Special Thread: Yanayojiri Mgogoro wa Ukraine na Urusi. Nini chanzo na hatma ya mzozo?

Acha unafki basi mzee .... Ebu angalia libya yetu hapa hapa afrika wala tusiende kwingine ......je ni sawa walivofanya ..marekani na ufaransa kuipiga libya mabom tena wakaweka NO FLY ZONE ....nchi yenye uhuru wake .....asa hivi wanaiba mafuta huko beghazi ......huku wakimwaga silaha watu wauwane wao haiwasumbui .....punguza unafki kidoho mzee ......CONGO hapa jirani yetu kila kukicha tunaskia kachinjwa huyu mara hivi .., ....MSUMBIJI hapo ....kugundulika kwa gesi tu tayari wameibuka waasi kusiko julikana ....NIGERIA ...kule .kwenye mafuta .....[emoji41][emoji41][emoji41][emoji41].....wewe sio mgeni kwa wanachokifanya wamaeekani hapa dunian ..........
 
hahaha nashkuru mkuu. Japo tuko mahasimu kweny hii vita .
But Mara moja moja tunapata kanafasi kaku have a fun .
Big up .
[emoji851][emoji851][emoji851][emoji851]...
 
Vietnam Kaskazini ilishambulia Kusini ; serikali ya Kusini iliomba Marekani kuingia na kusaidia. Hali halisi mamb
Utata unaouona kwenye suala la Vietinam ndiyo huo huo tuna uona Ukraine ! Republics mbili za Donestik na Luhangski zikiwa huru ziliomba msaada wa kujilinda baada ya kushambulia kwa miaka saba kabla ya kujitenga rasmi na Ukraine magharibi. Russia kama alivyofanya US kwa Vietnam ya kusini, akasailisadia na anaendelea kusaidia republics hizi huku akitangaza kuhakikisha anatekeleza operesheni ya kuondoa unazi na nguvu ya kujeshi itakayosumbua republics hizi.

Kwa hiyo, hiyo sheria yako ipitie upya, ili uweze kushawishi baraza hili adhimu la JF linalofuatilia mjadala huu.
 
Is EU a military alliance!? Kuna kipengele cha collective defence kwenye EU!? Alafu kwanza nikuulize Turkey ipo EU!?

Demilitarization, Denazification, Protecting of Russian speaking UKr of PRL & PRD. Hizo ndio lilikuwa lengo la Urusi hapo UKR

Russia lost the war!? Which war!? Hahaha

Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
 
Wewe pro marekani .....kwa hiyo unawachukulia warusi ni mapongoyoyo zumbukuku ......yaani unarahisisha tu eti Germani turkey sijui ufaransa wataipiga russia ikikiuka mashart kirahisi rahisi tu ...
..hizi ndoto za mchana tuziachege jamani .[emoji848][emoji848][emoji848]...kwamba russian wao hawajaweka mashart yao mezani .....
 
Hapo Sasa umeeleweka.
 
Mkuu ana jenga hoja zake kiajabu kweli huyo. Unaweza kushangaa sana.
Ndio walivyo lakini.

Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
 
Umeombwa nukuu ya sheria

Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
 
km ukraine itajiunga EU basi russia atakua ameipoteza Ukraine moja kwa moja,
EU Sio NATO.
Urusi Hana shida na Eu.
Kuna Wana NATO wengine sio wa EU,mfano Ututruki.
Na kuna Wana NATO wengine sio wa EU mfano UK.
Na kuna wa EU wengine sio wa NATO mfano Finland na Sweden.
Ukiwa EU Russia Hana shida na wewe,
Yeye ana shida na NATO.
 
Asante, umeleta mfano mzuri. Bado kuna tofauti muhimu. Vietnam kaskazini ilikuwa iliingia ndani ya Kusini, kusaidia waasi Wakomunisti waliopigania dhidi ya serikali ya kusini. Hadi hapo unaweza kuilinganisha. Kwa hiyo Marekani ilituma wanajeshi wa kwanza kusini kuimarisha serikali yake (kama Warusi katika Donbass). Baadaye Marekani ilianza kutupa mabomu kaskazini na kutuma wanajeshi wengi Vietnam Kusini, lakini mapigano yalitokea katika Kusini pekee. Jeshi la Marekani halikuingia Vietnam Kaskazini.
Ila Jeshi la Urusi lilivamia moja kwa Ukraine.
 
Jamaa yangu,ni hivi EU Sio umoja wa kijeshi,
Shida hapo ni NATO.
Uingereza haimo EU lakini imo kwenye NATO.
Urusi hataki majeshi ya USA jirani kwake.
 
Sielewi mambo hayo yana uhusiano gani na yale niliyosema? Nilimjibu mtu aliyetaka kumtangaza Putin kuwa mshindi mkubwa akijibu hoja langu simwoni mshindi kweli . . .
 
Uko sawa kabisa,hao waache wajifariji TU.

Na kwa hiyo Ukraine atatimiza masharti au matakwa ya Urusi,Sio Urusi kutimiza matakwa ya Ukraine kama yapo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…