Siasa za kindugu, umwagaji damu na Ukatoliki nchini Ufilipino

Pandora box linazidi kufunguka, kwahiyo ni kama Wakatoliki walikubali au kupitisha mswada wa 'mfalme' kuuawa 🧐🤔
 
Ndugu MPWIMBE, hakuna haja ya kufanya mjadala kwa ghandabu.

Tunajenga nchi moja na wala hakuna anayefurahia unyanyasaji ambao watanganyika na wazanzibari wamefanyiwa. Pengine nadhani tunapishana padogo sana, hebu jaribu kunielewa tena katika hili.

Mosi, TEC wamekuwa wakikemea maovu na kuonesha misimamo yao ya kisiasa tangu awamu ya kwanza. Hili ni muhimu kulifahamu kama msingi wa mjadala wetu.

Pili, TEC wamekuwa wakivutana hadi na viongozi wa kikristo akiwemo Mzee Nyerere na Mzee Mkapa. Minong'oni inasema Mzee Mkapa alishawahi kwenda kupiga magoti kwa Kadinali kuomba msamaha (Hii ni minong'ono tu haina ushahidi). Swali, je kweli Samia anapingwa na TEC kisa uislamu wake au kuna jingine ???

Tatu, TEC kama taasisi inayoongozwa na watu ni FALLIBLE. Kuna makosa mengi ya kihistoria ambayo mbali na mauaji haya ya kukosolewa, jambo ambalo naunga mkono asilimia 100000%, kanisa liliwahi kukosea kwa kuleta udini hasa kwenye suala zima la utoaji elimu. Hili ni kosa ambalo wengi hatupendi kulisema. Kitendo cha kutaka wasomi wawe Wakristo tu limelichafua kanisa mpaka leo hii. Yalikuwa ni makosa na Mzee Nyerere alirekebisha kwa kujenga umoja wa kitaifa. Swali langu hapa ni hili: Je, ni sahihi kutumia haya makosa ya kihistoria kujaribu kuifunga mdomo TEC pale inapokosoa serikali ??? (Nikatoa mfano wa Prof Richard Wolff vs Prof Jordan Peterson)

Nne, nimetoa mfano wa kimuktadha wa UFILIPINO nikitegemea kwamba wengi baada ya kusoma wangeenda kufanya utafiti zaidi na kufahamu nini kimemkuta bwana Rodrigo Duterte ambaye aliua maelfu ya watu na kanisa lilipomkosoa kupitia BARAZA LA MAASKOFU (CBCP) la Ufilipo alianzisha vita dhidi ya kanisa kwa kusema hawatakiwi kumkosoa kwasababu hawana MORAL AUTHORITY kutokana na makosa ya kihistoria na makosa binafsi. Leo hii Duterte ameiingiza familia yake kwenye mgogoro mkubwa na yuko ICC, lakini CBCP ambayo maaskofu wake waliuwawa na kutekwa bado ipo inaendelea. Nilitegemea kwamba wengi mngekuwa mshang'amua maana huu ni mfano hai.

Tano, kwasasabu huu ni mjadala endelevu nilitegemea kwamba tungezungumza kwamba huu mgogoro ambao upo kwasasa na una lengo la kuligawa taifa, ulianza lini ??? Kama kawaida wengi tunaangalia dalili bila kuchimba kiini cha tatizo (We look at the symptoms not disease). Viongozi wa kidini kuanza kutekeswa na kushambuliwa ilianza kipindi cha awamu ya nne. Tuliona mapadri wakishambuliwa kwa risasi kule Zanzibar, huku mwingine akiuwawa.

Kipindi cha JPM ambaye ni Mkatoliki mambo yalikuwa mabaya kupita kiasi kwasababu Mapadri wengi walikimbiziwa uhamishoni kwasababu alikuwa anawawinda. Kilichoshangaza zaidi ni kwamba Maaskofu walisaidia sana kumuweka madarakani bwana JPM na alikuwa ni kijana wao wa seminari. Haya yote ambayo anafanya leo hii Samia kushambulia mapadri yana mlolongo mrefu (The did not just exist in a vacuum, it's a long-coordinated government policy)

Sita, mambo haya mwisho wake ni hasa utakuwa nini hasa linapokuja suala la usalama wa nchi. Tanzania hakuna UKABILA ila kuna UDINI sana. Kweli imeshindikana kwa CCM+BAKWATA+TEC kuyamaliza haya mambo nyuma ya pazia kweli ??? Ni ukweli usiopingika kwamba CCM+BAKWATA+TEC ni moja kati ya nguzo muhimu sana kwa usalama wa nchi na ukanda huu. Kuna taarifa nyeti huwa hazitakiwi kufika hadharani kwasababu huwa zinaleta hisia kali baina ya wafuasi.

Alichokifanya Samia siku ile kilikuwa Unprecedented, lakini hata yeye ni zao la tatizo. Tatizo kubwa limejificha kwa chini ambapo hata akiondoka litaendelea kuwepo endapo hatutakubali kukaa chini na kujisahihisha. Hata haya mauaji wengi tuliyazungumzia humu tokea mwaka 2015 mpaka kufika sasa kwasababu tuliona mazingira mabaya. Hivyo hata Samia akiandoka nchi haiwezi kuwa na utulivu. JPM aliondoka na mambo yakawa mabaya mara mbili, unadhani Samia akiondoka ndiyo tatizo litatulia ???
=================================================================

TANZANIA ilifanya makosa mengi sana miaka zaidi ya 30 iliyopita na mnachokiona sasa ni matokeo tu. Ukiamini kwamba Samia ndiyo tatizo pekee utakuwa unajidanganya na nimeona niwaambie ukweli wote leo bila kuuma maneno. Huko ndani hali ni mbaya na hakuna maelewano na watu wanataka kugawana mbao.

HAKI LAZIMA IPATIKANE, lakini TRANSITIONAL JUSTICE inahitajika hapa. Twende kwenye kiini cha tatizo siyo dalili hizi. Haya muaji ya 2025 ni madogo ukilinganisha na mauaji mengine yatakayotokea siku za mbeleni. Rwanda kabla ya Genocide ya 1994 kulikuwa na muaji mengine makubwa mno, lakini watu kwakupenda kupuuza wakaona siyo ishu. Yalipotokea mwaka 1994 hakuna aliyeamini na kila mtu akawa muhanga.

============================================================
NATAMBUA HIZI MADA huwa zinaleta sana hisia kali, lakini wewe kama msomi hutakiwi kupelekwa kama WIMBI LA MAJI. Lazima ukubali kufanya mijadala inayouma ili uweze kufahamu upande mwingine unawaza nini. Mbali na kutumika kwa karata za Udini, kuna baadhi ya madai ya Waislamu yamekuwepo hapa Tanzania kwa miaka mingi bila kuzungumzwa kwa uwazi. Samia alipowahadaa waislamu kwamba atawasaidia madai yao wengi wamemuunga mkono kwenye huu ufedhuli wake. UKISHINDWA KULIFAHAMU HILI BASI TENAAAAA.
​
 
SAWA MKUU, binafsi I rest my case...

TUOMBE UZIMA, muda utaongea....
​
 
Jikite kuthibisha shutuma zako dhidi ya chombo rasmi, taasisi inayowakilisha wakatoliki Tanzania. Hao ndio uliowashambulia.
Taasisi ni watu.

Watu wanaongooza taasisi ya TEC ni MAASKOFU.

MAASKOFU wetu walihujumu mchakato wa KATIBA na ESCROW.
=============================================================
Hili nalo limekuwa gumu kueleweka kweli ???
​
 
Taasisi ni watu.

Watu wanaongooza taasisi ya TEC ni MAASKOFU.

MAASKOFU wetu walihujumu mchakato wa KATIBA na ESCROW.
=============================================================
Hili nalo limekuwa gumu kueleweka kweli ???
​

Kwanini serikali, vyombo vyote vinakuwa na msemaji rasmi. Mfano ikulu sio kila mtu anayefanya kazi ikulu anaweza kusema chochote kuhusu ikulu.

Vile vile wizara zote, serikali, taasisi zote kubwa kama Polisi, Jeshi, BOT. Mtu anaweza kuongea akijiwakilisha mwenyewe. Ukitaka taarifa rasmi unaenda kwa msemaji rasmi wa taasisi husika.

Mimi pia nashangaa kuna ugumu gani kuelewa hili.
 
Sasa mtu kaua, umekubali kaua, Wakatoliki wamemsema kaua, halafu unawalaumu Wakatoliki wadini?

Mimi ni atheist siamini katika kuwepo Mungu, lakini kama udini ni kuwasema wauaji, udini huu nauunga mkono.
Fuata mlolongo wa mada, nimesema mengi tu katika hili.

SAMIA ni muuaji na hawezi kupona kwenye hili.

Ila UKWELI NI KWAMBA, Samia siyo Ugonjwa bali dalili za ugonjwa uliofichika.

Mpaka mambo kama haya yakatokea unaona dhahiri mvutano wa wazi hivi basi fahamu kuna mlolongo mrefu. Taasisi za serikali haziwezi kutumika kupambana na TEC kama hakuna uratibu mkubwa kwenye ngazi za kitaifa (Coordination At State Level). Hapa tumefikaje ???


====================================================
Nimeuliza maswali mengi tu:
- Je, TEC wanamshambulia Samia kwasababu ya dini yake ???

-Je, TEC hawakuwashambulia viongozi wakristo kama Kaisari, Mkapa na JPM ???

-Je, kanisa liliwahi kufanya makosa ya udini wazi-wazi huko nyuma na hata sasa kwenye mambo kama MCHAKATO WA KATIBA na ESCROW. Lakini, je ni sahihi kusema TEC hawatakiwi kukemea ouvu kwasababu hata wao wana makandokando ????

-Je, nini kitakuwa ni mwisho wa huu mvutano mkubwa baina ya TEC+CCM+BAKWATA taasisi ambazo zinasaidia sana kwenye utawala wa Tanzania hasa masuala mazima ya usalama ???

-Je, Samia akiondoka hata kesho na Dr.Nchimbi kuwa Raisi mambo yatatulia na kurudi kawaida, endapo hatutakubali kuangalia mzizi wa tatizo ???
===================================================================

Waislamu wamekuwa wakilalamika kuhusu CCM miaka nenda rudi na wamekuwa na madai yao ya msingi kabisa ambayo yanahitaji majibu siyo kushambuliwa. Samia amewahadaa waislamu kwa kuwapa ahadi kwamba atashughulikia madai yao ndiyo maana wengi wameingia kwenye mkumbo wa kumuunga mkono wakiamini kwamba wanapingana na UTAWALA WA MFUMO KRISTO (Jambo ambalo sidhani kama kweli lipo, japo udini unaonekana baadhi ya maeneo)

Mfano kipindi kile Prof Malima amesema zianze kutumika INDEX NUMBER kwenye MITIHANI YA TAIFA, ghafla ufaulu wa waislamu ukaenda juu. AU kipindi kile Prof Joyce Ndalichako amekutwa waziwazi kwamba baadhi ya watoto wa Kiislamu wamefelishwa kwa maksudi na NECTA, ila baada ya kurudia kusahihisha wakakutwa wamefaulu. Kwanini watoto wa Kiislamu tu, siyo watoto wa Kilutheri ??? Huu ulikuwa ni UZEMBE au MKAKATI MAALUMU ???

SASA mambo kama haya yemechangia sana sisi kama nchi kufika hapa tulipo. Ubaya zaidi ni kwamba hatupendi kuambiana ukweli na tunaamini kwamba taasisi za kidini ni INFALLIBLE and BEYOND REPROACH.
==============================================================
ENIWEI kaka it's always good to see you.

Happy New Year Amigo...
​
 
Endelea kutema madini. So much to learn from you.

Ni kama umeishia njian.

Objective analysis, ila ukweli the church kwa maana ya Roman Catholic unaliatack ndivyo unaliimarusha na kujijengea anguko lako.

Ukitaka kutawala vema align na hawa watu, kosea, kubali makaosa, onyesha unajutia na unafanya juhudi kurekebisha.

The interst of the church ni wellbeing of the community ndio maana lenyewe binafsi linafanya juhudi hizo.

Asante sana mkuu kwa andiko lako.
 
Ndugu MPWIMBE, hakuna haja ya kufanya mjadala kwa ghandabu.​
Hakuna MJADALA TIMAMU uliojengwa kwenye UONGO, ILLUSIONS na STORI ZA KUFIKIRIKA.


Unataka mjadala TIMAMU jenga hoja kwenye USHAHIDI.

Tunajenga nchi moja na wala hakuna anayefurahia unyanyasaji ambao watanganyika na wazanzibari wamefanyiwa. Pengine nadhani tunapishana padogo sana, hebu jaribu kunielewa tena katika hili.​
Hufurahii unyanyasaji, ila wanaopinga unyanyasaji WANAKUKERA.

Kasimulie wajinga hizi stori.

Mosi, TEC wamekuwa wakikemea maovu na kuonesha misimamo yao ya kisiasa tangu awamu ya kwanza. Hili ni muhimu kulifahamu kama msingi wa mjadala wetu.​
Binafsi, sijawahi kuona TAMKO la TEC la Kisiasa, kama lipo liweke hapa.

Matamko ya TEC ni ya KIBINADAMU, KIUTU na KIJAMII kama UHAI, HAKI ZA KIRAIA na KIBINADAMU.

Sijaona TAMKO la TEC la kusema WANANCHI WACHAGUE MTU FULANI. Kama lipo liweke.

MAUAJI, WIZI, UPORAJI, RUSHWA, DHULMA siyo SIASA.
Kupiga magoti kwa KADINALI kama Nani??

ALikuwa kiongozi wake wa Kiroho au kama nani??

Maana Kadinali siyo kiongozi wa Maaskofu Katoliki kama ambavyo vibuyu wa CCM wanaamini.
Udini upi?

Hebu share hapa huo udini ulioletwa na TEC kwenye elimu.
Hili ni kosa ambalo wengi hatupendi kulisema. Kitendo cha kutaka wasomi wawe Wakristo tu limelichafua kanisa mpaka leo hii. ​
Hii mada yako, naona NI MATAPISHI YA PROPAGANDA in and OUT.

Umekula KITIMOTO iliyochacha???
Hii ilikuwa mwaka gani??

Hoja yako ni nini?

Tuko page ya 4?

Naona kila ukiandika ni KINYESI tupu.
Sisi kama umma tuna HOJA ZETU.

Wanachozungumza TEC ni SAUTI yetu.

Maana sisi tukisema MNATUMUDU, Ndio maana kina MDUDE, DEO SAKA, KIPANYA hawapo.

TEC wanasema kwa niaba yetu. Hizo stori zao za nyuma sisi hazituhusu.


Wenye akili timamu wana dili na SOURCE.

Hapa unachojaribu kufanya ni kutupia LAWAMA wasiohusika na kutaka ku-NORMALISE UJUHA na MAUAJI.
Walisaidiaje?
Mapadre gani walikimbilia uhamishoni??

Unatapika sana UJUHA kwenye hii mada.

Magufuli aliwekwa na Mkapa kama kijana wa Mkapa, na ushahidi uko humu, tangu mwaka 2014.

Kwamba TEC walimweka, kwahiyo TEC ni NEC ya CCM, na Halmashauri kuu ya CCM.

Kama TEC walimweka MAGUFULI, kwahiyo Samia kawekwa na BAKWATA???
Haya yote ambayo anafanya leo hii Samia kushambulia mapadri yana mlolongo mrefu (The did not just exist in a vacuum, it's a long-coordinated government policy).​
Kwahiyo kama yana mlolongo mrefu ndio yanatakiwa kuendelea???
Wayamalize vipi?

TEC walishatoa USHAURI hata kabla ya uchaguzi na baada ya mauaji wakatoa ROAD MAP.

Hawajaua mtu na hawana hatia.

Wenye hatia wawajibike. Jambo rahisi tu.

Alichokifanya Samia siku ile kilikuwa Unprecedented, lakini hata yeye ni zao la tatizo. Tatizo kubwa limejificha kwa chini ambapo hata akiondoka litaendelea kuwepo endapo hatutakubali kukaa chini na kujisahihisha. ​
Ukae chini nani na nani?
Samia kachaguliwa na nani?

Kaua watu ili amtawale nani??
Wenye matatizo zaidi ni waliozika. NGUO.

Matatizo ya MUUAJI, MFIRAJI na MTEKAJI hayawezi kunihusu.

WIZI, UPORAJI, MAUAJI, UTEKAJI ni matendo ya hiari ya KUJITAKIA.
MJADALA TIMAMU unajengwa kwenye UKWELI na USHAHIDI.

Siyo PROPAGANDA MAVI unazojaribu kutapika hapa ndani.
 
Unajichanganya sana.

Labda ulimwelewa Lissu vibaya.

Lissu alipinga utaratibu mzima kuhusu move ya Magufuli kushughulikia mikataba ya madini. Wewe ndiye mwenye shida maana ulijishughulisha na Acasia peke yake wakati Lissu aliongelea generally. Na hoja ya Lissu imekuja kudhihirisha kuwa alikuwa sahihi.

Kuhusu Acasia je tulilipwa hizo trillion tulizosema tunawadai? Tumelipwa kiasi gani na lini?

Kuhusu leseni zingine za madini tulizofuta vipi? Tuliposhtakiwa tumeshinda kesi? Hujui vyote vilifanywa kipindi kimoja? Hujui tumelipa kiasi gani pesa za walipakodi?

Kwa nini unauliza kama TEC wanampinga Samia kwa dini yake wakati unawatuhumu kwa udini?

Kama unasema waliwapinga marais wakristo na wakatoliki kwa nini unawatuhumu kwa udini?
 
Comprehension ndio shida kwenye huu uzi. Sababu kubwa, ni mleta mada kugusa ukatoliki na kama unavyojua watanzania wenzangu, ukigusa dini hakuna utakachosema waelewe.

Nilivyoelewa mimi, msingi wa hii mada sio madhaifu ya kanisa Katoliki, bali ni msimamo wa yale yanayopiganiwa na kanisa Katoliki. Madhaifu aliyoyataja mleta mada, ilikua ni kuonyesha tu kwamba hawako perfect, kuna sehemu waliwahi kukosea.

Swali la msingi ni je, hawapaswi kusimamia haki sasa kwakua tu waliwahi kukosea kabla? Hawapaswi kumkosoa Samia sasa hivi kwa sababu waliwahi kuhusika kwenye mauaji Rwanda? Watakiwi kupinga mauaji na utekaji sasa hivi kwakua waliwahi kutoa elimu kwa upendeleo kupitia mashule yao?

Nadhani hapo ndipo wengi mnachanganya. Na mleta mada ameenda mbali hadi kuwaonyesha kua TEC waliwahi kuwapinga hata Magufuli na Nyerere ambao walikua wakatoliki wenzao.

Kuna alarm kubwa kwenye ujumbe wa mleta mada, usipotuliza kichwa hauwezi kuiona!
 
Umempa makavu ya kutosha hadi nimemuonea huruma.

Eti anawasifia TISS? TISS hii iliyojaa washenzi ngumbaru wa ccm?

TISS hii inayovuliwa nguo na Kagame kila siku hadi JWTZ sasahivi ni jeshi kituko na Tanzania imeishia kuwa rafiki wa kudumu wa Zimbabwe, Burundi na Somalia?

Eti hiyo ndo TISS anayoisifia. Hii iliyoingiza mercenaries kuuwa Watanganyika ili Samia abaki madarakani?

Tiss hii ambayo nchi imekuwa ya hovyo na Wanasiasa kugeuka miungu watu na wanajinufaisha kwa maliasili za Taifa alafu eti anawasifia humu.

TISS iliondoka na Mkapa. Mabaki ya mkapa yakaishia na awamu ya kwanza ya kikwete. Sasahivi hatuna TISS bali tuna jumuiya ya usalama ya CCM iliyojaa vilaza na wapumbavu tu.
 
Unazunguka zunguka tu.

Kama TEC walimkosoa na kumpinga hadi Magufuli udini wao upo wapi?

Umewatuhumu TEC kwa udini ndo tunakuuliza hapa kama walimpinga na kumkosoa hadi Mkatoliki mwenzao udini wao upo wapi?

Kubali tu umekosea kuwapa TEC tuhuma za hovyo.
 
HAPANA, kiutawala na kisheria hili halipo sawa.

Kwenye jinai kuna dhana tunaiita The Concept of Immutability au The Concept of Imputability ambapo vitendo vya WAKALA (AGENT) huhesabiwa kuwa ni vitendo vya MKUBWA (STATE or SUPERIOR) endapo atatumia rasilimali za MKUBWA kufanikisha jambo lake bila MKUBWA kumuwajibisha.

Lakini pia kwenye sheria ya madai kuna dhana inaitwa VICCARIOUS LIABILTY ambapo WAKALA (AGENT) anahesabiwa kuwakilisha matendo ya MKUBWA (SUPERIOR). Leo hii kampuni ni taasisi, lakini makosa ya Mkurugenzi yanaweza kuliponza kampuni zima. AU Mfano mwingine wa kawaida. Unafuga wanyama wako, na wakaingia kwenye shamba langu kuharibu mazao. Nani anawajibika hapa: MNYAMA au MMILIKI WA WANYAMA

============================================================
Kama unachokisema kingekuwa na ukweli wowote, basi kusingekuwa na haja ya KANISA kuomba msamaha kwa MAUAJI YA KIMBARI kule nchini RWANDA kwasababu yalifanywa na viongozi wa kanisa binafsi, tena WAHUTU. Kama unakumbuka mwaka 1988, Majasusi wa Libya walishawahi kutumia silaha kulipua ndege (The Lockerbie Incident) na Kanali Gaddafi akasema kwamba yeye hakuhusika.

Ila ukweli ni kwamba, wale MAJASUSI walitumia rasilimali za serikali na nafasi zao kuweza kufanikisha ule ufedhuli. Serikali ilitakiwa iwawajibishe kuonesha haiungi mkono yale mambo.
====================================================================
Binafsi ningekuwa na uwezo ningezuia kabisa viongozi wa dini wasifanya kabisa siasa za moja kwa moja. Nimekuwa nikiyasema haya kwa zaidi ya miaka 10 sasa. Hata ule utaratibu wa kupokezana MKATOLIKI na MUISLAMU kwenye nafasi ya URAISI umesaidia nchi kutulia lakini pia umechangia sisi kufika hapa tulipo leo.

WAISLAMU na WAKATOLIKI huamini kwamba wao ni lazima watoe RAISI. Marehemu Mzee Lowassa aliwahi kwenda kanisani na kusema kipindi hiki ni zamu yetu WALUTHERI kutawala nchi. All hell broke lose. Kesho yake yaliyolewa matamko mazito kutoka kwa maaskofu, makada wa CCM na watu wengine wengi wasiompenda, kwamba anataka kuleta udini. Mimi binafsi nilighafirika sanaaaa.

Ila leo hii nikiangalia ukweli, Mzee Lowassa hakusema jambo ambalo CATHOLICS and MUSLIMS hawajawahi kusema hadharani. Kila DINI huunga mkono mgombea wao, na huu ndiyo ukweli mchungu kwa Tanzania. Tutapinga hapa ila ndani ya mioyo yetu tunafahamu ukweli.
======================================================
​
 
NDIO MAANA, nikikuita JUHA unaona tunapinga mjadala wako.

Kwahiyo unategemea Kanisa katoliki watu wote, wawe na sauti sawa?

Kwahiyo Pengo ndio msemaji wa mwisho wa kanisa katoliki?

Kwahiyo PENGO ndio alizima DOLA ZIMA na BUNGE la CCM la watu 600 kutopata katiba mpya????
Kwahiyo DOLA ZIMA limekufa.

Hata kukamata wala rushwa limeshindwa.

Sasa mbona RUGEMARILA DOLA zimeshindwa kumtia HATIANI???

Halafu ESCROW ni moja ya MJADALA wa KIPUMBAVU kuwahi kutojea TZ.


RUGEMARILA alikuwa na HISA zake zilipouzwa akapewa MGAWO wake, na akaanza kugawia watu.

Waliogawiwa wana kosa gani?

Halafu tunawajua waliopeana kupitia MKOMBOZI BANK,

Mbona mpaka leo waliopeana kupitia STANBIC BANK ,HAWASEMWI???
KESI ZA UTAPELI mifumo yetu ya kisheria inasemaje?

Au haipo????

Sheikh Zuberi ana tofauti gani na CCM na Magufuli??

Ni sauti ya nani??


Anaishi kwa UFISADI WA CCM?

Kipi hajafanya??
 
Hiyo focus ya Uislamu na Ukristo yote ni ujinga mtupu.

Na hizo divisions za kijinga za Uislamu na Ukristo ndizo zinawafanya mzidi kuwa masikini.

Dini zote hizi zimewapandikizia ujinga tu.
 
Malofa
 
Dah! Mkuu hili swala la kuwateka na kuwafira raia wao limekaa vibaya sana. Jamaa wanaroho mbaya mno.
Samia anateka, anaua watu, vikosi vyake vinafira na kubaka watu ili kuwakomoa alafu eti asisemwe na asikosolewe?

Haya yote yanafanyika alafu kuna wajinga wanajiita TISS na JWTZ. Sasa hao TISS na JWTZ wanafaida gani kama wananchi ambao ndio msingi wa maendeleo ya Taifa wanafanyiwa hayo?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…