Suala la ajira linazidi kuwa janga Tanzania

Elimu ya form 4 inamtosha mwanadamu kujiongeza
 
Kila mtu anapenda kujiajili lkn changamoto ya kujiajili bila pesa ni mzigo wa mavi mkuu kama kwel serikali ni ya wanyonge ijenge mazingira ya muhitimu yeyote iwe certificates au diploma na kuendelea wapewe fursa nchini ata kama sio pesa mana pesa itakua ngumu bali kupitia vyeti vyao TRA wangeomba vyeti vyao viwe vielelezo vya kujiajili bila makato ya kodi kabs na kupewa unlimited time mpk akuwe kimtaji na kampuni yake kwa kiwango cha muwekezaji wa kiwango fulani na serikali kuwapatia wataalamu ikiwezekana mi naami elimu yetu ni nzur tu ila muhitimu ajaona matunda kwenye kujiajili na wepesi wake mwanzon zaid ya kusimuliwa na kufanya research zake na kuona shida yake mana ana akili ya darasan ya kutambua changamoto mapema ila naona serikali za africa zinaigana utaratibu wake kwenye uongozi tusibeze elimu tu na mazingira pia ya muhitimu ndo majanga zaid mtt anapata elimu ya chuo mamilioni toka kwa mzazi labda kama kasoma kuanzia certificate hadi diploma au mpk degree kwa milioni zaid ya 8 alafu mzazi tena atoe mtaji wa milioni 8 jmn serikali iwe na huruma hapo kodi mil na ushee bado biashara kufanana mana idadi ya watu na mtaji mdg lazima idea zifanane serikal iangalie namna ya kufanya zaid hata kuchukua watu kuajili bado wataalamu wengi upotea mtaan ambao wangetumika vizur wangezalisha ajira zaid
 
Na nafikiria kitu kimoja hii hali ingeweza kumtisha jpm hivi tunavyoelekea uchaguzi angalau apunguze tatizo kwa sehemu ila wapi!

Sasa akipita hiyo 2020 si ndio hataajiri mtu hata mmoja!

Lakini Vijana tubadilike kimawazo na mtizamo unakuta graduate wako kwenye groups za wasap kujadili ujinga tu siku nzma!
Zaidi zaidi ukiwaambia Jamani tujifunze ata ufugaji wa kuku tu wanakuona mshamba na una mambo ya kizee!!
 

Hongera sana! umekuwa mzazi wa mfano kati ya wengine wengi! Ni jambo la maana sana kumsomesha mtoto na wakati huo huo kumpanua kimawazo kwamba anaweza kufanya jambo jingine, na sio kumjengea akilini kwamba asome ili aajiriwe. Angalia mawazo ya wengine humu ni ajabu kabisa... mtu anaona kwa kuwa kasomea mambo ya afya basi ni lazima aajiriwe hospitalini na hatakiwi kufanya kitu kingine zaidi ya kusubiri ajira! Wakati alitakiwa ajiongeze tu kwamba pamoja na afya ya huyo binadamu kuna mengi yanayomzunguka ambayo yangempa fulsa ya kufanya zaidi ya afya. Mwisho wa siku ni kulaumu serikali kwa nini haiwaajiri...mweeh tujiongezegeeeee
 

Kuna wajinga wengi sana na wewe ndio kilanja wao humu. Hivi unajua ni watu wangapi wamesomea Udaktari, Unesi na vya jamii ya hivyo??? sasa wote hao ni lazima waajiriwe??? kwa fungu lipi???? na kama serikali imeshindwa kuwaajiri unafirikia ni kwa nini? Jiongezeeeee Zama zimechange! kama ulifikiri kusomea unesi ndio lazima utaajiriwa umenoaaaa geuza shingilingi na uwaze upya nini kingine kifanyike zaidi ya kuajiriwa! Kadiploma tu ka famasist kanakufanya upayukeeee na kutukana watu humu! Kuna watu wana degree zaidi ya tatu na wanajishughulisha bila kuajiriwa... wewe kalaga baho subiri ajira.... piga keleeee kama chizi
 
Ni kukubariana na hali tu, kiongoz wapumbavu
Na life linakua just like that
 
Kadiploma tu ka famasist kanakufanya upayukeeee na kutukana watu humu!
Ulijuaje nina kadiploma ka tu ka famasist. Hili tu linakuondolea uhalali wa yote uliyoandika hapo juu kuwa huna chochote kichwani.
Wewe ngoja tu nikuweke akiba kwa hapo, kwa sababu siwezi kupoteza muda nawe asiyeweza hata kufundikisha. Kama umetumwa kwamweleze aliyekutuma kwamba nimekudharau na yeye pia namdharau hivyo hivyo. Sasa ngoja nikamwone bosi wako.
 

Wewe ndio hufundishiki.... usiyeweza kujiongeza. Tuliza ubongo wako usubiri kuajiriwa eeeee ndio unalotaka kuambiwa!!! Usiyetaka kubadilika... bakia na hilo lililojaa ubongoni mwako. Aliyenituma kaniambia eti umedumaa akili.... ebooooo acha kukariri maisha weweeeeeee!
 

Mtu anapokwenda kusomea digrii ya udaktari, ameamua kufuatana na uwezo wake aliojaliwa kuwa hiyo ndio kazi atakayoifanya, iwe kwa kuajiriwa au kwa kujiajiri.

Wewe hujui taratibu zilizopo katika aina hii ya kazi. Hakuna njia yoyote mtu huyu anayoweza kujiajiri mara tu baada ya kuhitimu katika masomo ya kazi hiyo. Itamlazimu apate ajira, iwe kwenye sekta binafsi au serikalini kwanza ili atimize matakwa ya kuwa na uzoefu wa kujiajiri mwenyewe; na pengine hata kupata mtaji.

Kwa hiyo huwezi kuondoa jukumu kwa serikali katika kumsaidia huyu mtaalam ili aweze kuendelea katika nyanja yake aliyosomea.

Na hapa ninaposema serikali kuwa na wajibu, sina maana moja tu ya kumpatia ajira. Serikali inazo njia mbalimbali za kuwezesha.

Mathalani: Serikali inaweza kuweka tu sera zinazoweza kutumika ili kada ya hawa watu isiongezeke bila mpangilio. Ni serikali hiyo hiyo inao uwezo wa kuwawezesha waliopo kwenye sekta binafsi katika nyanja hizi wawe na uwezo zaidi wa kuwahudumia waTanzania kwenye sehemu hii ya taaluma, hawa wakiwepo wa kutosha, watatoa ajira kwa hao wapya wanaoingia kabla na wao hawajafanya mipango ya kujiajiri.

Tanzania bado tupo chini sana katika uwiano wa Daktari na wagonjwa anaowahudumia. Kwa hiyo uhitaji wa wataalamu hawa bado upo mkubwa sana. Kuwaacha wakazagae mitaani ni kukosa mipango mizuri ya kuwatumia.

Wewe kwa kutojua unachokizungumzia unataka hawa watu wakajiajiri, hata kama ni kwenda kuchuuza mayai mitaani. Naomba unipe mfano mmoja popote duniani ulipowahi kuona hayo!

Majoto, sina lazima ya kubishana na wewe. Nimekuelewa tokea kwenye mchango wako wa mwanzo ulivyokuja na 'joto'.
 
Mjinga wewe! Soma nilichoandika na kuelewa. Unaweza soma kada ya Afya na bado ukajiajiri/ukafanya shughuli nyingine tofauti na afya. Tatizo umekariri kuwa ukisoma afya lazima ufanye afya. Jiongeze!
Jaribu kufikiria kusoma MD sio swala rahis kama unavyodhani ww 5 yrs + 1 yr intern unategemea mtu kufanya kazi tofauti na za sekta ya afya???? usifananishe MD na hizo degree za miaka 3
 
Magufuli kanyaga twende, mtapata tabu sana na kauli nyingine za kipuuzi kumtukukuza huyo dikteta wakati nchi inaangamia kiuchumi!!

Ama kweli mvunja Nchi ni Mwananchi.
 
Jaribu kufikiria kusoma MD sio swala rahis kama unavyodhani ww 5 yrs + 1 yr intern unategemea mtu kufanya kazi tofauti na za sekta ya afya???? usifananishe MD na hizo degree za miaka 3

Nakubaliana na wewe kabisa. Tatizo ni kwamba baada ya kusoma hata miaka 10 unajikuta ajira hupati. Tufanyeje sasa?? ndio tuanze kujipanga kwa kusoma bila kutegemea kuajiriwa. Ona hali halisi kuhusu ajira ilivyo kwa sasa, pamoja na kwamba watu wanahitajika lakini serikali inashindwa kuwaajiri kutokana na sababu mbalimbali, je tukae tuu tukisubiri ajira ambayo imekuwa ngumu? ni vema tukajiongeza kukabiliana na hali hii.
 
*Yametokea huko mwanza, mtu kaamua kujiua sababu amekosa kazi japo ana elimu ya chuo kikuu*
mwananchi.co.tz

Mwanza. Musa Ally (25), mkazi wa Kiloleli wilayani Ilemela jijini hapa anayedai wa kuwa na elimu ya chuo kikuu, amejirusha katika jengo la la Rocky City Mall na kufariki dunia.

Imeelezwa kuwa Musa alichukua uamuzi huo kutokana na kuwa na msongo wa mawazo, kukosa kazi.

Akizungumza na Mwananchi leo Ijumaa Desemba 21, 2018 kaimu kamanda wa polisi Mkoa wa Mwanza, Advera Bulimba amesema tukio hilo limetokea leo saa saba mchana.

Bulimba amesema kijana huyo alionekana akiwa amelewa kupita kiasi na tangu Desemba 16, 2018 na alikamatwa na kuwekwa kituo cha polisi Kirumba, kilevi kilipopungua aliachiwa.

Amesema katika uchunguzi wa awali marehemu alibainisha kuwa alikuwa na msongo wa mawazo kwa sababu ya kukosa kazi licha ya kuwa na elimu ya juu.

Bulimba amesema baada ya polisi kumuachia alikwenda kunywa tena pombe na baadaye kujirusha kutoka ghorofa ya tatu na kukutwa na pombe kali na ugoro.

“Uchunguzi wa awali umeonyesha kuwa kijana huyo amesema amejiingiza kwenye ulevi na asilaumiwe mtu yeyote. Amesema amechukua uamuzi huo yeye binafsi, pia akidai yeye ni masikini hana baba wala mama,” amesema Bulimba.

Amesema mwili umehifadhiwa hospitali kwa ajili ya uchunguzi zaidi licha ya kutotaja jina la hospitali hiyo.

Bulimba amesema, maandishi aliyokutwa nayo marehemu yalisomeka kwamba “yeye ana shahada sayansi ya kompyuta aliyoipata Chuo Kikuu cha Dar es salaam (UDSM).”
 
Tatizo kwa Tanzania sio ajira, tatizo ni elimu ya kujitambua. Kuanzia kwa baba hadi wajukuu - wanaojitambua ni wachache sana.
Jiulize ni wafanyakazi wangapi wapo nchini kutoka nje ya nchi?
 
Huyo fala tu; utu wake ni zaidi ya digrii alokuwa nayo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…