Southern Highland
JF-Expert Member
- Mar 22, 2017
- 16,074
- 27,490
Janshalewa keshalewa anatepeta tu leo
Insha-Allah...Half Time:
Simba 2 : 1 Berkane
Full Time:
Simba 4: 1 Berkane
Relax!Hii ni kama siyo sisi. Vizee vyetu ni vifupi. Halafu font-type ya m-bet siyo ya kwetu, ni ya uto
UtopwixNi kufa au kupona.
Ni fainali ya mkondo wa pili katika kombe la shirikisho barani Afrika.
Simba SC Vs RS Berkane, mchezo wa kwanza Simba alifungwa 2-0.
Leo atakuwa na nafasi ya kujiuliza katika mchezo wa mkondo wa pili.
Huku Mpanzu, kule Kibu D, pale Jean Charles Ahoua. RS Berkane wajishikilie show itakuwa nzito.
Mwana Simba uliopo Nakuru, Mbarara, Ndola, Bukavu, Mpanda, na kwingineko tembea kifua mbele, hii tunabeba.
Live updates zitakujia hapa katika uzi huu, mchezo utakuwa mubashara Azam Sports 1HD, Super Sports 227HD, Bein Sports pamoja na Canal Sports.
Mchezo no saa 10:00 jioni kwa masaa ya Afrika Mashariki.
Kila la heri kwa wawakilishi wa Tanzania katika mchezo wa Fainali.
Simba Nguvu Moja!!
ha ha ha
Nyuzi nzuri kama huu zimeunganishwa na Uzi wa hovyo kuwahi kutokea Kisa jamaa amewahi inadikitisha kwa kweli hakuna hata update yeyote mpaka muda huu PawLeo ndiyo siku iliyosubiriwa na wanamichezo wote barani Africa na duniani kote kwa ujumla,ni siku ya mchezo wa Fainal ya Kombe la Shirikisho barani Afrika ambapo Simba SC ya Tanzania inawakaribisha RS Berkane ya nchini Morocco katika fainal ya mkondo wa pili mara baada ya ile za mkondo wa kwanza kumalizika kwa wenyeji Berkane kuibuka na ushindi mnono wa mabao mawili kwa bila. Uwanja utakuwa ni wa New Amaan Complex visiwani Z`bar muda wa saa 10kamili kwa saa za Africa Mashariki.
Je mnyama Simba atafanikiwa kupindua meza na kubeba kombe hili la pili kwa ukubwa barani Africa,au RS berkane watalinda ushindi wao na kutwaa kombe hili mara ya tatu?
Macho na masikio yote tuyaelekeze visiwani Zanzibar kushuhudia mtanange huu mkali na wa kukata na shoka
Kwa ambao hawatapata nafasi ya kwenda Z`bar au kuutazama mchezo huu ktk tv au kuusikiliza kwa njia ya radio basi muambatane nami kuwaletea updaes za mchezo huu.
Karibuni