Sidhani kama watoto wa MO au Bakhresa wanajuta kuzaliwa kwenye familia zao 🤔

Sidhani kama watoto wa MO au Bakhresa wanajuta kuzaliwa kwenye familia zao 🤔

Bro uhuru wa nn we kama mtu ana uhakika wa kulambishwa asali mkuuu privacy its not an issue

Watoto wana njia nyingi za kutoboa maisha sisi wengine ni kituko tu hatujui hata kesho yetu ipoje tunasoma na kufaulu koneksheni hamna bora hata babaangu angetumia kondom tu ningeshatupwa huko kwenye dustbin

Daah acha tu aseee umasikni ni mbaya sana [emoji29]
Usiseme hivyo mwanangu! Unataka kuniliza sasa.
 
Steve Jobs, founder of Apple alisema at his expensive death bed, pesa zake zilishindwa kumuondolea maumivu, achilia mbali kifo kilichokua dhahiri na shahiri.
Duuh ni kweli mkuuu lkn kuna matajiri wana kula bata aseeee we acha tu 😔😔

Anyway na mimi muda wangu utafika acha nipambane na masomo tu 😁😁😁
 
Well said kabisa...kwenye swala la kuwa na mtoto halafu anpitie hustle kama zako ulizopitia hicho kitu sitokuja kufanya...ni bora nisiwe tu na hao watoto...nitakuwa ni failure kabisa...

Mimi sitaki kuwa tajiri, ila nataka nifikie kiwango ambacho chochote ninacho kitaka nakipata kwa wakati.
 
Ndio maana nasema humu kwenye mitandao ukiona Mtu ana matusi sanaa ujue anaishi maisha ya kipweke na hayupo happy na maisha yake,
Watu wamekua wakitumia mitandao ya kijamii kutukana watu, kudhalilisha watu wakiamini watapunguza machungu wanayopitia kumbe ndio kwanza wanaongeza, guilty + Karma.....

Kwanini nimeanza na hayo, umekua ukinitukana sana kwenye kila comment na alhamdulillah sijawahi kukujibu sababu nilijua fika unapitia kipindi kigumu kwa hiyo unatafuta mtu wa kummwagia nyongo, mara ya mwisho ulipigwa ban kwa matusi uliyonimwagia ulivyorudi ukabadili id name....

Nikushauri tu ndugu yangu, humu kwenye mitandao ukiitumia vizuri utapata connection, utapata marafiki, utapata ndugu, haijalishi unapitia magumu kiasi gani, jaribu kua humble na ukiona kuna fursa fulani mfate mtu muulize kiungwana kwa kua file lako litasoma vizuri unajikuta unapata connection na mambo yanafunguka....

Kama unahisi unatatizo lolote la kisaikolojia, tafadhali wasiliana na mimi, naweza kukusaidia.
 
Wazazi wengi ni wabinafsi mnoo,hawawazi kuhusu kesho ya watoto wao..mzazi anaweza kuwa na kazi nzuri na yenye Maslahi makubwa.

Kitu pekee anacho waza ni kujenga na kununua gari,hapo yeye anajiona kamaliza kabisa hivyo anasubiri kustaafu.

Haandai hata mazingira ya biashara na miradi mingine,kama urithi wa watoto hapo baadae,anachojua ni kulipa ada pekee ingali anajua wazi ugumu wa ajira ulivyo kwa sasa.

Wazazi tuache Ubinafsi..tuandae future za watoto wetu hata wajukuu zetu.
 
Back
Top Bottom