Wanadamu sisi wa ajabu sanaaaa. JPM tuliona hafai, tena wako mlioshukuru kuondoka kwake na leo tunasema samia nae hafai[emoji848]
Kwanini kumlinganisha Rais Samia Suluhu Hassan na John Pombe Joseph Magufuli?
Nyerere alilaumiwa kisha Mwinyi akaonekana afadhali, baadae Mwinyi akaumiwa sana Mkapa akaonekana mwema ila alipoondoka ikawa bora. Kikwete akonekana bora zaidi ya mkapa ila baadae lawama zilezile..... binadamu hatuna jema
SSH ni Rais wetu na hilo hatuwezi badilisha, tunatakiwa kumuombea na kumsaidia kutekeleza mipango sio kumsemea mabaya kila siku na kumlaumu
Tumwache JPM apumzike kwa amani na tumwombee Rais SSH na wasaidizi wake waendeleze yale aliyotuachia. Yote yametokea ndani ya mipango ya Mungu