Sheria ya Jeshi kuhusu mavazi ni ya kishamba na kizamani sana

Wapo sahihi. Kwa nini watu wasivae sare za marehemu, sare za wafungwa na wakimbilie za watu wenye mafunzo hatari ya kijeshi?
Sare za jeshi hayutakiwi kuzivaa sisi raia ila sio nguo zinazofanana na sare zao.. huo mi Ujuha.
 
Hivi imagine Kila kitu kinafanana kasoro nembo huoni Kwa tz inaweza kutumika kutapeli au kuonea watu...huko vijijini raia wanajua kweli mambo ya nembo?
Kwahiyo kwa sasa raia hawata tapeliwa tukiacha kuvaa sare za jeshi.... wewe binafsi mara ya mwisho kusikia mtu katapeliwa na mtu aliyevaa kijeshi lini?
 
Mbona wapo wanaotumia sare za shule kufanya uhalifu, hata za mapadri pia zinatumika, kwani askari hawafanyi uhalifu!
Acha kuuliza swali la kitoto jeshi ni chombo chenye mamlaka ya ulinzi wa nchi taswira yake ikichafuka watu watakosa imani ukizingatia wananchi wengi hawajui mambo ya nembo wala nn. Baadhi ya watu wanakuwa disguised kujifanya wanajeshi angali sio hivyo kufanya ujinga wao ukiona hivyo jeshi limefanya tafiti halijakulupuka.
 
Chanzo cha yote ni Siasa na madaraka... Kuna uwaja ulibadilishwa jina kutoka Peoples hadi kuitwa Bombadier... Makatazo yalianzia malalamiko ya mavazi ya walinzi wa mboe.
.
 
Hata Marekani kuna wafuasi wa Trump walikuwa wamevaa mavazi mfano wa jeshi walipovamia bunge January 6, 2021 wakitaka Bunge na Mike Pence wasithibitishe matokeo ya Urais wa Joe Biden.
Marekani na Tz ni nchi mbili tofauti,acheni utoto
 
Akili za kindezi hizi. Jeshi linaheahimiwa kwa mavazi?? Jeshi linaheahimiwa kwa mbinu za kivita na weledi wake. Siyo kuvunjia tofali kichwani na kulingishia raia mavazi
Unaongea kwa kiburi sababu nchi ipo salama sababu ya ulinzi imara wa jeshi,km ingekuwa legelege mambo ya kibiti yangekuwa mabaya zaidi ya Msumbiji,ebu acheni mambo ya kitoto
 
Kuna mambo mengi ya msingi yanayoathiri moja kwa moja ustawi wa jamii na taifa kwa ujumla ambayo wananchi wanatakiwa kuelimishwa. Katika orodha suala hilo unalolitaka laweza kuwa la mwisho kabisa

Sent from my TECNO BA2 using JamiiForums mobile app
 
Ni sababu za kiusalama...lakini pia ukumbe lile ni vazi rasmi, na linapaswa kuvaliwa na mtu rasmi.
 
Mambo ya Kishamba tu.... So Mtu akivaa Tshirt ama Pensi lake la Mabaka... akivunja dirisha nyumbani utamuangalia tu......
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…