Sijawahi kuona nchini yenye amani na usalama kama Zambia

Sijawahi kuona nchini yenye amani na usalama kama Zambia

Yes Zambia ni kweli kuna utulivu usion wa kawaida,nakumbuka wakati flani nikiwa na rafiki yangu tulifikia Taji Pamodzi Hotel-Lusaka.
Rafiki yangu alinnua kahaba,na usiku huo alikunywa pia pombe kupitiliza. Wakati wa kutoka asubuhi nampigia simu hapokei,kwenda chumbani na kugonga nkakuta yule dada yuko naye na mshikaji amekata moto kutokana na pombe. Dada yule alikuwa ana wasiwasi na simu ya mshikaji kaishikilia mkononi,kumbe aliogopa kupokea.
Kilichonishangaza jamaa alikuwa ameweka Dola elfu Saba mezani na yule dada hakuwa na tamaa ya kumuibia na kukimbia.
Najiulizaga tu mpka Leo,ingalikuwa hapa kwetu ingekuwaje?
Ingekuwa hapa kwetu dem angelamba simu, hela, viatu, wallet na mpaka suruali. Yani ungemkuta jamaa yako yupo uchi chumbani.
 
kipindi naishi mpanda katavi niliwahi kukutana na wazambia walionekana kuwa ni watu wenye roho ngumu na mbaya...niliamini kuwa wazambia ni watu wenye roho mbaya........
Wazambia kwa sasa ni mchanganyiko wa watu kutoka mataifa mbali mbali. Kuna wanyarwanda, warundi, wakongo, wamalawi wazimbabwe nk ambao wamechukua uraia wa Zambia. Kwahiyo ukikutana labda na mnyarwanda ambae anatumia identity ya Zambia akakufanyia ushenzi, wewe utahisi kuwa wazambia wote wapo hivyo, kumbe..
 
Hao wanaofanya business za hela NI wakinga , na ndiyo walioko hata Zambia , je unaweza iba hela ya mkinga ukaishi? Kwa hiyo usalama WA eneo haupimwi Kwa vitu hivyo peke yake, maana hata pale Tunduma border hela ziko nje nje tena zinawekwa chini kwenye box kama karanga nenda kaibe uone.
Mkuu Tunduma bora upewe chenji na mzambia, ila akikupa mbongo kama haujui thamani na hauko makini lazima atakupiga tu.
 
Long time enzi hizo wadogo ila tuna hustle kimtindo...kuna msomali mmoja alikuwa anakaa kupitia kino mvungi hospital alikuwa na bakery pale..tulikuwa tunapiga videiwaka tunapata pocket money
Nakumbuka yule mzee wao pale alikuwaga kwenye serikali hko Somalia ila alihamia tz.
Hela zetu tulikuwa tunawachiaga watuweke,kuna bibi mmja wa kisomali alikuwa anatuwekea kama anatusevia
Ilikuwa siku akitupa ilikuwa sherehee kwetu
Asili ya dhuluma hawana,ila sisi sasa
Utanfanyisha kazi hela humpi, mikwala mingi yaani matatizo tu juu ya matatizo
Nlijifunza mambo mengi sana kwao

Uaminifu kwa sisi sifuri kabisa

Ova

Halafu kama una exposure na hao watu huwezi kua kibaka kibaka wa pesa za watu, kudumu na kuendelea kwenye biashara ni pamoja na kua straight. Udokozi na udhulumati lazima utakumbana na makubwa kwenye biashara yako
 
Uchumi wa Zambia ni mdogo sana kulinganisha NA Tanzania ila wazambia wengi wao ni waaminifu sana.
Vyumba na vyumba vya kupanga tanzania hasa dar ndiyo sababu ya mambo kuwa mabovu serikali itunge sheria ya upangaji yenye kuzingatia usalama ...unakuta vijana wanachukua kigeto wanafanya uovu tu bangi madawa ya kulevya nk ...watu wanatoka nchi jirani bila vibali wanakuja dar wanapangisha makazi ..hii ndiyo sababu kubwa
 
Kwa kweli hizo cases sizijui sababu si dereva. Pengine tufumbue macho zaidi tuone shida iko wapi? Maana isjie ikawa madereva wetu wanapeleka mambo ya " kitanzania" huko.
Kweli kuna clip niliona anapigwa dereva wa roli ila ukijiuliza mtu ataanzaje kukupiga bila kosa
 
Dah ndugu unayoongea yana ukweli mtupu. Bila uaminifu lazima maisha yaje yakupige chenga, maana hata ukibahatika kupata matumizi yako yatakuwa ya hovyo hovyo kama akili yako. Ila ukiwa mwaminifu basi na maisha yatakuwa mazuri kwa kuridhika na kile kidogo au kikubwa unachokipata.

Mimi naamini sana kwenye uaminifu kwa sababu nimeendelea kwa uaminifu wa hali ya juu
Siwezi kutapeli wala kudanganya hata siku moja
Na mambo yanaenda vizuri tu
Uaminifu unaamini wa kwa mengi sana iwe serikalini au mitaani au kwenye familia

Kuna watu wametajirika kwa uaminifu tena wengi sana nawajua
Halafu masikini wa akili na mali anakuambia eti huo ni utajiri wa ndagu

Sasa yeye Kwanini asitafute hiyo ndagu?
 
Back
Top Bottom