Miradi nayogharamiwa na JMT je.
Pili, hao Zanzibar wanadai misaada, hizi nifikra za kijinga sana. Hiyo misaada wanapewa sehemu yake.
Kwa mfano, bajeti ya SMZ inapata ruzuku ya JMT.
Pili, Wazanzibar hawajui malipo ya deni la taifa hata siku moja, na hutawasikia wakiongelea kulipa madeni utawasikia misaada
Tatu, gharama za JMT zinabebwa na Watanganyika hadi kuwalipia wabunge wao na mengine yasiyosemwa kwa stara
Nne, misaada gani mbona hamhoji watoto wenu kupewa ''mikopo'' ya elimu ya juu bure tena wengi kuliko wa SMZ?
Tano, mnachangia kiasi gani bajeti ya JMT?
Sita, hamna bajeti ya ulinzi, mambo ya ndani, nje n.k. Hiyo bajeti ya jeshi tiu hamuwezi hata kwa wiki 3
Saba, kila mwezi mnapata mgao wa benki kuu ambao kimsingi ni mapato ya Tanganyika.
Ngo'eni nyaya za umeme, tafuteni umeme wa upepo au meli.
Hizi habari za kuwabebesha raia wa Buguruni zigo la SMZ zifike mwisho.
Raia wa Mbagala analipa LUKU , SMZ haitaki kwasababu haitaki tu. Hii ni fedheha wala si aibu.
Raia wa Bunju anajua wajibu wake kwa familia yake kwa kulipa umeme, halafu anabebeshwa zigo la Zanzibar! Shame on you. Haya si mambo ya kuzungumzia Wazanzibar, yanawaacha ..ashakumu
Msisumbuke kutoa taarifa, acheni kununua umeme wa Tanesco, ugomvi hakuna