Siasa za ajira za GPA na hatma ya vyuo vyetu vya Madaktari Tanzania

Nilishaona vyuoni huku nikama kutesana, kunyanyasana, kuzarauliana tu, nakumbuka prof.mmoja pale Sua siku moja anatuambia ili mgraduate mpaka nione jasho la damu linawatoka, nikaja kumuelewa semista ya mwisho, aise halikaza paper kila mtu alikohoa kwenye mtihani
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa uelewa wangu mdogo neno ‘Diploma’ lilitumika kabla ya mfumo wa Bologna kuanza kutumika mwaka 1999. Ikijulikana kama the Bologna Process, mfumo ulileta standardisation kwenye elimu ya juu Ulaya, na kuleta mageuzi kwenye aina za digrii. Ulitoa hiyo ‘Diploma’ ambayo ilikuwa ikitolewa kwa miaka 5 kama sikosii, na kuigawanya kwenye miaka 3 ya Bachelor na miwili ya Masters. Pia ulileta mfumo wa ‘semester’.
 

Sasa chief, kama nimekuelewa vizuri, pendekezo lako litakuwa halitibu tatizo, bali linalipoza tu.

Kwanini ninyi mlioko huko vyuoni msipiganie upatikanaji wa mazingira ‘supportive infrastructures’ ili kutoka kwenye ufundishaji wa ki-manually kama unavyosema? Naamini hii ndiyo itakuwa tiba ya kudumu.
 
Mkuu mleta uzi anafikiri yeye ndiye anajua kila kitu na wakati hayuko focused na anachokitaka na ndio maana nilijitoa nimuachie dimba kwani hayuko tayari kwa mawazo ya wengine. Kiufupi lengo la kuleta uzi hapa jukwaani ni kutaka members wenye experience na mawazo mbadala wachangie, sasa kama yeye tayari ana hitimisho la hoja angeandika kila anachofikiri kifanyike ili wengine tugonge like kusupport tu.
 
Kumwambia kipofu atazame ni kupoteza muda!
 
Kumwambia kipofu atazame ni kupoteza muda!

Wewe una uwezo wa kuona wenzio ni vipofu?

Wewe sio kipofu?

Huu uwezo uliupata wapi?

Au kwavile wewe ni “daktari”?

Hii self aggrandization unayoonesha is not from this planet aisee!

I see!
 
Tiba mojawapo kuboresha miundombinu ni kuongeza wakfunzi wenye uwezo ktk vyuo vikuu vya madaktari! Hawa wapo mtaani lakini wamezuiwa na 'unrealistic criterion' (GPA). Hebu rejea hoja ya msingi pale mwanzo kabisa! Unapokuwa na Mkufunzi mmoja au hakuna kabisa (ukitegemea wa kuazima) ktk idara inayohitaji wakfunzi angalau watatu, kufundisha mamia ya wanafunzi! . Ubora wa kinachofundishwa hauwezi fikia lengo tarajiwa! Wanafunzi ndio watakao athirika zaidi!
 
Kumwambia kipofu atazame ni kupoteza muda!

Sikutaka kuchangia hii mada, lakini naona ngoja nitie neno. Elimu ya Muhimbili sio ngumu kiasi cha watu kushindwa kupata GPA za 4 kwenda juu. Shida ni walimu wenu hao wana mambo ya kizamani. Kinachotakiwa ni walimu kubadilika na sio GPA kushushwa.

Kitu kingine cha kuchekesha ni kuona kwamba wewe mwalimu( kama kweli) unalalamikia GPA wakati ni nyie wenyewe ndio mmeweka hicho kiwango.

Mwisho kabisa ondoa hiyo notion kwamba products za Muhimbili ni bora. Labda siku moja ukikaa chini na mtu aliyesoma Havard au Yale utagundua kwamba hicho unachokiona bora ni punje ya haradali.
 
Mimi sio kuwa nafahamu kila kitu, nime'share' experience' ya uhalisia wa changamoto za upatikanaji wa wakfunzi ambazo vyuo vyetu vya kutengeneza madaktari wetu zinapitia na kuonyesha moja ya sababu kuu inayochangia tatizo hilo ambalo ni la kujitakia, pia nilitoa na namna bora mojawapo ya kulitatua hilo ili kupunguza au kulimaliza kabisa!
Waswahili wanasema, kilio kina mwenyewe… changamoto hizi tunaziishi tuliopo mavyuoni (wakuu vya vyuo, wakfunzi na wanafunzi). Wakfunzi wachache waliopo wanafanya kazi kubwa sana kujaribu kufidia ukosefu wa wakfunzi husika, lakini ubora wa ufundishaji unaathirika sana! Na wahanga wakubwa zaidi ni wanafunzi wetu ambao mwisho wa siku wanaishia kupata makalayi na tunaanza kuwahukumu kuwa GPA zao ni ndogo!
 
Eti kupata GPA 4.0 sio ngumu…Unataka wahitimu wapate GPA 4.0, huna walimu baadhi ya idara, unaazima mwalimu wanakuja fundisha sehemu ya kufundisha kwa miezi 5, anafundisha na kumaliza mwezi 1 au 2, na akitoa mtihani unatarajia mwanafunzi apate 'A' ili mwishowe awe na GPA 4.0!
Walimu kubadirika ni kauli pana sana, na hata kuipima kwake ni kugumu sana, hizi ndio huwa naziita porojo! Shida iliyopo waalimu ni wachache sana, pili vitendea kazi navyo ni duni! Mwisho wa siku mwalimu anatakiwa ahakikishe mwanafunzi huyu anahitimu akiwa na uwezo wa kutibu pasi kuleta madhara kwa mdonjwa.
Hii inampa wakati mgumu zaidi mwanafunzi kupanda mlima ulioletwa na uchache wa waalimu, na miundombinu wezeshi mingine kuwa duni!
Msingi wa hoja yangu kuondoa umbwe la waalimu, kwa kurejea upya vigezo vilivyopo vya upatikanaji wa waalimu ili tuwe waalimu mahili wa kutosha kuwezesha wanafunzi kufikia malengo yao kwa wepesi!
Sijasema mimi product za Muhimbili ni kuwa bora kuliko za Havard, ila kwa mazingira yetu, vyuo vyetu vya madaktari vinajitahidi sana kutoa wataalamu wa afya wenye kutatua matatizo ktk jamii yetu kwa kiwango kikubwa sana hata wa kuliko wa mataifa yalioendelea (including Havard).
Nikuhakikishie Noel, ukimleta aliyesomea Havard, intern aje fanyia hapa, atapata taabu sana kwa mazingira tuliyo nayo. Atahitaji 'adjustment za kutosha kabla hajaweza endana na mazingira yetu…kwa hiyo naweza kusema wahitimu wetu wapo vizuri kuendana na mazingira yetu.
Hata aliyehitimu MUHAS na vyuo vyetu vingine akienda kufanyia kazi havard, atahitaji 'adjustment' za kutosha, lakini kizuri ni kwamba kwake yeye atakula bata zaidi kuliko huyo anayetoka Havard kuja bongo!
Kuhusiana na GPA, nafikiri unajitekenya na kucheka mwenyewe, kigezo cha GPA kilipangwa na wakuu wa vyuo (maVC) siyo kila mwalimu alihusika! Na ki msingi wakuu wa vyuo vikuu vya madaktari pasi kujiuliza wali' adopt' hizo cut-off GPA bla kuangalia uhalisia.
 

Mwamba ngoma huvutia kwake. Unaweza kuniambia utofauti wa ratio ya walimu kwa wanafunzi kati ya Muhas na vyuo vingine ?
Na kwa ufahamu wangu mdogo Muhimbili ina resources nyingi ukilinganisha na hivyo vyuo vingine kama Kaihiruki, Bugando, na KCMC.
Tatizo ni walimu, wabadilike waache zile elimu za kukomoana.
 

Narudia tena na tena, kupata gpa ya nne sio ngumu. Ni mfumo wa usahihishaji wenu tu walimu sio mzuri.
 
Oh, samahani sana kama nimeeleweka hivyo! Nafikiri kila mtu achangie, kikubwa uchangie huku unaelewa swala zima lilivyo, lengo likiwa kusaidia kutatua tatizo ukiwa na utimamu wa akili (bila mihemko). Nilichokiandika ni kile nachokiishi, sina lengo la kuonyesha kuwa mimi ndie najua kila kitu kama ww unavyotaka kuaminisha umma!
 
MUHAS ya sasa imebadirika saana, kukomoana kumepungua saaana sasa hivi, miaka ya 2000 kurudi nyuma ndio ilikuwa balaa, nakumbuka ukipata 'A' walimu waliitana ili kudhibiti, mwalimu anakosa raha kabisa kuwa ametunga mtihani rahisi sana au umevuja! Siku hizi 'A' mbona zinapatikana tu. Shida imekua ku'maintain' ktk idara zote, zaidi ya 16 anazopitia mwanafunzi!
 
GPA haipimi mgonjwa ila GPA ni indication kwamba ulikua serious na masomo na kama ulikua serious na masomo basi utakua serious kwenye kupima/kutibu wagonjwa.
Mkuu GPA na Application Ni invesre relationship.
Mara nyingi mtu Alie na GPA kubwa vitendo huwa Ni zero kabisaa.
Nashauri kada Kama za udaktari watu waangaliwe ujuzi walionao Katika Afya na Wala siyo GPA iliyopo kwenye makaratasi.

Kumbuka: Ni ukweli usiojificha kuwa Elimu yetu ya Tanzania Ni ya makaratasi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Narudia tena na tena, kupata gpa ya nne sio ngumu. Ni mfumo wa usahihishaji wenu tu walimu sio mzuri.
Acha kuchekesha wasiotaka kucheka ndugu yangu! "Strictness is one of the hallmark in medicine". You either know or you don't know! Hii ni kwa usalama wa wagonjwa baadaye. Mwanafunzi anatakiwa kujuwa na kufikia kiwango kinachotakiwa kutibu mgonjwa bila kuleta madhara. Hii haijarishi ni mazingira wezeshi ya aina gani huyu mwanafunzi amepitia. Mhitimu wa udakatari aliyemaliza intern, huyu tayari ni salama kutibu mgongwa. Ndio maana nikasema, tuboreshe mazingira ya kuwawezesha wanafunzi wetu ambao kimsingi uwezo wanao mkubwa sana ila shida ni mazingira. Kwa kuanzia, wawepo walimu wa kutosha, tupunguze ukiritimba ktk ajira za wakfunzi wa udaktari.
 

Mfumo wa kuangalia GPA peke yake unatuletea majanga sana.. Ni vyema huu mfumo ukaangaliwa upya hasa tuwe na aptitude test ya kugrade interviewees.. Unakuta mtu amesoma chuo kibonde kama IMTU au St Joseph pale lakini GPA yake inasoma balaa wakati matokeo yake ya form 4 na 6 ni dhaifu sana ukilinganisha na aliyesoma Muhimbili.. Ni wazi ukiwapa APtitude test hawa watu utagundua jinsi gani viwango vyao vilivyopishana tofauti kabisa na GPA..

Kwa nini GPA haitoshi? Tukipima job seeker tunasaka sifa nne sifuatazo;
1. Communication
2. Creativity
3. Problem Solving skills
4. Skills in Innovation

Ukiangalia kwa upana hapo GPA haikupi picha kamili maana hata mitihani wanayopewa chuoni huijui na huwezi kujua walimu wao walipima nini hasa.. Kimsingi wengi wanapimwa kwa uwezo wa kukumbuka jambo "Memorization skills".. Hili wala halitusaidii kabisa.


Ni vyema TCU wakakaa na kusolve hili jambo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…