Katika , hali ya kutatanisha , shule ya masister inayomilikiwa na Kanisa katoliki mkoani DODOMA iitwayo HURUMA secondary school, imezua vurugu miongoni mwa wazazi wa vijana wa kidato cha nne .
1. Shule hiyo inadaiwa kuondokewa na waalimu wao mahili katikati ya maandalizi ya NECTA ijayo , vijana hao wa kidato cha nne wengi wao hawawezi kubadilisha shule/ kuhama shule kwa sasa , hivyo wanalazimika kubaki shuleni hapo kulinda usajili wao.
Mkuu wa shule hio anadaiwa kuwazuia wanafunzi wote wa kidato cha nne na kuwataka walipe fedha za kufundishwa TUITION kipindi cha likizo ijayo JUNE 2023 kwa kua wanajua shule hio haijawafundisha watoto hao baada ya kuondokewa na waalimu .
Wazazi waliowengi wanatamani wanafunzi wapewe uhuru wa kuamua kurudi kwa wazazi likizo ili wapate masomo ya ziada binafsi kwa waalimu wenye uwezo kuepusha kufail kwenye mtihani ujao .
2.Wazazi wengine wamelalamika pia , tetesi za shule hio kuwa na wanafunzi wanaojihusisha na mapenzi ya jinsia moja , hivyo wanaomba watoto wao warudi likizo kuepusha madhara zaidi ya kimaadali
RAI yangu kwa wizara ya ELIMU ,na TAMISEMI PIA, fuatilieni mienendo ya kimaadili kwenye shule hii ya masister iliyopo DODOMA kuna tabia za kimagharibi ambazo wazazi wanashindwa kuzisema waziwazi maana zinadharirisha utu wa watoto wao , ndio maana wengi wanataka watoto wao warudi likizo waongee nao .
==========UPDATES===========
Shule inagoma kuwaachia watoto kwa kuhofia tetesi hizo za usagaji zinaweza kuenea na kupelekea kufungwa au kuchunguzwa