Sijui kama nimekuelewa unataka nisemeje!
Nachokumbuka tulipokuwa intern pale Muhimbili miaka hiyo, hawa jamaa waliokuwa wanakuja na vyeti vya misonge ('A') kutoka urusi na uarabuni walikuwa wanaitwa MD-russia yaani ni vilaza maana walikuwa wanapata wakati mgumu sana kwa mchakamchaka wa machief pale Mubimbili na wengine waliishia kukimbia kabisa. Mimi pia nilihusika pia kuwasaidia saana hasa katika ku'manage' wagonjwa! Kiukweli walikuwa wamepauka sana ukilinganisha na misonge iliyokuwa kwenye vyeti vyao. Ilibidi wafanye kazi saana mpaka kuweza maliza intern salama. na kimsingi walipopitishwa kwenye tanuru la muhimbili walitoka wakiwa vizuri kwa walioweza pita salama.
Elimu ya urusi imeandaliwa na pia kuwa na miundombinu wezeshi za huko huko urusi! Inapoletwa tanzania bila kuwa na miundombinu wezeshi yake hapo ndio shida inapoanza tokea! Kwa hiyo haitoi majibu ya changamoto zetu za huku kwa ukamilifu wake.Je huko Urusi huduma za afya zikoje? Usitake uniambie URUSI ni wajinga kaisi kwamba wawe na elimu ya hovyo kwenye Matibabu.
Sent using Jamii Forums mobile app
Tatizo vyuo vyetu havina standard yoyote wa muhas anapata gpA ndo wakati yule wa wa imtu ambaye anafundishwa na mwalim yule yule anakuwa na gpa kubwa
Wa IMTU anafundishwa na mwalimu wa part time wa MUHAS ambaye continuation ya kupata contract yake kifundisha IMTU ipo tied na wanafunzi wake wa huko IMTU kufaulu afterall hiyo ni private institution! So anakuwa lenient kidogo huko imtu!
Sent from my iPhone using JamiiForums
GPA (namaanisha iliyo patika kwa kusoma na kuelewa) inaonyesha mtu yuko vizuri kichwani anaweza ku analyse mambo na kuja na solutuion mbali mbali zitakazo tatua tatizo.
Sasa akiwa na uwezo mzuri wa ku analyse mambo na akiwa mzuri kwenye kufanya vitendo basi huyo ndiye almasi nnayoitaka! sitaki mtu ambaye yuko nusu nusu!
Umeelewa?
Muhimbili mna-complicate pasipo sababu. Mnaponda waliisoma nje lakini ndipo wengi wanapoenda kutibiwa na kupona nyie mmekalia semina na kukamata wanafunziSijui kama nimekuelewa unataka nisemeje!
Nachokumbuka tulipokuwa intern pale Muhimbili miaka hiyo, hawa jamaa waliokuwa wanakuja na vyeti vya misonge ('A') kutoka urusi na uarabuni walikuwa wanaitwa MD-russia yaani ni vilaza maana walikuwa wanapata wakati mgumu sana kwa mchakamchaka wa machief pale Mubimbili na wengine waliishia kukimbia kabisa. Mimi pia nilihusika pia kuwasaidia saana hasa katika ku'manage' wagonjwa! Kiukweli walikuwa wamepauka sana ukilinganisha na misonge iliyokuwa kwenye vyeti vyao. Ilibidi wafanye kazi saana mpaka kuweza maliza intern salama. na kimsingi walipopitishwa kwenye tanuru la muhimbili walitoka wakiwa vizuri kwa walioweza pita salama.
Pole sana Mtonzi na Mwanagenzi
Kama huna Undergraduate GPA 3.8 nenda Halmashauri hukoo
Lakin ukiaplay master nje wanalijua hilo au hata hapa ndani tu utaoneka disqualified be because of lowa gpa over
Sent from my iPhone using JamiiForums
Kwanza ni kandarasi na sio "kandalasi"Hata huko kwenye uinjinia kwenu, hivi mmekwama wapi na GPA zenu kubwa mbona kandalasi zinachukuliwa na watu wa nje.
Na mnapopewa mnaharibu majengo na miundombinu…tena kwanza ebu tupishe hapa naona mnayo makandokando mengi sana yaliyowashinda! Yashughirikieni kwanza yenu!
Siyo kwamba sisi wakufunzi wa vyuo vya udaktari tunakamata wanafunzi, isipokuwa miundombinu tuliyonayo siyo rafiki kwa mwanafunzi wa udaktari kufikia viwango vinavyotakia kuwa daktari salama. Kwa maana nyingine, ni kama watu wawili wote wanahitaji kufika point X, mmoja anabaiskeli na mwingine ana pikipiki! Ni wazi wa baiskeli itabidi afanye kazi ya ziada ili kuweza fika point X kwa wakati. Huyu anayetumia pikipiki ni sawa na hao wanaosomea udaktari ktk vyuo vilivyoko nchi zilizoendelea kwenye mazingira rafiki!Muhimbili mna-complicate pasipo sababu. Mnaponda waliisoma nje lakini ndipo wengi wanapoenda kutibiwa na kupona nyie mmekalia semina na kukamata wanafunzi