi. Je nao jeshi waseme wavae kama raia mtawachukuliaje? Tusikaze mafuvu yetu ili kuepusha shari na vyombo wa usalama.
Hivi duniani kote wanajeshi wanapenda kuogopewa na raia kama ilivyo Tanzania?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…