Spika Tulia Ackson: Mtu akimsema vibaya Rais nyooka naye, akinisema vibaya Nyooka naye

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2012
Posts
5,108
Reaction score
10,191
Wakuu nawaletea kideo, spika wa bunge akiwataka vijana kushughulika na yeyote anayemsema vibaya Rais, Mbunge, Diwani au Mwenyekiti wa mtaa kwa tiketi ya CCM.

Hivi karibuni kuna ndugu wa Temeke alisema wao kazi yao ni kuwashugulikia wakosoaji na wazee watawaombea radhi kwa watanzania.

Sijui nataka niseme nini ila pateni kideo hapo.

========

Akihutubia Vijana wa CCM katika Jimbo lake, Mbunge wa Jimbo ya Mbeya Mjini ambaye pia ni Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania amewataka vijana wa Jimbo hilo kutoshiriki katika Kumsema vibaya, Rais na Viongozi wa Jimbo hilo

Amesema, “Isitokee Kijana yeyote anaungana na mtu yeyote anayemsema vibaya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Rais Samia ni Rais wa Nchi lakini pia ni mwenyekiti wa Chama chetu. Asitokee mtu yeyote wa Nje ya Chama, wa Ndani ya Chama akawa anamsema vibaya Rais halafu wewe ukamtazama, shughulika naye, CCM hoyeeeee”

Ameendelea, “hata mimi Mbunge wako akiwa ananisema vibaya nyooka naye, unajua sababu ni nini? Hata Diwani, Madiwani wote wa Mbeya Mjini sasa hivi ni CCM, hata akimsema vibaya Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa, na yeye ni CCM, nyooka naye’
 
Hao vijana waitike tu ila tutawanyoosha, kiongozi anayeogopa kusemwa ana mapungufu ambayo hapendi aambiwe
vijana wanajazwa ujinga halafu ndo wa kwanza kulalamika ohh hakuna ajira,mara mitaji nk lkn leo wanapiga makofi kujazwa upuuzi.je vijana watatoboa kweli kwa mtindo huu.ndo maana leo naamini vijana ni taifa la kesho.
 
Akihutubia Vijana wa CCM katika Jimbo lake, Mbunge wa Jimbo ya Mbeya Mjini ambaye pia ni Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania amewataka vijana wa Jimbo hilo kutoshiriki katika Kumsema vibaya, Rais na Viongozi wa Jimbo hilo

Amesema, “Isitokee Kijana yeyote anaungana na mtu yeyote anayemsema vibaya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Rais Samia ni Rais wa Nchi lakini pia ni mwenyekiti wa Chama chetu. Asitokee mtu yeyote wa Nje ya Chama, wa Ndani ya Chama akawa anamsema vibaya Rais halafu wewe ukamtazama, shughulika naye, CCM hoyeeeee”

Ameendelea, “hata mimi Mbunge wako akiwa ananisema vibaya nyooka naye, unajua sababu ni nini? Hata Diwani, Madiwani wote wa Mbeya Mjini sasa hivi ni CCM, hata akimsema vibaya Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa, na yeye ni CCM, nyooka naye’

Tulia ni Spika makini bungeni.
 
Back
Top Bottom