IJUE VOLVO XC 90
Na KIMOMWE MOTORS (T) Ltd- Waagizaji Magari
Utangulizi
Gari hii yenye inayotengenezwa nchini Sweeden, iliingia sokoni kwa mara ya kwanza mwaka 2003 ikishindanishwa na Mercedes Benz G Class, Jeep Grand Cherokee, pamoja na BMW X5
Injini na Mafuta
Petrol ina Cc 2500 ina Turbo inakadiriwa kwenda Km9/L wakati ya Cc 3000 inakadiriwa kwenda Km7/L.
Diesel ina Cc 2400 na inakadiriwa kwenda km 12 kwa lita.
Vifaa
Vifaa ni vichache kwa gharama za juu japo uzuri ni kwamba vinadumu mda mrefu. Uzuri mwingine ni kwamba gari hizi zinaongezeka kwa kasi kubwa nchini sababu watanzania wengi wamegundu hii ni moja ya gari zenye usalama mkubwa za bei ndogo hivyo vifaa vinazidi kuongezeka.
Nyongeza
Airbags 8, Ngozi, Viti 7, Option za Usukani, Fm inayofika 107 badala ya 90.
Maoni na Ushauri
Kwa sababu za usalama mfano wizi wa magari, Kukinga abiria wote walio ndani, kuepuka safari za mara kwa mara garage, hii ni gari unayoshauriwa kuiwazia kwa haraka.
Changamoto ni gharama kubwa za vifaa pindi vitakapohitajika.
Gharama
Kwa kuagiza ya Petrol inaanzia 20m wakati ya Diesel inaanzia 27.5m