Suala la Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) na Vipengele kadhaa vya Kisheria

Suala la Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) na Vipengele kadhaa vya Kisheria

Tuangalie sheria na mantiki.

Tusiandike kwa hisia zinazoongozwa na jazba za kisiasa.

Magufuli anavunja katiba, sana tu.

Mfano, kupiga marufuku mikutano ya kisiasa ni kuvunja katiba wazi.

Katiba inatoa "right to assembly" wazi kabisa.

Hatuhitaji kutunga uongo kwamba Magufuli kavunja katiba kwenye suala la CAG.

Kutunga uongo kwenye hili kutafanya hata tunaposema kweli Magufuli anapovunja katiba kweli, tuonekane tunazusha uongo.

Kiranga, I have a surprise to you, Up to Five minutes ago I was seeing eye to eye with you, but I came accross the following subsection of the law detailing how the situation of not renewing the contract of CAG could be handled.

Let us reason together

I herewith attach the subsection.

Img-1572853035577.jpg


NI DHAHIRI KWA KIPENGELE HIKI CHA SHERIA MAGUFULI AMEVUNJA SHERIA NA UTEUZI WAKE WA CAG MPYA NI BATILI
 
Nimeshakujibu Raisi Hana mandate ya kumteua mtu for less than 5 years kwenye U CAG .Professor Assad kabakiza miaka miwili ya kufikia 60 ya kikatiba .Asingeweza kupewa 5 years huyo .Rais angekuwa kavunja katiba.Lakini professor Assad angekuwa na miaka 55 Raisi angeweza kumpa akafikia 60.Na akifikia 60 angeweza akitaka kumpa mingine Mitano afikishe 65 ya kuidhinishwa na ubunge .

Tatizo umri wa Assad umekaa vibaya hauingii vizuri kwenye katiba umekaa kishirikina
Angalau wewe una point ya msingi.
 
Mkuu tunakushukuru saana kwa kutuchambulia na kutufafanulia kwa uhakika kabisa na kisheria.kuhusu kutenguliwa kwa CAG na Mamlaka aliyonayo CAG
Sasa ndio tunazidi kufahamu ukweli upo wapi

Tuliambiwa kuwa Prfs Musa Asaad ametenguliwa kwasbb ya umri wake umefika mwisho.pia tukaambiwa kuwa ana umri wa miaka 60.Hio ndio ni sababu kuu ya kutenguliwa
Kumbe Prfs Asaad ana miaka 58..!!!
Hii ni Aibu ya wazi kabisa na inaonesha dhahiri kuwa panachuki binafsi baina ya viongozi wa Nchi hii[emoji2211]

Hapa hasa ndio siri ya urembo ilipo.
 
Mi sijaelewa mnapobishana mbona jamaa kajitahidi kutoa tafsiri ya kisheria kuhusu neno "Shall" kwa mujibu wa sheria zetu. Hizo quotation zako zote sijui kama umejipa muda wa kutafakari huku ukiunganisha na maana za kisheria. Tatizo lenu mnatoa tafsiri zenu kutokana na uelewa wenu wa lugha ya kiingereza. Sheria haiendi hivyo.

Unaposema katiba inasema The President shall be eligible for re-election. Maana yake "election" ndo ya razima. Ila sio lazima kuwa Rais hivyo kama hataki au chama chake hakijampitisha hakuna ulazima wa yeye kugombea tena, ila akitaka kuwa tena Rais ni lazima apitie ktk uchaguzi. Lakini pia awe eligible, eligibility ya Rais imetajwa tayari na katiba ktk ibara ya 39 na 40.

"Shall be eligible for renewal" hapo eligibility inayozungumziwa hapo ameshatoa tafsiri yake kuwa, kama hayupo eligible basi kuwe na uchunguzi. Yaani eligibility ya CAG haitokani na mtazamo wa mtu bali ni lazima uchunguzi, ufanyike kwa mujibu wa katiba. Otherwise kama hakuna uchunguzi ni lazima mkataba wake uwe renewed. Ndo maana ya hiyo sentence "shall be eligible for renewal"
Wewe unapotosha tu angalia hapa kwa Rais elligible for re-election na kwa CAG elligible for renewal (hapa napo renewal si automatic bwashe. Renewal ni subject to performance) Kitu kikubwa hakupata renewal anaondoka zake
 
Acha ujinga, asubuhi hii chukua hata simu mpigie mama/baba yako uwaambie unawapenda na uwatakie siku njema utabarikiwa zaidi, kwa maana siajabu hata mtoto wake haumizwi na kumpigania hivyo huyo Asadi kama wewe, labda hata washakubali matokeo na kumove on wewe mwenzangu na mimi bado unakosa usingizi, so sad!
Hoja hupingwa kwa hoja, wewe badala ya kuleta hoja kukanusha ya mtoa hoja umeamua kutukana, inasikitisha sana
 
Img-1572853035577.jpg


Kifungu hiki cha sheria ndo. kimekata mzizi wa fitina, Hiki kipengele kinasema kwamba kama Rais hatsmuongezea CAG mkataba mpya wa miaka mitano basi sababu za kutomuongezea lazima zifuate utaratibu uleule wa kumuondoa CAG ulioelezewa katika ibara ya 144.

Kwa hiyo, Uteuzi wa CAG mpya ni batili ni. kinyume cha sheria na CAG mpya siyo CAG halali kwa mujibu wa sheria
 
Wewe unapotosha tu angalia hapa kwa Rais elligible for re-election na kwa CAG elligible for renewal (hapa napo renewal si automatic bwashe. Renewal ni subject to performance) Kitu kikubwa hakupata renewal anaondoka zake

Mkuu kuna kifungu kingine cha sheria kinachoelezea sababu ambazo zinaweza kupelekea mkataba wa CAG usiwe renewed.

Hiki hapa:

Img-1572853035577.jpg
 
Acha ujinga, asubuhi hii chukua hata simu mpigie mama/baba yako uwaambie unawapenda na uwatakie siku njema utabarikiwa zaidi, kwa maana siajabu hata mtoto wake haumizwi na kumpigania hivyo huyo Asadi kama wewe, labda hata washakubali matokeo na kumove on wewe mwenzangu na mimi bado unakosa usingizi, so sad!
Mkuu hoja inapingwa kwa hoja sio kwa taarabu, mwenzako kaja na data wewe unampinga kwa kuimba taarabu kwama mwanamke wa Pwani!
 
Acha ujinga, asubuhi hii chukua hata simu mpigie mama/baba yako uwaambie unawapenda na uwatakie siku njema utabarikiwa zaidi, kwa maana siajabu hata mtoto wake haumizwi na kumpigania hivyo huyo Asadi kama wewe, labda hata washakubali matokeo na kumove on wewe mwenzangu na mimi bado unakosa usingizi, so sad!

Hapa Kaka umejibu kwa hasira badala ya busara. Jifunze kutoka kwa Kiranga alichoandika kujibu. Post baada ya hiyo yako.
 
Yasije mkuta Yale ya yule raisi wa Zanzibar nilokuja mjua baada ya kufariki alokua kizuizini kigambon
 
Nafahamu kwamba watu wengi wameanzisha threads wakijaribu kuelezea suala la CAG Kisheria! Hata hivyo, wengi wao kama sio wote walichofanya ni kurundika vifungu vya kisheria bila kutoa ufafanuzi!

Mbaya zaidi, hawatoi ufafanuzi wa matumizi ya neno SHALL kwa mujibu wa sheria zetu! Nimelazimika kuanzisha uzi huu ili kuondoa mapungufu yote hayo, na ni matumaini yangu kwamba uzi huu hamtaunganisha na nyuzi nyingine ili watu wapate kuelewa suala hili kwa ufasaha!

Tuendelee.

Bila kujaza vifungu vingi, Katiba yetu Ibara ya 144 (1) inasema wazi kwamba:-
Kwamba, CAG ATALAZIMIKA kuachia ofisi akifikisha miaka 60 au umri mwingine wowote utakaotajwa na sheria zilizotengenezwa na Bunge!

SWALI 1: Je, Profesa Mussa Assad amefikisha miaka 60?! Jibu HAPANA kwa sababu kumbukumbu zinaonesha amezaliwa Oktoba 06, 1961... kwa maana nyingine, atafikisha miaka 60 Oktoba 5, 2021.

SWALI 2: Je, Bunge limetaja huo UMRI MWINGINE WOWOTE?!

Jibu linapatikana kwenye Sheria ya Ukaguzi wa Hesabu za Umma, yaani Public Audit Act ya mwaka 2008, Ibara ya 6(2)(a) inayosema:-

Kumbe, Bunge likatunga sheria kwamba badala ya miaka 60, hatimae CAG ATALAZIMIKA kuachia ofisi akifikisha miaka 65. Tumeona Prof Assad ndo kwanza ana miaka 58.

SWALI 3: Nini hutokea CAG akimaliza miaka 5 ya kwanza?!

Hapa tena jibu linapatikana kutoka Public Audit Act 2008 Ibara ya 6 (1) inayosema:-Hapo kwenye neno SHALL ndipo panapozua mgogoro!!

Watetezi wa uamuzi wa Rais wanasema neno SHALL sio shuruti! Kwa bahati mbaya sana, tafsiri yao wanaitoa kichwani na sio kwa mujibu wa sheria zetu!

Kwa mujibu wa sheria zetu, na kwa kuangalia Interpretation of Laws Act Ibara ya 53 (1&2) inasema kwamba:-
Kumbe, kwa mujibu wa sheria zetu, pasipo na SHURUTI hutumika neno MAY lakini linapotumika neno SHALL, hiyo ni SHURUTI!

Kwa maana nyingine, Public Audit Act inaposema "...and shall be eligible for renewal for one term only. Hapo suala la renewal ni SHURUTI kama ilivyosema Interpretation of Laws Act 53 (2).

Itakuwa sio SHURUTI either kama ameshafikisha miaka 65, au kama ambavyo 2008 Public Audit Act Ibara ya 6(2)(a) inavyosema kwamba:-Kwa maana nyingine, kwavile Prof Assad hajafikisha miaka 65, hapo tafsiri yake ni kwamba AMETUMBULIWA na sio kwamba muda wake umeisha!!

Na CAG atatumbuliwa "...Unless the question of removal becomes the subject of investigation in terms of Article 144(3) of the Constitution."

Hiyo Ibara ya 144(3) ya Katiba yetu inasemaje? Jibu ni hili:-If the President considers that the question of the removal of the Controller and Auditor-General from office under the provisions of this Article needs to be investigated, then the procedure shall be as follows:Kama tulivyoona hapo juu, CAG atalazimika kuachia ofisi endapo atakuwa amefikisha miaka 65, kinyume chake anaweza KUTUMBULIWA kabla ya huo umri ikiwa ametenda jambo linalohitaji investigation.

Hivyo basi, ni ama Rais atengue uamuzi wake wa awali wa kuteua CAG mwingine, au tuone akiunda Tume ya Kijaji ya Kumchunguza CAG kwa kosa analojua yeye na timu yake!!

CAG akiongezewa miaka mingine 5, ataimaliza akiwa na umri wa miaka 63... umri halali kwa mujibu wa Sheria ya Ukaguzi wa Hesabu za Umma ya mwaka 2008!!
[/QUOTE]Kama tafsir ya 'shall'n lazima ktk muktadha tajwa
Bx hili likatiba halina budi kusema waz kuwa cag anatakiwa kuhudum kwa miaka kumi

Badala ya kutuumiza kichwa na 'shall' nyiiiingi mara "maaaaaaaaaay"
 
Wewe unapotosha tu angalia hapa kwa Rais elligible for re-election na kwa CAG elligible for renewal (hapa napo renewal si automatic bwashe. Renewal ni subject to performance) Kitu kikubwa hakupata renewal anaondoka zake
Nani ana measure hiyo performance? Wapi imeandikwa? Usijitungie tu kutoka kichwani kwako. Kama CAG akishindwa ku-perfom hiyo ni subject to investigation. Lazima uchunguzi ufanyike kwa mujibu wa Katiba.

Usijilazimishe kutokuelewa ndugu yangu.
 
Nani ana measure hiyo performance? Wapi imeandikwa? Usijitungie tu kutoka kichwani kwako. Kama CAG akishindwa ku-perfom hiyo ni subject to investigation. Lazima uchunguzi ufanyike kwa mujibu wa Katiba.

Usijilazimishe kutokuelewa ndugu yangu.
Bunge lishamkataa kufanya kazi naye umesahau?
 
Back
Top Bottom