Siri ambayo waombaji wengi wa Kikristo hawajaijua. Chukua hii uone matokeo katika maombi yako

Hujanijibu Mkuu Kunena kwa LUGHA mlitoa wapi?

Hata katika Filamu ya YESU sijaona Akisema Shakara "babababbaa la bosika la matembweleza salambaba"

Mmeitoa wapi hiyo staili?
jitahidi kusoma Biblia. Mungu akusaidie.
 
Sasa nikujibu kwa niaba ya wasomaji wengine wewe endelea kupiga hizo sabrakataaaaatattaa
Ila kuomba kwa Roho

1. Ni kuwa chini ya uwepo wa Roho Mtakatifu ni muombaji kuomba akiwa chini ya uwepo wa Mungu wa amani faraja furaha ambapo tunda la Roho ni mtawala wa tabia yake

31 Basi kanisa likapata raha katika Uyahudi wote na Galilaya na Samaria, likajengwa, likiendelea na kuongezeka katika kicho cha Bwana, na faraja ya Roho Mtakatifu.
Matendo ya Mitume 9:31

2. Ni kuomba katika Mapenzi ya Mungu ambapo muombaji haombi vyovyote bali kile ambacho Mungu ndio mapenzi yake. Nikuacga Roho aobgoze muombaji ili asiombe yasiyostahili ni kuomba kilicho sahihi kwa maisha ya muombaji

26 Kadhalika Roho naye hutusaidia udhaifu wetu, kwa maana hatujui kuomba jinsi itupasavyo, lakini Roho mwenyewe hutuombea kwa kuugua kusikoweza kutamkwa.
27 Na yeye aichunguzaye mioyo aijua nia ya Roho ilivyo, kwa kuwa huwaombea watakatifu kama apendavyo Mungu.
Warumi 8:26, 27

3. Neno la ki Greek lilotumika "katika"(kiswahili)
Ni " kumaanisha, kuongozwa, kujisalimisha.
Hivyo kuomba kwa Roho hakupo katika namna ya kutamka maneno bali kuwa chini na uongozi wa Roho au Roho anavyomaanisha
Tumia muda mwingi kusoma neno na si hisia. Hizo cheketu chekuttu na maneno yasiyo na maana hata wapunga pepo na waganga wanatamka hizo lugha.

Nimejibu kwa Upendo sitaki ushindi
 
ULIVYOJIBU, unaonyesha wewe ni msomi mzuri wa theolojia, ila theolojia iliyokita mizizi yake kwenye mapokeo ya dini yako, sio Neno la Mungu linavyomaanisha, na hamtataka kuelewa vingine vyovyote kama vinapinga mapokeo ya dini yenu nzuri. ni huzuni kubwa sana kwamba watu huwa wanasoma theolojia kwa miaka mingi, ila hawajamjua Mungu na wataenda motoni kwa kumkosa Mungu.

kwa kukusaidia, KUOMBA KWA ROHO ni kunena kwa lugha, ni pale unapojazwa Roho Mtakatifu akatumia kinywa chako kikinena/kikiomba kwa lugha nyingine kadiri Roho alivyoamua na akili yako inakuwa haina matunda/haihusiki. Roho Mtakatifu anakuwa ame-take over na kutumia kinywa chako kunena katika maombi. hivyo ndivyo ilivyokuwa wakati ule wa Pentecost, na maeneo yote wanafunzi wa Yesu walipopita kuhubiri waliwekea watu mikono ili wapate kipawa hiki.

Yesu alisema, Na ishara hizi zitaambatana na wote waaminio, kwa Jina langu watatoa pepo, wataweka mikono yao juu ya wagonjwa nao watapata afya, watasema kwa lugha mpya (meaning watanena kwa lugha)....., hicho umeandika hapo juu hakieleweki kabisa, digrii zako ulipoteza miaka yote bure kabisa. ungejua ungebaki tu nyumbani na kama hiki ndicho mnafundisha waumini wenu, ni hasara kubwa sana.

1Korinto 14:14 inasema; Maana nikiomba kwa lugha, roho yangu huomba, lakini akili zangu hazina matunda.
MATENDO 10:44 INASEMA:
44 Petro alipokuwa akisema maneno hayo Roho Mtakatifu akawashukia wote waliolisikia lile neno. 45 Na wale waliotahiriwa, walioamini, wakashangaa, watu wote waliokuja pamoja na Petro, kwa sababu Mataifa nao wamemwagiwa kipawa cha Roho Mtakatifu. 46 Kwa maana waliwasikia wakisema kwa lugha, na kumwadhimisha Mungu.
 
Waigizaji wa filamu ya Yesu walifanikiwa vitu viwili Vikuu.KUPOTOSHA kwamba Yesu alifanana na yule wa igizo pia WALIPIGA hela nyingi sana kutokana na mauzo ya filamu.
Most of christians wanapoomba kwa jina la Yesu moyoni mwao wanamwona yule Ibilisi wa kwenye filamu.
Sasa ninaamini kuwa ule ulikuwa mpango wa Ibilisi
 
Kama unanena na akili yako haijui. Uko deceived tayari. Hizo ni roho za mashetani zifanyanyazo ishara na maajabu

14 Hizo ndizo roho za mashetani, zifanyazo ishara, zitokazo na kuwaendea wafalme wa ulimwengu wote kuwakusanya kwa vita ya siku ile kuu ya Mungu Mwenyezi.
Ufunuo wa Yohana 16:14
 
soma hapa, halafu ujitathmini. ndio maana tunasema muokoke, hamtaelewa kama akili zenu hazitakuwa zimefunguliwa.

1Korinto 14:14 inasema; Maana nikiomba kwa lugha, roho yangu huomba, lakini akili zangu hazina matunda.
 
soma hapa, halafu ujitathmini. ndio maana tunasema muokoke, hamtaelewa kama akili zenu hazitakuwa zimefunguliwa.

1Korinto 14:14 inasema; Maana nikiomba kwa lugha, roho yangu huomba, lakini akili zangu hazina matunda.
Watakisaidiawengine maan a tayari wewe uko kundi la watu wanaonena bila kitumia akili(akili hazina matunda).
Kama ndio uamuzi wako ni hiari yako ila hakuna lugha zisizo na maana.
Ungetumia kanani ya kuomba kwa roho na akili ungefaidika sana

15 Imekuwaje, basi? Nitaomba kwa roho, tena nitaomba kwa akili pia; mtaimba kwa roho, tena nitaimba kwa akili pia.
1 Wakorintho 14:15
 
Umeongea kitu kikubwa sana Wakristo wote wakiielewa hii wataenda matawi sana katika Ulimwengu wa Roho na watakua Spiritual haina mfano,
Nilianza kufanya hivi mwaka mmoja uliopita,
Ipo siku nitawaletea uzi humu kama ushuhuda niwape elimu watu juu ya Ulimwengu wa Roho unavyofanya kazi!
Ubarikiwe sana!
 
Sijaelewa kwakweli.
 
Hakuna kuomba kwa kupoteza muda, hilo siamini.

Kwa maana hiyo roho mtakatifu anaomba kwa niaba yako sio??
Na wewe huelewi kinachoombwa?


Sawa mkuu ila mimi naamini Mungu ananisikia hata nimuombe bila huko kunena.
 
Kunena kwa lugha huja automatic ukiwa ktk maombi yenye deep trust and connection, na ni raha ilioje maana ukija stop unajihisi ni mtu wa tofauti kabisa, ninakumbuka siku fulani nikiwa kijijini nilipigwa kimbola nilikuja gundua usiku nikiwa bed mwenyewe nilihisi tumboni kama kitu kinazunguka alafu mwili kama nabanwa na chatu
Nafeel kabisa na nipo macho anakuja hadi usoni nikasema asintanie

Nilichukuwa bible sio msomaji sana ila nilifungua tu accidentally ikaja zaburi fulani hivi bwana atanilinda na maadui zangu, nikasoma kwa hisia sijui mara ngapi nikajikuta nipo ktk maombi sijui nilikuwa nazungumza nini ila kimpangilio kabisa ilikuwa moja ya best experience kwangu ule usiku mi sio mlokole na wala sio mtu wa kanisani na sikuwah rudia tena maombi yale ni mwaka wa nne now itabid nimrudie Mungu
 
Hakuna kuomba kwa kupoteza muda, hilo siamini.

Kwa maana hiyo roho mtakatifu anaomba kwa niaba yako sio??
Na wewe huelewi kinachoombwa?


Sawa mkuu ila mimi naamini Mungu ananisikia hata nimuombe bila huko kunena.
Si vibaya kuomba Kwa mwili,

Changamoto yake ni kuwa adui atakuwa unachoomba na ni Rahisi kuzuia au kuchelewesha maombi yasiende au yakienda ni Rahisi kuzuia majibu kukurudia Kwa wakati.

Kuomba Kwa lugha ni Mungu anaomba kupitia kinywa chako, hakuna traffic au jam hapo.

Ukurusha kombora kupitia kuomba Kwa lugha, adui hawezi jua au kuzuia silaha hiyo maana hatojua anapigwa na nini, saa ngapi na wapi, hivyo hawezi kukwepa.

Ongeza kiu ya kufika viwango hivyo, omba tena na tena kupokea kipawa hicho, jitenge na dhambi, jitakase Kila mara. One day yes!!
 
Haya sawa.
 
Haya sawa.
Kuomba Kwa mwili kunachosha, kumaliza saa Moja ni mtihani Kweli Kweli, lakini ukiomba Kwa Roho, unaweza omba usiku kucha na kiu haikati ,huchoki kububujika katika kuomba.

Ni kama tu kusoma BIBLIA Kwa mwili, tv au gazeti waeza soma fluent bila kuchoka, ila ukisoma BIBLIA, adui atakuletea Kila aina ya USINGIZI, uchovu na vikwazo, lakini ukisoma Kwa Roho, hutachoka.

Mungu ni ROHO, nao wamwabuduo halisi imewapasankumwabudu katika Roho na Kweli.

Ndipo hapo kuomba, kusoma au kuimba au kuandika Kwa lugha umuhimu wake unapokuja.
 
Hakuna kuomba kwa kupoteza muda, hilo siamini.

Kwa maana hiyo roho mtakatifu anaomba kwa niaba yako sio??
Na wewe huelewi kinachoombwa?


Sawa mkuu ila mimi naamini Mungu ananisikia hata nimuombe bila huko kunena.
endelea, ila unatwanga maji kwenye kitu.
 
Nitaweka kwa video nikikamilisha somo la Roho Mtakatifu na karama zake .
Somo nishaliandaa kwa mtindo wa kitabu lakini nawaza nifanye video.
Lengo ni kuwafungua watu fikra si kupata pesa. Kwakweli sihitaji pesa kwa njia ya Injili
Umelaumu waombaji tuu, lakini wewe mwenyewe inaonekana huelewi kuomba ktk roho, ksb hujaeleza kuomba ktk roho unafanyaje au unaombaje.
 
Uko sahihi kabisa, Mungu anawajibu wote wanaoomba kwa lugha zao na lugha ya roho mtakatifu, wengi wanaonena kwa lugha hawaelewi wanachoomba, mi nafikiri kwa mahitaji binafsi omba kwa lugha yako huku ukijua kabisa hapa nimeomba kitu Fulani, Tena omba ktk roho Ili Roho mtf akakuchukulie mahitaji yako katka hazina ya Mungu. Asiwe conservative sana kwenye swala maombi, kama jinsi Bwana anavyojua dhambi zetu, hazuiliki kusikia maombi yetu kwa lugha yeyote hata kwa kuwaza tuu.
 
We mjomba, hakuna kiumbe chochote m inguni na duniani kinachoweza kumzuia Mungu asisikie maombi yako au kujua dhambi zako.
 
Amina mkuu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…