Umeeleza vizuri mwishoni umejichanganya, rais wetu amevunja katiba waziwazi.Assad alipaswa kustaafu 2024 kama rais asingetaka kumuongezea miaka mitano ya ziada iliyowekwa Na katiba, Na hiyo ya nyongeza anapaswa kumuongezea MTU asiyezidi 65 years.
Naomba unukuu maneno ya katiba yanayoonesha rais kavunja katiba.
Katiba inasema CAG hawezi kuongezewa muda baada ya kutumikia serikali kipindi cha pili.
Mwisho wa utumishi wake kama CAG ni miaka 10.
Baada ya miaka 10 hatakiwi kuongezewa muda tena kwenda kipindi cha tatu.
Katiba haijasema CAG akitumikia kipindi cha kwanza cha miaka mitano, ni lazima aongezewe mkataba kwa kipindi kingine cha miaka mitano.
Hivyo rais, ana haki ya kutoongeza muda wa CAG baada ya kipindi cha kwanza cha miaka mitano, kwa sababu yoyote au bila sababu.
Bila ya kuvunja katiba.
Na kama unafikiri kuna sehemu katiba imevunjwa, weka hiyo sehemu hapa tuichambue.
Mimi sipendi uongozi wa Magufuli. Sipendi kwa mfano ATCL ilivyoenda kisiasa na CAG akakatazwa kukagua vitabu vya kihasibu. Assad alikuwa CAG mwenye msimamo, na inaonekana anaondolewa kwa sababu ya msimamo wake.
Lakini, katika hili la Assad kuondolewa, hakuna sehemu ambapo katiba imevunjwa.
Sipendi utawala wa Magufuli kwa sababu unavunja katiba mara nyingi.
Marufuku ya mikutano ya siasa ni kuvunjwa kwa katiba. Magufuli kavunja katiba hapo. Let's call him out on that.
Lakini hii habari ya Assad kuondolewa hakuna sehemu katiba imevunjwa.
Kama unafikiri kuna sehemu katiba imevunjwa, tujadili katiba imesemaje neno kwa neno.