Siri ambayo waombaji wengi wa Kikristo hawajaijua. Chukua hii uone matokeo katika maombi yako

Ndugu sitamgazi biashara, kama jambo hauko interest pita kimyakimya.
Unaweza kujiona una hekima kumbe uangamivu uko mlangoni kwako.
Sasa umekuja kifundisha nini kama unaanza kuwa mkali.... Nieleweshe Mtumishi zile Lugha zinatokeaga wapi? Na zina maana gan
 
Msingi wetu hauko katika filamu ya Yesu. Ile ni ya waigizaji tu waliigiza kama njia ya kutafuta pesa.
Soma Maandiko hayo ndipo tulikotoa kunena kwa lugha.
Ni maagizo ya Yesu mwenyewe.
Maagizo ya YESU?
Naomba Andiko mtumishi nijifunze hilo.... Yesu kawaambia wanafunzi wake wanene kwa Lugja
 
Nitoe siri iliyo kuu kuliko zote, mara muombapo msiropokeropoke,
Siri ya pili, kuomba katika lugha sahihi, binafsi natumia lugha halisi, ya zama hizo, lugha yake yeye, lugha aliyoiongea yeye, huu ni mfano wa Sala ya BABA YETU,
""ABBA NAWASHABAH SHAMAYIIM QADASH HAYAH SHAM KA AHAYAH MALAK NAWASHABAH SHAMAYIIM...... ""
Aramaic the language of heavenly!
 
mtumishi
-Kama ataweza kuomba masaa 2 katika roho non stop mtu huyo ataweza kuuvuta muujiza wowote mbele yake?

Mawazo yangu chariti
kuomba katika roho kwa masaa mawili mfululizo hakuna mahusiano na matokea
kinacholeta matokeo
maombi+hazina yako+imani+fuata hatua zote za maombi ikiwepo na toba=na muujiza lakini sio muujiza wowote itategemea sana hazina yako mbinguni

mtumishi
-Uhai wa Mkristo uko katika maombi, mkristo ambaye haombi huyo ni mkavu, aidha amekufa kiroho au anakaribia kufa kiroho?

Mawazo yangu chariti
tunafahamu maombi ni upanga wa roho yaani silaha lakini imani ndio ngao au kinga uhai wa mkristo unashikiliwa na maombi? mbona yesu aliomba lakini walimsulibisha uhai wa mkristo ni imani buana mtumishi yesu imani ndio ilikua uhai wake alikua anaimani atatoboa hata nini kimkute

mtumishi
-Kuomba katika roho kwa mujibu wa Mtume Paul ni kuomba katika lugha ya MBINGUNI (lugha za malaika, lugha za Kimungu) , lugha ambazo wakuu wa anga kama waliomzuia Gabriel kumpa majibu Nabii Daniel hawazijui

Mawazo yangu chariti
mtumishi hujamwelewa vizuri mtume paulo
kuomba katika roho lengo ni kumpiga chenga shetani kwa namna yoyote sio kumficha lugha tu, hata kuomba mbele yake mara nyingi ni kosa imeandikwa sehemu nyingi kwenye biblia kwanini yesu alikua anajitenga peke yake kwenda kuomba, ukienda mbali linakuja swala la kufunga ile unajitenga na watu kweli kweli, hufungi kijanja janja kama kanisa la leo na dini nyingine wafanyavyo ili kuwafurahisha walimwengu

nadhani sijakukwaza mtumishi.
 
Yes alikuwaga na ROHO MAKATIFU Ila hakuwahi kuomba kwa KUNENA nyie mmeitoa wapi bhandugu?

Au ndio mashetani ya kigalatia yanapandishwa hivyo

Nauliza tu
Siku ya pentekoste mitume alinena kwa lugha gan? Walizitoa wapi hizo lugha?
 
Dini ya kweli ni upendo. Na kushika amri zake Mwenyezi Mungu mpende Mungu wako kwa moyo wako na akili zako zote.
Mpende jirani yako kama unavyo jipenda.
 
Barikiwa sana
 
Dini ya kweli ni upendo. Na kushika amri zake Mwenyezi Mungu mpende Mungu wako kwa moyo wako na akili zako zote.
Mpende jirani yako kama unavyo jipenda.
Na mtu wa tatu tuliyeagizwa tuwapende ni adui zetu
 
Msingi wetu hauko katika filamu ya Yesu. Ile ni ya waigizaji tu waliigiza kama njia ya kutafuta pesa.
Soma Maandiko hayo ndipo tulikotoa kunena kwa lugha.
Ni maagizo ya Yesu mwenyewe.
Waigizaji wa filamu ya Yesu walifanikiwa vitu viwili Vikuu.KUPOTOSHA kwamba Yesu alifanana na yule wa igizo pia WALIPIGA hela nyingi sana kutokana na mauzo ya filamu.
 
Huu mstari huwa unauchukuliaje ndugu? Marko 16:17 imeandikwa, Na ishara hizi zitafuatana na hao waaminio, kwa Jina langu watatoa pepo, watasema kwa lugha mpya
Basi Mkuu tusije leta pengine ubishani kwenye neno la Mungu. Sote ni wa Mungu. Asante kwa neno
 
Basi Mkuu tusije leta pengine ubishani kwenye neno la Mungu. Sote ni wa Mungu. Asante kwa neno
sote sio wa Mungu, kuna uwezekano mkubwa wewe sio wa Mungu ndio maana huutaki huu mstari. hutaki kujazwa Roho Mtakatifu, unaamini ni kipawa wanapewa wachache tu wakati mstari huo Yesu anasema ni ahadi kwa kila atakayemwamini, wote watapewa. hata wale wa siku ya pentecost walijazwa WOTE, Roho hakumwagwa kwa wachache tu kwamba ni karama NO, wote walijazwa Roho Mtakatifu na wote walisema kwa lugha mpya. nakushauri tafuta hiki kipawa. Petro alipoulizwa tufanyeje aliwaambia tubuni mkabatizwe kila mmoja kwa Jina lake Yesu mpate uondoleo la dhambi nanyi mtapata kipawa cha Roho Mtakatifu.meaning, unatakiwa kuokoka, hapo ulipo hujaokoka ndio maana huyajui haya, uondolewe dhambi zako nawe utapata hiki kipawa, ni ahadi yako, ni haki yako ukija kuokoka. USIPOKUWA NA ROHO MTAKATIFU WEWE SIO WA MUNGU.

WARUMI 8: 12 INASEMA, Lakini ikiwa Roho wa Mungu anakaa ndani yenu, ninyi hamwufuati mwili; bali mwaifuata roho. Lakini mtu awaye yote asipokuwa na Roho wa Kristo, huyo si wake. 10 Na Kristo akiwa ndani yenu, mwili wenu umekufa kwa sababu ya dhambi; bali roho yenu i hai, kwa sababu ya haki. 11 Lakini, ikiwa Roho yake yeye aliyemfufua Yesu katika wafu anakaa ndani yenu, yeye aliyemfufua Kristo Yesu katika wafu ataihuisha na miili yenu iliyo katika hali ya kufa, kwa Roho wake anayekaa ndani yenu.

kwahiyo wengi wanaabudu dini na mapokeo ya dini, wanakataa kipawa cha Roho Mtakatifu ambaye Yesu alisema bila huyo hamwezi kufanya neno lolote. angelikuwa anamaanisha ni kitu ambacho mmoja anaweza kupokea na mwingine hawezi, asingeongea akimmaanisha mmoja mmoja namna hii. kwanza alisema atakayemwamini atampokea ni ahadi yake, pili alisema bila huyo ninyi mnayemwamini hamuwezi kufanya neno lolote. na hapo warumi inaonyesha wazi, usipokuwa naye, manake kama hujajazwa, wewe sio wake, na kunena ni ishara ya kujazwa.
 
Hiki unachoeleza na mafungu uliyotumia haviendani kabisa. Mafungu yanasema uombe kwa roho na ufahamu(akili)[understanding] wewe unaongea kuhusu eti mashetani hayajui lugha.

Jambo lingine ambalo hujui techniques hizo ambayo Christian science inafundisha ni Visualization kitu ambacho si kweli bali kuongizwa na spirit guide usiyemjua ambaye hutamka maneno ambayo hata wee unayeomba hujui.
Mwisho ni uelewa kuwa Maombi hayamtawali Mungu bali Yeye hujibu kwa kanuni moja kuu nayo ANAKUPENDA na KUKUJALI hivyo maombi yako yatajibiwa kulingana na hayo.
 
unaelewa nini maana ya "kuomba kwa roho" na unaelewa nini maana ya "kuomba kwa akili". labda tuanzie hapo.
 
Nenda mstari wa 8

8 Imekuwaje basi sisi kusikia kila mtu lugha yetu tuliyozaliwa nayo?
Matendo ya Mitume 2:8

Lengo la kunena kwa lugha nyingine ni kupeleka ujumbe kwa watu wasio wa lugha yako ambao wanatakiwa waupate
KWa akili zako timamu unadhani ile filamu ni uhalisia wa Yesu?
Fuata biblia ilisema nini na sio filam
 
Nenda mstari wa 8

8 Imekuwaje basi sisi kusikia kila mtu lugha yetu tuliyozaliwa nayo?
Matendo ya Mitume 2:8

Lengo la kunena kwa lugha nyingine ni kupeleka ujumbe kwa watu wasio wa lugha yako ambao wanatakiwa waupate
hiki mlichokaririshwa baada ya kuona mmeshindwa kumpata Roho, wapi wameandika kwenye Biblia? Roho Mtakatifu hata leo hii hunena kwako kwa lugha ile yeye atakayoiamua kutumia, iwe ya mbinguni au ya duniani, iwe ya malaika au ya kidunia.

pia, ukisoma Matendo 19:3, Paulo alifika akaona waongofu walihubiriwa na apolo, akawauliza walibatizwa kwa ubatizo gani? wakasema wa Yohana, akawauliza kama walijazwa Roho, wakasema hawajawahi hata kumsikia, akawabatiza kwa Ubatizo wa Yesu, na akaweka mikono juu yao, wakajazwa Roho wakaanza kunena kwa lugha. hapo walikuwa wanamtafsiria nani kwa akili yako?

pia, huwa mnahalalisha kutokunena, kwasababu paulo alisema awepo mtafsiri. hamjui mazingira yepi aliongelea hilo. ni kwamba, palikuwepo waongofu wapya ambao walifurahia mno kipawa hiki, wakawa wakikutana ibadani wananena tu hawahubiri Neno, ndio paulo akawa anawafundisha kwamba msinene muda wote, awepo mtafsiri pia kwa wengine waliowatembelea hapo. hakumaanisha kwamba msinene.

siri ipo hapa, kwamba, tunaposema mnene kwa lugha, hatumaanishi muda wooote muwe mnanena tu msiombe hata kwa maneno ya akili,ndio maana Paulo alisema nitaomba kwa roho na nitaomba kwa akili pia, akimaanisha, nitanena kwa lugha na nitaomba kwa akili/maneno ya kawaida pia. AJABU YAKE NI KWAMBA, ninyi na wachungaji wenu na mapadre wenu hadi maaskofu wenu, hata walau mara moja tu kunena kwa lugha hamjawahi, mmechagua kuomba kwa akili peke yake. kwanini basi kama mmeamua kulipinga hili, msiombe walau kama Paulo? muombe kwa lugha, na muombe kwa akili pia? imekuwaje hamuwezi kuomba kwa lugha? ni kwasababu hamna Roho na mmemkataa. Paulo alisema ananena kwa lugha kuliko wote? kwanini hakuwa anaomba kwa akili peke yake? mlishawahi kutafakari hili?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…