IJUE MITSUBISHI DELICA D5
na KIMOMWE MOTORS (T) LTD
Utangulizi
Gari hii ya juu kiasi uzalishaji wake ulianza mwaka 2007 ukilenga kuchuana na watangulizi wake kama Toyota Noah, Nissan Serena na Mazda Biante. Hii iliboreshwa zaidi kwenye utulivu katika barabara zote za lami na vumbi huku muundo wake ukiwa kati ya SUV na matumizi mazuri ya mafuta licha ya kua na body zito.
Injini na Mafuta
Ina injini aina mbili za Petrol zote zikiwa na teknolijia ya MIVEC (Toyota wanaita- VVTi) yaani 4B11 yenye Cc 2000 ikienda mpaka km 14 kwa lita wakati 4B12 yenye Cc 2400 ikienda mpaka km 11 (injini hii ikiwa kwenye outlander yenye uzito wa tani 1.5 inaenda mpaka km 13 kwa lita- Delica ina tani 1.7).
injini zite hizo ni nzuri na ngumu haswa hiyo kubwa ya 4B12 inayopatikana katika Mitsubishi Outlander pia.
Utulivu/Uimara
Gari hii iwapo kwenye mwendo mkali, inaelezewa kua ni imara na tulivu kiasi cha kukuruhusu kumaliza speed 180 tofauti na mshindani wake Noah ambae huonekana kua mwepesi kiasi awapo katika mwendo mkali (noah zinakuja na tani 1.4 wakati Delica inakuja na tani 1.6).
Vifaa
Vifaa vya gari hii vinapatikana zaidi katika jiji la Dar huku vikiwa na bei juu kidogo kuliko washindani wake lakini vikiwa na uimara wa kudumu mda mrefu.
Nyongeza za gari hii
Gari hii inakuja na Airbag 6 zikiwemo 2 zinazokinga magoti ya dereva na abiria wa mbele, Buti lake linafunguka kwa kutumia umeme au mkono kutegemea na utakavyohitaji.
Maoni na Ushauri
Ikiwa unahitaji gari familia yenye viti 8, hii ni moja ya gari unayoweza kuifikiria kwa kua ni ya kisasa kwenye upande wa options ilizonazo kuanzia teknolojia ya injini na hata bodi lake. Muundo wake unairuhusu kupita katika njia za vumbi na lami bila kutetereka kwa kua iliundwa ikilenga kua SUV japo ni Wagon.
Gharama za Kuagiza
Kwa wastani jumla ya gharama ni kuanzia 23m. sababu kubwa ya gharama zake kua juu kuliko washindani wake ni ushuru ambao umekua mara 2 zaidi ya manunuzi ya gari hii huko nje.
Mawasiliano
Tunapatikana Dar- Magomeni Mapipa au Mbeya- Mwanjelwa...zaidi piga 0746 267740 au 0719 989 222