Siku Rais Samia akigundua wanawake ndio wanaompinga zaidi, atawapigia magoti wanaume

Kama bado ana portion ya fikra yakinifu anatakiwa mambo ya kijinsia kuwaachia mazuzu wa mitandaoni.

Kama rais kujikita kwenye mambo hayo ni fedheha kwa taasisi ya urais
Ni hulka ya mtu asiyejiamini ndio maana anaamini katika kubadili badili watu na kuweka wake. Mbona kina condoleza rice, theresa may, madeline albright walishika nafasi kubwa za juu na walikuwa wakisimama kuongea wanaongea kama viongozi wa nchi hawaongei kama wanawake.
 
Hajatambua nafasi ya urais. Yawezekana keshaupenda urais ili unakuwa mzito kwake.

Sasa ni bora angekuwa na wanaume walau tuna huruma kwa mwanamke na pengine tungempa sympathy votes kuliko wanawake ambao wanataka kuona matokeo na hawatoi sympathy votes kwa mwanamke. Njia ya kuwashawishi ni kuwaletea maendeleo. Nyimbo za usawa wa jinsia hawazielewi.

Unamuimbia usawa wa kijinsia mtu ambaye kashindwa kufungua saluni kutwa nzima kwa kukosa umeme, mtu kashindwa kuuza maji na juisi kwa kukosa umeme, mtoto wake karudishwa nyumbani kwa kukosa mchango.
Sio rahisi kukuelewa. Labda hiyo nyimbo aimbe na kina mama queen mlozi au ummy mwalimu.
 
Asimame kwenye haki na Mungu atambariki. Nje ya hapo, Mungu huwa hakawii kudhihirisha ukuu wake!
 
Je unaweza ukaja na data kusupport your urgument kuwa wanawake wengi wamemchoka Rais. What you have said is what we call sweeping statement kujaribu kutoa hoja mfu.
Udibidhe wewe uliza wanawake wakioko jirani t'yaki utapata majibu mwenyewe
 
Hapo kwenye kuchangia mbegu ndo kaniacha hoi, yaani wanaume wanavyo menyeka kwa ajili ya ku maintain familia kumbe wanaishia kutambulika kama wachangia mbegu tu.......kweli akutukanae hakuchagulii tusi.
Yaani mama anapiga hadi anamkufuru Mungu. Mwenyezi Mungu mwenyewe anatambua baba ndio kichwa cha familia.

Hii njia anayotumia mama kutafuta urais inabidi ashauriwe. Ye anasahau kuwa yeye ni zao la usawa wa kijinsia. Yaani utadhani kaupata urais kwa kupambana kwa nguvu zake mwenyewe. She is planting the seeds of her own destruction. Wanaume wameanza kumchoka na wanawake hawatopiga kura za jinsia.
 
Alikuwa na kazi ngumu sana ya kuitekeleza ingawa anaweza kuwa kaifanya kuwa ngumu zaidi...

Tatizo huenda hapo nyuma tuliaminishwa hadi vitu ambavyo havipo kwamba vipo (propaganda) kwahio tukirudi kwenye uhalisia mtu anayefuata kazi yake inakuwa impossible..
 
Labda lengo lake ni kutaka kukumbukwa kama Rais aliyepigania usawa wa wanawake ingawa anatumia njia mbaya ambayo inalijeruhi kundi lingine ambalo kundi hilo lina ushawishi kwa kundi analolipigania hapo ndiyo shida ilipo na hatafanikiwa

Kwa bahati aliyoipata ndiyo ilikuwa njia nzuri kuonyesha kuwa wanawake pia wanaweza kwenye hiyo nafasi ila bahati mbaya ameonyesha hawawezi na ikitokea 2025 akaondoka itachukua miongo kadhaa kwa jinsi yake kuchukua hatamu labda itokee bahati kama aliyoipata ila siyo kura
 
Pengine ana vita nafsi na wanaume.
Sasa hii inamdrain sana.
Kwann lazima Awaattack ?
Kwann lazima ahakikishe wamekuwa belittled?
Kwann lazima awatandike za uso kuwa mimi ni mwanamke na ni Rais..

Najikuta najiuliza maswali mengi sana.
Nani alikuwa anamdunisha kwa UANAMKE wake kiasi anataka KULIPA kisasi?
Ah sijui tu but mi imeshanichosha sana.
 
I for one sitapiga kura kwake au kwa yeyote kwa vigezo vya jinsia zao.
Kama anaamini hii ni turufu, ajipange upya.
 
Kama bado ana portion ya fikra yakinifu anatakiwa mambo ya kijinsia kuwaachia mazuzu wa mitandaoni.

Kama rais kujikita kwenye mambo hayo ni fedheha kwa taasisi ya urais
Mimi ninachokiona kuhusu Raisi wetu,kuna kikundi na si wanaume wote kama watu wanavyomchukulia,kilimpa shida au kinaendelea kumshutumu juu ya uongozi wake kama mwanamke,ndio maana kila mara amekuwa akionesha kuwa mwanamke ni mtu anayeweza.Kwa level yake usitegemee atamtaja au kuwataja kuwa wakina flani wanaongea kuhusu mimi kuwa raisi kama mwanamke,na lengo la kurudia hilo ni kuondoa hiyo notion kwenye jamii ambayo tokea ipate uhuru Raisi amekuwa ni mwanaume,otherwise mimi sioni shida sana,with time watu watamkubali na maisha yatasonga.....
 
Hivi anaelewa hutuba zake zinasikilizwa na kila lika watoto na wazee kwa nini anataja maumbile
I for one sitapiga kura kwake au kwa yeyote kwa vigezo vya jinsia zao.
Kama anaamini hii ni turufu, ajipange upya.
Kifupi hutuba yake ya mbegu inatia aibu kuisikiliza
 
Mimi ninachokiona kuhusu Raisi wetu,kuna kikundi na si wanaume wote kama watu wanavyomchukulia,kilimpa shida au kinaendelea kumshutumu juu ya uongozi wake kama mwanamke,ndio maana kila mara amekuwa akionesha kuwa mwanamke ni mtu anayeweza...
Awaprove wrong and awawajibishe kwa Mamlaka aliyonayo.
PERIOD!!
Kulalamika now and then inampa tu wakati mgumu zaidi.
Wenzie hatuwaoni,hatuwasikii wanayofanya.

Kwann anakubali kuwa intimidated?
 
Ona sasa!
Yani anakosa namna nyingine ya kuaddress Taifa zaidi ya hoja za Jinsi na jinsia?
Image umekaa na watoto unaangalia taarifa ya habari ya Mama ana anza kuhutubia mbegu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…