Mkuu mbona una jenga hoja za kuchekesha na kusadikika?Naomba usome nilichoandika juu kuhusu swali la mshindi. Nilimjibu mchangiaji aliyemwona Putin kama mshindi, hapa sijagusa swali la haki. Nilisema sidhani kutakuwa na mshindi kweli, nikataja vifo upande wa ukraine pia.
Nakubali Zelensky angeweza kusema waziwazi zaidi anachosema sasa, ambacho alitamka pia lakini si kwa maneno ya wazi vile.
Hata hivyo, hadi sasa naona tofauti kidogo. Nisipokosei wanajeshi wengi (sisemi wote) wa Ukraine walijitolea kutetea nchi, hawakupigania kama watu wanaolazimishwa.
Upande mwingine sina sababu ya kutia shaka taarifa zote kwamba sehemu ya askari wa Kirusi (sisemi wote) hawakuambiwa wanatumwa wapi, hawakulizwa kama wako tayari kupigania vita ya mashambulio, na walichoambiwa kuhusu serikali ya Neo-Nazi na kutetea raia Warusi wa Ukraine ilikuwa uwongo mtupu. Na udhaifu ulionekana upande wa jeshi la kirusi unalingana na idadi kubwa ya askari ambao hawakuwa na moyo wa kupigania...
Nakupa sehemu za sheria ya kimataifa zinazohusu; narejelea kesi ya kongo dhidi Uganda, kanuni zinatajwa humo ukipenda kuzisoma zinapatikana online:
Na baada ya vita tutaanza kudai vitu vyetu na vya watu wetu.Sasa bot zinahusiana nini na vita huko ndo kuchanganyikiwa sasa[emoji16][emoji16]
Nchi zaidi ya 30 zinakimbia uwanja wa vita na kuenda kukamata watu wasio husika[emoji16][emoji16][emoji16]
Nato mnatuahibisha kwa kweli
USA,UK na Turkey sio wanajumuia wa EU.Russia Lost the war, baada ya mazungumzo
Ukraine wamekubali kutokuwa na Upande na kutjiunga NATO kwa Makubaliano ya Kusaidiwa ulinzi na Mataifa ya NATO, pia Russia wamekubali Ukraine wajiunge na EU, This means ikitokea Russia anavunja Mkataba wake kwa Ukraine basi Itabidi apigane na Turkey, UK, US na Germany.
Hili ni somo kwetu ambao Marais wetu wananguvu ya kufanya hata wanayoambiwa na wenza wao
Bwana wewe si mtoto, usilete hapa hoja za kitoto. Ukitaka kushiriki hapa, jielimishe!!Mkuu mbona una jenga hoja za kuchekesha na kusadikika?
Ya kwamba wanajeshi wa Urusi hawa kuulizwa kama wako tiyari kwa mapigano?
Kwa hiyo siku hizi wanajeshi wakitaka kutumwa vitani wana ulizwa kwanza kama wako tayari au la ?mm ndo nalisika kwako leo,sasa je wakisema hawataki una ahilisha vita.
Mwana jeshi kwenda vitani huwa sio ombi huwa ni lazima kwa sababu ni jukumu lake tena la razima, na ndio maana sheria namba moja jeshini hutakiwi kihoji amri unayo pewa jukumu lako ni kutekeleza basi.
Mkuu una chuki sana na Urusi sijajua ni kwann ,lakini hatua alizo chukua Urusi zingechukuliwa na nchi yeyote ile iwapo usalama wake ungekuwa mashakani, wakiwemo hao wamagharibi unao waona watakatifu.
Katika maisha yako ukitaka kuwa salama jifunze kucheza mbali na maslahi ya wenye nguvu.
Ila sasa imejipatia. Tangu uvamizi wa kwanza wa Ukraine 2014 NATO iliamua kutuma vikosi (bado vidogo vya askari 1,000) katika nchi jirani za Urusi yaani Estonia na Latvia. kabla ya uvamizi huu havikuwepo.Urusi hataki majeshi ya USA jirani kwake.
Marekani imekuwa ikiiomba na kuibembeleza Turkey ipeleke S-400 air-defense system yake huko Ukraine ili Ukraine iweze kujikinga na mashambulizi ya anga ya Russia.
Ktk kubembeleza huko, Marekani akamwambia Erdoğan kuwa akiipeleka S-400 Ukraine, Marekani itaondoa vikwazo ilivyoiwekea Turkey wakati iliponunua S-400. Pia Marekani ikamwambia Erdoğan akifanya hivyo, Marekani itamrejeshea Turkey program yake ya kununua pisi 100 za ndege za F-35 (ikumbukwe Turkey alikuwa ni mbia 'partner' ktk project ya kutengeneza ndege hizo za F-35, ali-fund hiyo project na alihusika ktk utengenezaji, ingawa aliondolewa ubia baada ya kununua S-400 ya Russia)
Pamoja na ahadi zote ikiwemo kuuziwa hiyo midoli 100 ya F-35, Turkey amekataa kuitoa S-400, mfumo makini na bora zaidi wa Ulinzi wa anga.
Mwambieni Marekani apeleke ma-vyuma vyuma yake chakavu (THAAD, Patriot PAC-3 n.k) Ukraine ikalipuliwe yote na Russia, watu hawataki ku-sucrifice S-400 ya Russia (USD milioni 300) kwa kupewa midoli 100 ya F-35 (jumla: USD triloni 7.8 ! ,midoli ambayo imeweka rekodi nzuri sana ya ku-crush hovyo hovyo kila mwaka).
View attachment 2168229
Sorry Mimi nilikuwa namjibu mdau mmoja aliyekataa kuwa moja ya malengo ya Russia siyo regime change(kumtoa Zelensky na serikali take).MKUU
PUT IN na wenzake waliutumia msemo ule ule wanaoutumia wamagharibi waloutumia kwa SADDAM HUSSEIN wakampaka matope ama wakampa jina baya kuhalalisha mauaji waloyafanya
RUSSIA sio kwamba kama angeamua kuivamia UKRAINE bila sababu angeshindwa hapana angeweza nahakungekua nawakumzuia si US si EU si UN si NATO siyeyote
ila kaamua kutafuta sababu ili hata wengine wapate kumtetea ama kua nyuma yake nakweli kwenye hizi sababu ziwe zauongo ziwe zakweli kapata wafuasi wakutosha kuanzia mtu mmoja mmoja huku KINTIKU jf mpaka taasisi ama mataifa makubwa makubwa angesema tu kama kaamua kuivamia UKRAINE bila yasababu watu wasingemuelewa
lengo kuu kuu kuu kabisa la RUSSIA ni UKRAINE kutokujiunga nakua naukariba na NATO yeye majamaa hata wakiwemo EU maadam hawapo NATO kwake sio kitisho nandio maana akawatwanga
kwenye hii vita kwa 100% UKRAINE ndio mshindwa sababu kukishakua na neno VITA kufa na hasara za majengo inakua kawaida kwapande zote ingawaje hapa kwenye kufa kote wamekufa ila kwenye majengo UKRAINE ndio kapoteza mpaka jana kama habari za kweli kufanyia repair ile nchi inahitajia Trillion 1100s
tukija kwenye masuala mengine yale alokua anakataa UKRAINE awali yakafanya aingie vitani hayo hayo kaja kuyakubali angeyakubali haya kabla yakumwaga damu ingekua simple tu tena kubwa nchi yake inaenda kumegwa
nawasilisha pia MKUU nakubali kutokukubaliana
Mkuu punguza hasira na jaziba hapa tunajadiliana na hatufokeani.Bwana wewe si mtoto, usilete hapa hoja za kitoto. Ukitaka kushiriki hapa, jielimishe!!
soma Moscow Times: 12 National Guards Appeal Dismissal For Refusing To Invade Ukraine - The Moscow Times
Askari 12 wa National Guard wa Urusi walikataa kwenda Ukraine maana sheria ya ajira yao inasema kazi yao ni kutetea Urusi, si kuingia nchi nyingine. Wako mahakamani sasa wakipinga kuachishwa jeshini.
Pia katika sheria ya kimataifa mambo yamebadilika tangu 1945. Majenerali Wajerumani walihukumiwa kwa jinai za kivita, sheria kimsingi haikubali tena kutekeleza amri yoyote kama ni dhahiri si halali.
Ninajua pia kwamba utaratibu huo unapuuzwa mara nyingi hadi leo, lakini ni angalau misiningi ilianza kuwekwa.
Halafu usitangaze porojo eti ninachukia Urusi. Unajuaje? Kwa sababu nampinga kiongozi mbaya anayeingiza nchi yake katika vita na umaskini mimi nachukia taifa hili kubwa lenye watu wengi wazuri? Waliochangia mema mengi kwa utamaduni wa Dunia?
Tafadhali, washa akili kabla ya kuandika. Naamini unayo ila siasa kali inaweza kuzimisha.
Mkuu hapana kabla ya vita aslimia 65 ya mkoa wa Dombas ilikuwa chini ya serikali ya Ukraine.Sorry Mimi nilikuwa namjibu mdau mmoja aliyekataa kuwa moja ya malengo ya Russia siyo regime change(kumtoa Zelensky na serikali take).
Pia majimbo hayo mawili UKraine angepata tabu kuya-control maana mpaka vita inaanza sehemu kubwa nilikuwa inamilikiwa na wwasi.
Nakukumbusha baadhi ya sababu za kuanzisha vita ni neo Nazi (regime change +nationalists-Azov militants),Demilitarization(including NATO ,remilitarization to Conquer Two territory Donbass)..
So fanyia kazi hivyo utanielewa na utajua either Russia katimiza malengo yake ,na kama hivyo ni yote na kama yote kwa kiwango gani %? Na he Ukraine ka-lose ,kama ndio kwa katika nyanja ipi? Na kiwango gani!
Kaka amka, acha ndoto.Hadi sasa tatizo la Ulaya si njaa, ni unene wa kupindukia.Huko Ulaya Hali inazidi kuwa tete.Hakina gesi,hakuna mafuta,hakuna uzalishaji.
Kichwa kimoja TU Cha VVP kimevuruga vichwa karibu 35 yaani vichwa vya NATO 30 plus vichwa kama Japan,Korea kisini,Finland,Taiwan na Norway.
OK thanks kwa kunisahihisha!Mkuu hapana kabla ya vita aslimia 65 ya mkoa wa Dombas ilikuwa chini ya serikali ya Ukraine.
Nisamehe lakini picha yako ya utaratibu wa kijeshi na sheria ya kimataifa ina mapengo makali. Usipuuze sheria maana ndani ya nchi inakupa usalama (na hapo jitihada za kuimarisha sheria - mfano kuzuia polisi kukamata watu hovyo na kuwatesa).Mkuu punguza hasira na jaziba hapa tunajadiliana na hatufokeani.
Hiihii Urusi inayo ongozwa na dikteta kwa mujibu wako ndio wana jeshi wagome kwenda vitani na waachwe bila ya kupewa kesi ya uhaini?maana hata Marekani baba wa demokrasia huwezi thubutu kukataa amri ya mkuu wako wa jeshi.
Lini watu wenye mitazamo ya kimagharibi mkampenda Putin ? Putin ana kubalika na wananchi wake kwa zaidi ya aslimia 75 wewe ninani mpaka umuone ni kiongozi asiye faa?
Eti una mchukia kwa kuitia nchi umaskini ww maisha ya warusi yana kuhusu nn mpaka huumizwe na ugumu wao wa maisha ?ww kwenye nchi yako isiyo kuwa na vikwazo vya wamagharibi maisha ni rahisi sio?
Na rudia tena katika maisha yako jifunze kucheza mbali mno na maslahi ya wenye nguvu ili ubaki salama tofauti na hapo yata kukuta na wala hizi sheria hazita kusaidia kwa lolote.
Hapana, habari ni sahihi, Dombas ni mikoa hii miwili na kwa jumla 2/3 ilitawaliwa na serikali. Ni katika 1/3 ile kwamba jeshi la Kirusi liliwahi kuingilia kati 2014 na kuzuia hao waasi kufukuzwa.OK thanks kwa kunisahihisha..nahisi ni kuni mikoa miwili pale Donesky na Luhask( nahisi Lugask ndio ulimilikiwa kwa kiwango kikubwa na Waasi)
NILI SEMA HILI JAMBOsi walisema baada ya mazungumzo russia wametoa majeshi karibu kiev ? mbona sahivi kiev inachezea kichapo muda huu
Wachambuzi wa mambo wanasema putin hatakubali nchi yake iangamie kirahisi x2; kwahiyo akibanwa sana atainuke US Ili waende sawa1. Tutaona kama mwisho wa mapigano utakuja kweli. Isingekuwa ajabu kama Putin anataka kujipatia muda tu. Maana mwisho wa Aprili vijana wapya watalazimishwa kuingia katika huduma ya kijeshi; wale waliomaliza mwaka wanaweza kuajiriwa kama askari kamili. Ilhali Putin aliahidi kwamba hatatumia vijana kwenye kipindi cha huduma ya kitaifa, anakosa sasa askari wa kutosha. Jambo ambalo linasaidia kuacha mashambulio dhidi Kiev. Tuona kama atachukua nafasi ya kupata lakhi 1 wanajeshi wapya.....
2. hata kama wanapatana kusitisha mapigano, swali litakalofuata litahusu pesa za Urusi kwenye benki za kigeni, nadhani kidogo zaidi ya nusu ya hazina ya Putin. Maana kufuatana na sheria ya kimataifa Urusi inapaswa kulipa fidia kwa uharibifu wote katika Ukraine. Mshambuliaji anatakiwa kulipa. Putin atakataa, na hapo nahisi hatapata pesa yake.
Hayo yote yanaweza kuweka msingi wa kuanza upya...
Acha akili za kitoto usionyeshe ujinga wako.Bwana wewe si mtoto, usilete hapa hoja za kitoto. Ukitaka kushiriki hapa, jielimishe!!