MAONI YA MBUNGE JUMANNE KISHIMBA KUHUSU SEKTA ELIMU TANZANIA, KWETU USUKUMANI DINI YA JADI NI WENGI KUPITA DINI ZA KIGENI
5 April 2024
MH. JUMANNE KISHIMBA (MBUNGE NA MFANYABIASHARA MKUBWA) KATIKA MAONGEZI :
UCHUMI NI MATUMIZI PART 2
View: https://m.youtube.com/watch?v=oiiHH-pgamEMfuatilie Mheshimiwa Mbunge Jumanne Kishimba akieleza umuhimu wa matumizi ambayo yanaweza kuufanya Uchumi uwepo, usimame au usiwepo na ufe.
Shida ya vijana kukosa ajira nini tufanye kama nchi ? Ni vyuo vikuu kukosa kuunganisha masomo na mahitaji ya mazingira nje ya chuo hivyo ni muhimu vyuo na wizara ya uwekezaji kufanya kazi hiyo.
Miaka inakwenda wanafunzi waanzie wapi? Sisi tuna mitaji ya mamilioni tunapeleka mamia ya ngombe zetu tunalala ktk vitanda vya double decker lakini mwanafunzi wa chuo kikuu hajui kubana matumizi kutokana na ubongo wake kuchakachuliwa na ustaarabu kuwa hawapaswi tena kulala ktk kitanda cha double decker.
Waliomaliza elimu ya vyuo vikuu wanapoanza maisha kutokana na mshahara hivyo hawataweze ku 'save' wawekeze ktk biashara inayoleta mapato endelevu badala ya kukabiliana kununua usingizi kwa mikopo ya nyumba au mkopo wa gari ili aishi ilivyopandikizwa chuoni kuwa wao ni watu special..
Wanafunzi wanaomaliza vyuo vikuu hawarudi nyumbani au vijijini hivyo miji ya wazee wao ambayo ni mitaji kama mashamba na mifugo inakufa hivyo familia zinakosa muendelezo wa maendeleo ya kiuchumi yaliyoanzishwa miaka mingi.. mfano jamii yetu ya kihindi hawakati mnyororo ulioanzishwa na wazazi wao tofauti nasi wamatumbi ambao tunaukata mnyororo wa utajiri walioanzisha mababu zetu ktk mashamba, mifugo, uvuvi n.k
Kombinashe nyingi ikiwemo masomo ya dini, kichina na mitaala mipya isiyo endana na mazingira yetu n.k mbunge Jumanne Kishimba anasema imesahaulika dini kubwa za kienyeji ambazo zina watu wengi kuliko ukristo au uislamu.
Kwanini imani hii ya kienyeji yenye mambo mazuri zimepuuzwa ktk ngazi za shule za sekondari na elimu ya juu na kubwa mila za wenyeji ambazo zinasisitiza utaratibu wa maisha kama tabia njema, kutoa ahadi za kuaminika, kutekeleza ahadi, kujaliana n.k
Tunakopi sana mambo ya wageni na kusababisha gharama kubwa za ustaarabu wa kigeni na kupelekea maisha kuwa magumu, pesa kutohifadhika kwa kuwa hatuna mipango ya matumizi na kukua uchumi kwa kiasi kikubwa ni kudhibiti matumizi ...
Hakuna ukomo wa uwekezaji hivyo kila mmoja asiwekeze ktk usingizi yaani nyumba ya anasa ya gharama kubwa au gari bali katika mtaji wa biashara ya kuingiza mapato anasisitiza mbunge Jumanne Kishimba ... na hii elimu ya vyuoni na shuleni ni elimu ya zamani sana na haiendi na kasi ya mabadiliko ya ulimwengu tulionao...
Rasilimali, teknolojia na wingi wa watu ...
Source : sociology tanzania