Spika Tulia Ackson: Mtu akimsema vibaya Rais nyooka naye, akinisema vibaya Nyooka naye
Mauji ya Kimbari hayakutokea tu bahati mbaya ila kulikuwa na Viongozi wenye akili mbovu kama za @TuliaAckson walikuwa wanahubiri uhasama na kuwajaza Vijana chuki mwisho wa siku wakawachinja ndugu zao, jiulize kama Tulia anasema vile hadharani akiwa sirini anawaambia nini Vijana?
 
Wakuu nawaletea kideo, spika wa bunge akiwataka vijana kushughulika na yeyote anayemsema vibaya Rais, Mbunge, Diwani au Mwenyekiti wa mtaa kwa tiketi ya CCM.

Hivi karibuni kuna ndugu wa Temeke alisema wao kazi yao ni kuwashugulikia wakosoaji na wazee watawaombea radhi kwa watanzania.

Sijui nataka niseme nini ila pateni kideo hapo.
View attachment 2375676

========

Akihutubia Vijana wa CCM katika Jimbo lake, Mbunge wa Jimbo ya Mbeya Mjini ambaye pia ni Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania amewataka vijana wa Jimbo hilo kutoshiriki katika Kumsema vibaya, Rais na Viongozi wa Jimbo hilo

Amesema, “Isitokee Kijana yeyote anaungana na mtu yeyote anayemsema vibaya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Rais Samia ni Rais wa Nchi lakini pia ni mwenyekiti wa Chama chetu. Asitokee mtu yeyote wa Nje ya Chama, wa Ndani ya Chama akawa anamsema vibaya Rais halafu wewe ukamtazama, shughulika naye, CCM hoyeeeee”

Ameendelea, “hata mimi Mbunge wako akiwa ananisema vibaya nyooka naye, unajua sababu ni nini? Hata Diwani, Madiwani wote wa Mbeya Mjini sasa hivi ni CCM, hata akimsema vibaya Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa, na yeye ni CCM, nyooka naye’
Kati ya watawala wajinga ni pamoja na huyu bibi
 
Back
Top Bottom