Special Thread: Yanayojiri Mgogoro wa Ukraine na Urusi. Nini chanzo na hatma ya mzozo?

Hawa waajemi ni noma aisee one step at a tume wanatoboa vikwazo
 
Kama kuna watu wana enjoy kuhabarika basi ni wale wanaofatilia siasa za nje mbali ya aina silaha gani zimetumika kwa nani kumpiga nani.

Again!

[emoji298]As reported by Hohols[emoji298]

#Analysis
It should be understood that as soon as Turkey becomes a gas hub, the Ukrainian GTS will immediately cease to have its value.
I must say thanks to the Turks, they take advantage of the situation and simply take the last money cases from Ukraine to themselves. Cool allies.

[emoji2772] Hapo kinacho zungumziwa ni issue ya Turkey kua International Gas Hub for Europe. Hizi Geopolitics are confusing ila ukizielewa unachekelea sana!
 
RUSSIA kupinga hili suala haliondoi ukweli kwamba walilipanga nandio maana wakalitekeleza

Suala la RUSSIA kuingia kijeshi UKRAINE baada ya yale yalokua yanaendelea baina ya hayo mataifa mawili yalikua wazi kwamba kuna mtu anaenda kupigika

US toka hio miezi wanasema kua RUSSIA wanaenda kuvamia UKRAINE wangekua majasusi wamaana(sipingani na uwezo wao waufanyaji kazi hapana)ila kama wangesema SVO itaanza tarehe fulani ila kwahali ilokua inaendelea pale ilikua inajulikanika lazma mtu anaenda kupigwa ila lini ikawa siri ya KREMLIN hili lalini jamaa anapigwa hata PENTAGON hawajalisema walisema tu kama kuna vita bas

Kuhusiana na namna ya kuendesha OP nyie ndio mnataka iende mnavyotaka nyie wakat wao wanataka iende wanavyotaka wao

Mnataka air superiority ipi wakat drones za RUSSIA zinazagaa na zinapiga lengo tena hapo hapo mji mkuu wa KIEV

Utataka kulinganisha walichofanya US au NATO pale LIBYA IRAQ nk

Tukiwaambia kama msaada anaopewa UKRAINE hakuna taifa lolote limepewa tokea iumbwe DUNIA likiwa vitani na eidha US ama RUSSIA mnabadilisha maneno

Kuhusiana na suala la RUSSIA vs US unataka wapigane unavyotaka wewe kama wametokea kupigana hakuna ulazima wakutumia meli wala nn kwa US ama RUSSIA wawili hawa wakiingia vitani yaani usitegemee NATO wakapigana na RUSSIA wakapeleka jeshi lao kwenye ardhi ya RUSSIA na kinyume chake hili sahau MKUU tena sahau kabisaaa

Kitakachotokea hapa si US wala RUSSIA watataka wamalizane atakae kufa afe wakubaki abaki mambo mengnr yaendeleee

Suala lenu la ambush na attack cjui invasion hilo nimewaachia wenyenu mie mtazamaji tuuu
 
Kwamba hukusikia MKUU hao wa UKRAINE wenyewe wanalalamikia kuhusiana na hizo Drones za TURKEY

Mpaka wanalumbana na wakuu wahio kampuni kwamba wamewapiga

Tukija kwenye hizo Drones za IRAN kwamba hujasikia hao wakubwa wanavyolaani na kuiekea IRAN vikwazo kwamba inaingilia ama kujihusisha na wanayoiita vita wakat wao wameto vingapi HIMARS JAVELIN HAWK leo IRIS nn cjui

Ila wameshtushwa na Drone za IRAN ila wewe unazibeza

ISRAEL anaombwa msaada akapeleke awasaidie UKRAINE unapokataa kuwasaidia wanaoonewa kwahakika unaungana na mvamizi
 

Akili yako imejazwa propaganda za kirusi ambazo zimejaa ujinga. February 24,2022 wakati anavamia Ukraine lengo lilikuwa kuupindua utawala uliopo aweke Maliki anaotaka yeye bahati mbaya sana alipiga mahesabu yake vibaya .Askari wake waliweza kuingia Mjini Kiev walipata mkong'onto wa kutosha kutoka majeshi ya Ukraine askari wa Russia wengi walikufa ndipo Putin kaamuru kuyaondoa majeshi yake kutoka Kiev baada ya kipigo hicho ndipo Kanzaga kupeleka majeshi yake huko mashariki na kusini mwa Ukraine kwenye mini ya Kharkiv,Luhansky,Donesky,Zaporizhzhia na Kherson Mwezi September Ukraine ilianzisha Operation Counter-Offensive iliweza kuyashinda majeshi ya kivamizi kutoka Russia kwenye miji mbalimbali ya Ukraine na sasa mashambulizi nayo ya Ukraine yamelengwa kwenye Miji ya Luhansky,Donesky,Zaporizhzhia na Kherson ambako sasa hivi Russia anapata taabu sana na Askari wake wengi kuuwawa na majeshi ya Ukraine.Ni uongo wa kijinga na kipumbavu mtu kudai eti Putin hakuna na haja kuuteka Mjini mkuu Kiev Huo ni uzuzu sema tu alipozidiwa na Askari wake wengi kuuliwa alibadirisha Gia angani na kuelekea mashariki na Kusini mwa Ukraine ambako mpaka sasa anapigwa vibaya sana muda Wowote Kherson itakombolewa.

Putin alitangaza pia kuwa eti anataka demilitarise Jeshi la Ukraine hayabagui sasa miezi 8 imepita bado anahangaika na kuua raia,Kuharibu majengo yao na Kuharibu miundo-mbinu ya kiraia kitu ambacho ni War-Crime.Amekimbia huko Mstari w Miele anaenda Kwa raia wasio na silaha huu ni woga kabisa.Huko Kherson wanajeshi wake wanapiga vibaya sana ameshindwa kuwasaidia Kwa lolote.
 
Mtu mwenye akili timamu hawezi kushabikia uvamizi dhidi ya nchi hambayo haikuwai kurusha hata jiwe kwenye mipaka ya nchi vamizi,

Sent from my Infinix X660B using JamiiForums mobile app
Russia hawawezi kukurupuka kuvamia Ukraine huku wakijua kuna gharama.mimi sishabikii vita ila ninauhakika warusi wapo sawa Kwa maamuzi yao
 
Mkuu, Iran inatumia drones zenye GPS, rejea kusoma vizuri hiyo GPS nimeitaja wakati nazungumzia nini.

Russia wako nyuma kwenye drone technology ndio. Taja drones 3 the best za Russia nikutajie drones tatu tatu kutoka Israel, US, China, Turkey zinazozidi hizo za Russia. Kwani Iran angeleta drones kama Russia anaweza
 
Kwamba Ukraine imelalamikia hizo drones, zina uwezo mdogo au nini mkuu.

Sasa kumbe Russia inashindwa kuzuia drones zenye uwezo mdogo mpaka waliozinunua wanalalamika ila Russia yenyewe inateswa nazo.
Snake island hapa air defence system iko hapo hadi kwa camera inaonekana ila imedumaa tu

 
Mkuu kilicho badilika ni jina na ukubwa wa mipaka tu kutoka Soviet Union kuwa Russian federation ila uwezo na nguvu bado ni ule ule.

Kama ilivyokuwa Soviet union inaogopeka nisawa tu na Russia inavyo ogopeka sasa, mifano hai ipo mingi sanaa nadhani kila mtu anaona kila siku jinsi nchi zaidi ya 30 zilizo ungana kijeshi zikitamka wazi kuwa hazipo tayari kuingia vitani na Urusi (utadhani siyo wao walio ilipua Yugoslavia na libya) pia nadhani wote tunaona yanayoendelea pale Ukraine siyo USA, NATO, EU wala UN ambae anaweza kuithibiti Russia pale Ukraine kufanya mambo yake zaidi ya kupiga makelele tu nje.

Pia nadhani nguvu ya ushawishi ya Urus kwa mataifa mengi duniani ipo dhahili, haihitaji hata kuwa na phd kulitambua hilo (Achana na makaratasi ya UN yasiyo ni effects kwa USA na Russia). Soviet union ilikuwa na uwezo wa kujiamulia mambo yake yenyewe na ikayatekeleza bila kuingiliwa na mtu yeyote, the same thing kwa USA na Russia wote hao asilimia kubwa ya mambo yao hata UN haiwezi kuyaingilia zaidi ya kupiga umbeya tu pale New York, Mifano ipo mingi sanaa kama USA kuivamia Iraq, USA kumega eneo la Cuba na Mexico, Russia kuivamia Ukraine, Russia kumega eneo la Georgia na Ukraine na n.k, huku UN ikibaki kubweka tu bila kufanya chochote.

Ok tusichoshane sana najua wewe ni muelewa, pia najua unajua Russia ndo taifa tishio kwa USA kama ilivyokuwa Soviet union kwa USA huyo huyo. Pia najua unajua kuwa USA hawezi kupigana vita ya moja kwa moja na Russia kama ilivyokuwa kwa Soviet union.

Kiufupi ukiachana na mahaba binafsi, Nguvu ya Soviet union ni copy and paste ya nguvu ya Russia hata USA analijua hilo ndo maana anahangaika kila kona ya dunia kuiangusha Russia ili apumue na kutimiza mipango yake ya ovyo juu ya hii dunia lakini ameshindwa na anaendelea kushindwa.

Soviet na Russia ni "like father like son" ni ngumu kuwatofautisha kimuonekano zaidi ya kutumia tofauti ya umri wao.
 
[emoji1255] [emoji635] - Russia now see the "de-satanization" of Ukraine as a war aim.
Mkuu, pamoja na Iran? Nikielewa vema Iran ni hodari sana kupambana na shetani. Tutumaini tu kwamba kati ya Wakristo Waorthodoksi na Waislamu Washia waelewane kuhusu shetani (ambayo si kazi ndogo - nisipokosei wasingeelewana kuhusu Mungu, labda ni rahisi zaidi kuhusu kinyume?)
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…