Sheria ya Jeshi kuhusu mavazi ni ya kishamba na kizamani sana

Ni kweli usemayo lakini kwa Tanzania watu wanayatumia vibaya hayo mavazi, siyo kwa uzalendo wala fashion.

Ni sawa tu yapigwe marufuku, mpaka tufikie wakati wetu wa utayari.
Hata Marekani kuna wafuasi wa Trump walikuwa wamevaa mavazi mfano wa jeshi walipovamia bunge January 6, 2021 wakitaka Bunge na Mike Pence wasithibitishe matokeo ya Urais wa Joe Biden.
 
Mwanajeshi hana uwezo wa kupiga raia?
Unaongea ukiwa nchi gani
 
Nimemsikiliza askari aliyekuwa akihojiwa na CloudsTV anasema sheria ya mavazi ya jeshi unasema;-
"Ni marufuku raia kuvaa sare za jeshi ama mavazi yanayofanana na sare za jeshi". Ili iweje...
Ukiona kwenye hii dunia ya vita vya drones bado askari wetu wanapasuliana matofali kichwani, hapo ujue tuna jeshi so outdated mno. Ndio maana unaona wanajikita kwenye mambo madogo madogo kama mavazi ya kufanana na jeshi. Jeshi linalofurahia kuogopwa na raia wasio na silaha hapo ni vituko vya karne.
 
Ni kweli usemayo lakini kwa Tanzania watu wanayatumia vibaya hayo mavazi, siyo kwa uzalendo wala fashion.

Ni sawa tu yapigwe marufuku, mpaka tufikie wakati wetu wa utayari.
Kwa umri wako sishangai ukiwa na mtazamo huu. Wazee na watu wasiojitambua ndio wana mtazamo huu.
 
Mkuuu umeongea the voice from within kabisa
 
Nimemsikiliza askari aliyekuwa akihojiwa na CloudsTV anasema sheria ya mavazi ya jeshi unasema;-
"Ni marufuku raia kuvaa sare za jeshi ama mavazi yanayofanana na sare za jeshi". Ili iweje...
Ni kifungu kipi kinachosema kuwa ni kosa kuvaa mavazi yanayofanana na ya jeshi.
 
Lakini Kwa nini na wewe raia utake mavazi ya jeshi lakini??? SI uchokozi huoo ni kumshika mwanaume matako huko
 
Mleta uzi umeandika ujinga mtupu. Kama una hamu ya kuvaa mavazi ya jeshi fanya namna ujiunge nalo na sio kulazimisha kuvaa sare zao zinazoweza kutumika vibaya na watu kufanyia uhalifu. Watu imefikia hatua wanashona kaunda suti na kujifanya wanausalama. TII SHERIA BILA SHURUTI AU HAMA NCHI.
 
Sheria gani ya nchi inayopinga uvaaji wa hayo mavazi yanayofanana na sare za jeshi au kaunda suti za usalama??
 
Wewe ndiyo umegonga mahala pake. "Jeshi siyo sare". Safi sana
 
Tuna wanajeshi wasio na mafunzo. Wapo wapo tu. Kazi yao kujimwambafai kwa kuvaa sare. Bure kabisa.
 
 
Acha uwoga wewe. Mavazi ya jeshi siyo rangi bali ni nembo.
 
Sioni mantiki ya jeshi kukataza lakini sioni mantiki ya raia kukomalia kuvaa ikiwa wameamua hivyo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…